Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Kwa mkuu huyu tegemea record ya vyote either awamu Moja tu
Au awamu zaidi ya mbili

Sijui Umenielewa
 
Kweli upumbavu wako hauna gharama
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi; Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili; Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu; Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
 
Na wagamboshi walifanya nini? Usitubambikie maombi ya Gamboshi
 
Mh. Rais atarudi kwa kishindo zaidi, Watanzania wengi tuko na imani nae kwa miaka mingine 6 iliyobaki..

Mungu Mubariki Mh. JPM..

Mungu ibariki Tanzania, Amen...
Yupo wapi kwani? Maana me sielewi kinachoendelea
 
Nahisi huu ni muda muafaka kwa mamlaka husika kututoa hofu wananchi , c vyema kukaa kimya kwa mamlaka husika
 
Poleni kwa kubaki wakiwa.

Naona km wenzio wametelekeza umebaki peke yako ukipiga ramli
 
meangalia clip inayotembea imeonesha alifukiziwa moshi wa KOROSHO !!! ka kweli naona wa kusini wana tekinolojia ya hatariiii.......

Mejiuliza JE kuna umuhimu wa misafara ya viongozi kuwa na WAGANGA waaguajiiii...wanaoweza weka makarai ya maji na kuongeza usalamaaa...IJAPOKUWA serikali haiamini uchawi/ushirikina
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…