Ni kweli usemayo watu na utamaduni wa sasa imekuwa sifa kujitumikia wao (ubinafsi na sio mapana ya nchi na vizazi vijavyo) wizi umekuwa ni sifa na hili siwaulama wao tu angalia leo watu wanacheka familia ya Nyerere kwamba alikuwa mjinga- kuna watoto ndugu na jamaa zake ni masikini (sasa unategemea huyu mtoto anayemcheka leo Nyerere kwamba hakulimbikiza mali za kuwasustain mpaka vitukuu akipata nafasi ataangalia Taifa au atafanya chini juu asiwe kama Nyerere) ?
Ndugai alivyokuwa Spika alihakikisha wabunge so called anawatengenezea mambo mazuri (tena kwa siri) unategemea huyu hata asingemtetea mtanzania wabunge wenzake wangemtupa ? Lilipokuja suala la Posho za vikao ni wabunge wangapi walikuwa upande wa kuzifuta na waliopinga hilo wakaonekana kwamba wanatafuta kiki na political mileage....
Ingawa mimi naona hawa wabinafsi wanajiona wana akili lakini hawajui kula na vipofu (hili gap la umasikini na utajiri) linavyozidi kuwa kubwa hata kama sio wao tu huenda wakawaletea vitukuu vyao shida sababu wananzengo watasema shida tunazozipata leo ni upuuzi waliofanya wazee wenu na kila mlicho nacho ni zao la unyonyaji wa wazee wenu.....
Kwahio mimi njia hio nimesema sio kwamba inawezekana lakini ndio njia ya uhakika ninayoona mimi itaondoa huu ujinga (hata kwenye maisha ni kweli kuchunguzana na kuwekeana camera CCTV mtaani huenda tukaita ni police state) ila sababu tunajua binadamu huwa wanaiba basi uwepo wa hio camera hapo utawazuia kuiba kwa wakati huo - kwahio since mali ni ya mwananchi basi mikataba ya mali hio mwananchi ajue kila kinachoendelea hata kama asiposoma lakini kiwepo sehemu wazi akitaka akasome..
Huko tunapoelekea dunia ya machawa / udini na ukabila - Usishangae kabisa mtu akashikwa kwa kutenda maovu ila jamii yake aliyokuwa anakula nayo / kudhani alikula nayo ikamtetea kwamba alikuwa msafi (refer ukabila wa Kenya na yule Gavana mla mrushwa ingawa watu wake wanamtetea sababu ni kabila lake) - Au kama kweli unaamini Trump alikiuka sheria ama la ; ila wafuasi wake wanaona kwamba ni propaganda za watu....., Au Upinzani wa Brazil ambao watu wapo so divided ambapo ukimshika kiongozi wa upande mmoja hata kama kweli alifanya kosa itaonekana ni politically motivated hence nchi kuchafuka - Utaona kwamba kwa hayo yote hata mahakama itapata kigugumizi cha kufanya maamuzi na hata maamuzi yakifanyika itakuwa after the fact (tumeshapigwa) pia mbuzi wa kafara huwa hakosekani....
Hivi katika mambo ya Escrow, Dowans n.k. instigators walikuwa ni kina nani ? Na wote walishikwa na kukemewa au baadhi walitolewa kafara and we don't even know what happened anyway...., Na kina Balali Je ?
Again, sina tofauti ya msingi na maandishi yako. Sote tunalenga sehemu moja ya manufaa kwa wananchi wetu.
Kwa kuepuka kuandika maneno mengi sana ngoja nitumie mifano miwili hapa itatosha.
Hakuna anayeweza kusema nchini Marekani hakuna rushwa na mambo mengi ya hovyo yanayoendana na hali hiyo ya kimaisha.
Lakini kwa mfumo wao wa serikali, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kufanya madudu kama tunayoyaona hapa kwetu, halafu akaendelea kuwachekea wananchi kama hakuna baya lolote lililotokea.
Samia angekuwa ni kiongozi wa nchi hiyo ya Marekani, wakati huu hata sijui angekuwa katika hali gani.
Mfumo wao hao Marekani umewafikisha hapo. Huo ni mfano wa kwanza.
Mfano wa pili, mara nyingi huwa nasema humu jukwaani kwamba waChina kwa kawaida yao ni wezi sana. Hii ni kutokana na jinsi wanavyojionyesha wanapokuja huku kwetu na kutaka kukwapuakwapua kila kinachopita mbele yao.
Lakini kule kwao ni nadra sana kusikia wakifanya kama wanavyofanya wanapokuja huku kwetu. Ina maana kuna kitu kinachowafanya wasijihusishe na ukwapuaji huo.
Pamoja na kuwa mfumo wao wa kisiasa ni tofauti na ule wa Marekani, lakini kiongozi wa China ukisikia kajihusisha na mambo kama haya wanayoyafanya akina Samia, hawezi kamwe kubaki salama.
Kwa hiyo, kwa mifano hii miwili, utaona kwamba viongozi wa nchi hizo wanabanwa, hawana wigo wa kufanya maamuzi mazito yanayoweza kuleta maafa kwa nchi zao kwa kutaka kujinufaisha tu wao wenyewe.
Swali linalopashwa kuulizwa ni kwa nini isiwezekane nasi kuwafunga gavana hawa wapuuzi wetu hapa?