Ujinga ni hali ya kutojua kitu fulani, sasa kwa watanzania sio kua hawajui, wanajua ila wanafanya, so hapo huwezi kuwaita wajinga.
Mfano wako wa uchafu barabarani sio kua hawajui kua uchafu utupwe wapi ila wanapuuza kutupa sehemu sahihi, huwezi waita wajinga hawa ni wapuuzi.
Ndio maana ukiweka sheria unaweza hata usiwaoneshe pa kutupa ila uchafu hawatatupa hovyo, ni kua wanajua ila kibri na kujisahaulisha.
Sio kua hajui wanasiasa na chawa wanamdanganya, anajua ila anaishi kinafki kwa maslahi yake binafsi, huyu sio mjinga(maana anajua analofanya ni kosa ila analifanya kwa manufaa yake).
Anajua kiongozi fulani ni fisadi ila anaogopa kumuweka hadharani akijua fika kumuweka hadharani kutamuweka matatani kiongozi na yeye pia. Huyu pia sio mjinga ila ni muoga.
Tumia maneno sahihi wakati sahihi mkuu, unataka kuelimisha wasomi ilhali na wewe unapaswa kuelimishwa.
Labda useme una uhaba wa misamiati ya kiswahili, kama umeshindwa kabisa basi tumia hata majina ya wanyama au wadudu wenye tabia za hovyo kama kupe, nzi nk.