Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

I have 2 questions
1.Je in kweli Serikali yetu inakosa trillion 1 kuwekeza kwenye bandari, hadi kuamua kuwapa D.P world au kuna watu wanatafutiwa ulaji kupitia uwekezaji huo?
2.Kama issue ni ufanisi pale bandarini,Rais kama Kiongozi wa Nchi anashindwaje kusimamia ufanisi huo au kuna makundi ya watu wanatumia bandari hiyo wana power kuliko yeye,na kama ndivyo kuna maana gani ya yeye kuwa Rais?
 
Ni mjinga (huhitaji kuelemishwa) tu asiyejua kuwa moja ya vichochezi vya uchumi ni uimara na ubora wa miundombinu ya usafiri (ardhini, majini na angani).

Hivyo basi, kuendelea kuelezea manufaa ya uwekezaji bandarini, badala ya namna na jinsi ya uwekezaji huo, ni dhahiri ni kutetea ubatili wa vifungu vya IGA.

Swali kwako FaizaFoxy, ulijibu kwa nia njema kabisa.

Kwani hakuna njia mbadala na ya win-win situation (nipe-nikupe) ya kuboresha bandari zetu?
 
Kwa kujibu swali lako,kweli DP world wala dubai hawaendeshi bandari yetu,.namimi pia nakuuliza swali

Nijuavyo mimi mkataba wa dp world ni wa milele na hakuna nafasi ya kuvunja kama ikitokea sintofahamu,kweli si kweli?
 


Umezidi kutupigia kelele, kwani unapewa hela kila siku? Imetosha sasa.
 
1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Ujue nyie watu mlio nje ya system kuna mambo mengi hamuelewi,ngoja nikueleweshe kidogo.
1.IPO hivi kila kitu kuhusu mikataba ya uendelezaji wa bandari na DP world ilikuwa tayari-issue ambayo ilikuwa bado ni execution ya mkataba.
2.huu mkataba kuja public-fahamu kuna msamalia mwema,ulipita mkononi mwake akaupiga copy na kuutoa kwa umma ujione.issue hapa ni kuwa aliofanya hiki kitendo alifanya kutokana na uchungu na Nchi au masilahi ya kisiasa??
-haijalishi sababu iliyopelekea huyo jamaa kufanya hivyo,but unachotakiwa uamini ni kuwa kwa 99% sasa hivi jamaa amisha patikana na ni marehemu
3.Huo Mkataba mkataba kupelekwa Bungeni,ni njia ya kupoza joti la kisiasa maana haikutakiwa kwenda huko.
Kwa kujibu swali lako,each & everything kuhusu DP world kimisha kamilika na walikuwa wamisha anza preliminary jobs, how & when siwezi kuelezea wala hapa.
 
PTA = TPA. Shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Tulipo fika na kwa kua mwanzo wananchi hakushirikishwa ,limkataba lifutiliwe mbali tuanze upya , mliohongwa rudisha pesa za watu
 
ccm wametukosea kama Taifa leo tunajadili kuuza bandari karne ya 21 badala ya kujadili bandari zetu kuzifanya free ports.
 
Uko sahihi kabisa Mkuu. Hawa ndugu zetu wanajichanganya. Yeye na Spika wake. Wanasema IGA ( Intergovernmental Agreement)sio mkataba ni Agreement lakini wanasema kinachofuata ni kuingia kwenye mikataba. Kinachofuata baada ya IGA ni HGA ( Host Government Agreement). Sasa itakuwaje HGA iwe mkataba lakini IGA isiwe mkataba wakati zote ni Agreements? Faiza tunaweza kumsamehe lakini Profesa wa Sheria hapana. Yule anafanya makusudi.
Kutokana na hii IGA, hatuna haki ya kuingia mkataba na mtu mwingine katika lile eneo hata kama DPW atazembea au hatutapenda masharti yake katika HGA. Ndicho kilicho wakuta Djibouti.

Amandla...
 
Hakuna cha kuvunjwa, kwanini wavunje makubaliano kwa matakwa yako?

Sasa rudi kwenye swali langu:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Faiza, wakati mwingine unajitakia mwenyewe kusemewa ovyo. Swali lako la kwanza halieleweki na la pili niliisha lijibu.

Amandla...
 
Na katika Point yangu kubwa ninachosisitiza ni Transparency, sababu hata sasa tunachoongelea wanaweza wakaja wakasema tumerekebisha ila marekebisho yenyewe ni siri kwahio hapa tutaendelea kupigwa; au wanaweza wakarekebisha alafu mwaka unaofuata wakafanya amendments na hata hizo amendments zikienda bungeni wanaweza wakapitisha mlungula wala wengi wasijue ni nini kinaendelea au kuweka clause ambazo ni ambiguous..

Na kwa kuonyesha kwamba hawa watu hawaaminiki na kwamba jinamizi linalotumaliza ni lack of transparency ngoja nikupe mifano miwili:

TICTS alikuwa amepewa mkataba wa miaka mitano ili achunguzwe kama yupo poa aongezewe iwe kumi; kabla ya hio mitano haijaisha akaongezewa mpaka kumi na tano (refer kuna speech ya JPM akiwa Bandarini)

Mfano wa Pili according to JPM Mkataba wa Bagamoyo ulikuwa wa hovyo; kipindi hicho hakuna aliyebisha wala Jakaya aliyekuwepo hakubisha kwamba JPM anayosema ya clause za utata ni ya kweli au uongo...., JPM amekufa tunaambiwa Mkataba huo ulikuwa bora hakuna mfano na ni Propaganda zake...., Sasa kama Binadamu anaweza kuwa mwongo na Rais atakayekuja kesho huenda akawa ana Propaganda au ni kweli watu wanaweza kuingiza nchi katika mikataba ya madudu kwanini kila kitu kisiwe wazi, kila mwananchi (ambaye ni mwanahisa by default ya hizi maliasili) aweze kuona mwenye na sio mpaka kuambiwa kutoka kwenye hearsay....

Kwahio tatizo kubwa watawala hawa wanajiona wenyewe ndio vichwa zaidi na wanaweza kuamulia mpaka vizazi na vizazi na wanajificha kwenye jinamizi la Siri za Mikataba; Ingawa sijawahi kuona hizo siri yaani hata mwenye mali (anafichwa) na mwenye mali ni mwananchi hawa wengine ni walinzi wa muda mfupi mfupi tu
 
Unasema wabunge wa Zanzibar walipelekwa Dubai kwa Gharama za Tanganyika suali kwani hiyo Tanganyika ipo?
 
Well said
Well said. Chukua tano
 
Wewe ni mzanzibari sio mtanganyika
 
Huwezi ukajadili jambo na mtu aliyetanguliza chuki,hii issue wengi wanaendeshwa na chuki tu na ubaguzi,

Subiri uone wakakavyokuja na matusi badala ya kujikita kwenye hoja.
Mpaka hapa ww nawe umethiitisha chuki zako
 
Hivi unajua kwanini nimesema not more than 49 Percent ? Maana kubwa ni kwamba mwisho wa siku unakuwa na VETO na hakuna anayeweza kukubishia wala kukuendesha After all kama ni Pesa hata sisi tunaweza kuzikopa au kuzitafuta; Lakini hakuna mwekezaji anaweyeweza kutengeneza ardhi yake ziwani iwe Bandari (huo ni urithi ambao tumebahatika kuwa nao)

Okay hata ukisema labda wewe uchukue 30 na wengine kumi wachukue 7 percent each kitakachotokea mtu mmoja anaweza kuwanunua hao tisa hence akawa na 70 percent (hizo faulo za corporations take over zilifanyika sana huko UK hata mwisho wa siku Bwana AL Fayed akajikuta amejinyakulia Bingo la Harrolds); Ndio maana nikasema ifike wakati hata hao USA , UK wasiwe ndio Case Study ya kufanya vitu bali tufanye vitu bora zaidi kuliko hata wao na kulingana na mazingira yetu
 
Acha unafiki, eti tuache kejeli, jazba na ujinga. Wew ni mbinafsi, mdini kibaya zaid tayar ushakunywa maji ya bendera ya DP world so hakuna utakubaliana nacho. Ogopa kitu inaitwa.... DP world payroll supporters!!!
 
Weka post moja swali moja.
Jibu unayoweza! Hakuna haja yakujaza Saver!

Swali la Mwisho:- Tunaambiwa IGA haikutaja thaman ya hwekezaji wala nini tutafaidika! Ila HGA ndizo zitataja. Tuamini kuwa Serikali yetu haikujua inahitaji uwekezaji wa thaman gani kuifanya bandari yetu iwe bora? Mpaka wanasaini IGA hakujadiliana ni thaman gani itawekezwa katika bandar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…