Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani

Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani

Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa mila na desturi tuna namna bora ya kuheshimu wakubwa wetu kwa umri ama madaraka waliyonayo. Tusilete umagharibi kisa uhuru wa kusema chochote. Moja ya tunu zetu kama taifa ni kuwa na utu.

Hii ni bila kujali nani amewahi kuvunja utu wa mtu, halileti haki kwa namna yeyote ile kuvunja utu.
Umagharibi ni nini?
 
Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa mila na desturi tuna namna bora ya kuheshimu wakubwa wetu kwa umri ama madaraka waliyonayo. Tusilete umagharibi kisa uhuru wa kusema chochote. Moja ya tunu zetu kama taifa ni kuwa na utu.

Hii ni bila kujali nani amewahi kuvunja utu wa mtu, halileti haki kwa namna yeyote ile kuvunja utu.

Mila na desturi zetu ni zipi na ilikuwaje zikawa mila na desturi zetu.
-kuheshimu watu kwa sababu ya ukubwa na madaraka hiyo si heshima bali ni uoga, unafiki na upumbavu.Heshima ni kwa kila mtu bila kujali hadhi wala ukubwa na udogo wake.
-Hao viongozi wanafanya ufisadi, wanawanyonya wananchi, wanaongeza ufukara na ujinga kwa wananchi, huo utu unaozungumza ni utu gani kama wao hawana huo utu.
-
 
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake
...
Mama ameamua kuleta upole kwenye nafasi ambayo haihitaji upole ,shida inaanzia hapo.
 
Tamaa ya mamlaka, mali na pesa imewafanya watu wengi wakiwamo watanzania kukosa kabisa utu hata kufikia hatua ya kuliumiza taifa ili tuu wapate kile wanachokitaka.
Vyama vya Upinzani walikiri haya. Kuwa Wametengeneza mazingira haya, na sasa athari zake zimeenea kwenye wanja la Siasa na Jamii, kisa? Madaraka, vinyongo na visasi Binafsi. Wamo na masaliti wengine ndani ya CCM.
 
Niache kumheshimu mama aliyepo kijijini akipambana na kilimo bila msaada wa serikali nimheshimu kikongwe anayezurura bila malengo na kutumia hovyo kodi za wananchi

IMG-20240409-WA0000.jpg
 
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake

Nimesikia na kufuatilia kwa uchache sana mambo yanayoendelea mitandaoni na vile yanavyopokelewa na jamii ya watanzania nimejifunza mambo muhimu moja kubwa likiwa ni kukosekana kwa uzalendo na maadili kwa watanzania, na pili udhaifu wa fikra au ujinga pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia haswa kwa habari za mitandaoni.

Mtu yeyote mwenye mdomo au uwezo wa kuandika anaweza kuongea au kuandika na kupost kitu chochote mitandaoni - ila inahitaji mtu mwenye akili na uwezo wa kuchambua mambo kujua kwamba bila uthibitisho, sio kila kinachoongelewa au kuandikwa ni cha kweli!
Kama ambavyo mtu anashabikia jambo ambalo limeandikwa au kuongelewa, na ambalo hajathibitisha ajue hata yeye watu wanaweza kushabikia jambo linaloongelewa au kusemwa kuhusu yeye ambalo hata yeye halijui!

Watanzania tubadilike, kuwa kwetu nyuma ya keybords kusitufanye tukaongea na kushangilia mambo maovu yanayoumiza nchi yetu, viongozi wetu na hata sisi wenyewe na vizazi vyetu...

Ni wakati muafaka sasa kwa kila mzazi na kila mwenye nafasi ya kusimama kama mlezi kwa watoto na vijana wa Kitanzania kuwakumbusha na kuwafundisha kuwa wazalendo na kuwa na heshma, kukumbatia upendo kwa ajili ya kujiletea maendeleo wao wenyewe na nchi.

Tuwakumbushe na kuwafundisha watoto na vijana kuipenda Tanzania, kuwapenda watawala na viongozi wetu, na kujipenda wao wenyewe kwa kusimama katika kweli na haki, kutofuata na kutoamini mambo yasiyo na ukweli au ushahidi na kutojkujihusisha na tabia mbovu kwani wanapojipenda na kujitunza, hawatoingia kwenye matatizo.

Tuwalinde watoto na vijana wetu kwa kuwapa elimu na kuwatia ufahamu wa kuacha mihemko ya kingono kwa kuachana kabisa mitandao inayosambaza habari za ngono na kila uchafu kama wenyewe wanavyoziita "connection".
Vijana wanapaswa kukua wakielewa kuwa ngono haifai, na kujamiiana kunapaswa kuwa na nidhamu na kutumika kwa makusudi ili kuzalisha binadamu wapya na sio kutumika kwa kitu cha kufurahisha."

Kijana anatakiwa kujua kuwa "Uzalendo ni upendo kwa nchi yake na watu wake, lakini pia anatakiwa kujua hilo haliwezekani bila kuwa na subira na kujiepusha maovu huku akitoa maoni na kukemea maouvu kwa njia ya staha bila kusema uongo au kutumia matusi au kutoa maneno ya kuudhi."

Uzalendo ni hisia ya upendo, kujitolea, na hali ya kushikamana na nchi au serikali. Kiambatisho hiki kinaweza kuwa mchanganyiko wa hisia tofauti kwa mambo kama vile lugha ya nchi ya mtu, na nyanja zake za kikabila, kitamaduni, kisiasa au kihistoria.

Unachohitaji kujua; ni pamoja na wale wanaoamini Mungu yupo kumpenda Mungu, kuipenda nchi yetu Tanzania, kuwapenda wazazi wetu, kuwapenda watoto wetu, kuwapenda ndugu zetu; tunatakiwa kujua jinsi wanadamu wanavyobadilika, na kujipenda mwenyewe pia.

Tamaa ya mamlaka, mali na pesa imewafanya watu wengi wakiwamo watanzania kukosa kabisa utu hata kufikia hatua ya kuliumiza taifa ili tuu wapate kile wanachokitaka.

Kabla ya kutukana na kuongea maneno ya kuudhi simama kwenye nafasi yake, au msimamishe mama yako mzazi, mke wako, binti yako, shangazi yako au bibi yao kwenye nafasi hiyo halafu uone kama ingekuwa rahisi kwao kuongoza hili taifa wa amani na utulivu uliopo.

Tendelee kumuombea Rais wetu na Mama yetu Samia Suluhu Hasan na kuliombea taifa letu.

Kwa wale waamini wa Mungu tunakumbushwa​

1. Kutii Mamlaka​

Warumi 13: 1-5​

"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.
Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."

2. Utii na heshma kwa wazazi - Mzazi ni yule aliyekuzaa pamoja na yule mwenye rika sawa na alieyekuzaa​

Kutoka 20:12​

“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako."

Quran inatukumbusha kuheshimiana​


Utu wa kila mtu aliopewa na Mungu lazima uheshimiwe, bila kujali imani yake, rangi, asili ya kabila, jinsia, au hali ya kijamii (Quran, 17:70). Kwa sababu kila mtu ameumbwa na Mungu Mweza-Yote, Muumba wa wote, ni lazima wanadamu watendeane kwa heshima, staha, na fadhili-upendo kamili.
70. Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchikavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilishakwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba
Hili gazeti ilifaa ulitume Kwa Mange uyakoge matusi yako.
 
Niache kumheshimu mama aliyepo kijijini akipambana na kilimo bila msaada wa serikali nimheshimu kikongwe anayezurura bila malengo na kutumia hovyo kodi za wananchi

View attachment 2965068

Pole kwa jazba

Kwanza jiulize ilikuaje mama yako kikongwe akabaki akilima kijijini au ndio shule ilimkataa zamani nae akaikataa??

Maana hata Rais hakuzaliwa Ikulu, alitokea hukoooo kijiji cha Kizimkazi
 
Back
Top Bottom