Mkuu ndio maana nilimuuliza kama 'agreement' inaridhiwa na Bunge. Alikimbia na mwisho akasema hajui.
Ukweli ni kwamba katiba ya JMT (1977) Sura ya Tatu sehemu ya kwanza Bunge (63)-1(e) inasema bila utata '' Kujadili na kuridhia mikataba yoteinayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa''
Kwa mantiki hiyo kilichoridhiwa Bungeni ni Mkataba ingawa Spika ambaye ni Mwanasheria na Prof wa chuo kikuu anakwepa ukweli huu bila kuonyesha maridhiano yameanishwa wapi. At least
FaizaFoxy amekwepa kujibu.
Hii ina maana nyingine, kwamba, Jamhuri ya muungano ni pamoja na Zanzibar. Sasa kuna sheria gani nyingine ambayo ipo juu ya katiba ya JMT? Hapa ndipo wanaosema kuna hoja za Uzanzibar wanapata nguvu sana.
Kwamba Wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT walikwenda Dubai kwa gharama za Tanganyika kama Watalii kwasababu hili jambo haliwahusu. Lakini je, haliwahusu? Katiba inatamka ni la muungano.
Ikiwa si jambo la muungano vipi waziri na mwenzake ambao ni Wazanzibar wasimamie jambo lisilo wahusu wakimshauri Rais Mzanzibar kwa masilahi ya Tanganyika ambayo wao kama Wazanzibar wameyakwepa ?
Wenye hoja ya Uzanzibar wana neno!
Ni kwa mantiki hiyo Zanzibar imepewa nguvu sana hata kusigina katiba. Hii si mara ya kwanza, tunakumbuka katiba ya Zbar 1984 toleo la 2010 imekiuka ile ya JMT, hakuna anayehoji kwasababu wanaofanya hivyo ni Wazanzibar.
Mbowe alipotoa tahadhari kama kiongozi mwenye wafuasi hilo likawa balaa. Kwamba Mtanganyika hawezi kusimamia masilahi ya nchi yake kwasababu haki hiyo kapewa mzanzibar peke yake.
Kwa tukio la Bandari kuna kufungua ''pandora box' au can of worms. Ni jambo baya lakini pia ni zuri kwasababu limeonyesha matundu yaliyopo na limesaidia sana kuwaamsha waliobeba Muungano kutaka haki ya kuwa na maamuzi ya nchi yao. Hoja ya Tanganyika haitaondoka na katiba mpya haikwepeki.
Mwisho, ikiwa tunakubaliana Bunge liliridhia Mkataba, mkataba ni jambo binding, kwasasa hatuwezi kuchomoa hata kwa bahati mbaya. Hapa ndipo tunajibu swali la Faiza kwamba, DP Haiendeshi bandari yoyote lakini tayari sisi umefanya commitment. Tukiondoka tu lazima kuna kitu watalamba.