Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Sijakuelewa ni swali au au ni maelezo kwa muoni wako?

kama ni swali lifupishe, kama ni maelezo basi yaache kama yalivyo tutakusoma.

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Umesema kwamba mikataba haiwezi ikawa transparent kutokana na NDAs nikakujibu hayo yapo katika msahafu gani kwamba hayawezi kubadilishwa na lazima yafuatwe ?

Sababu mzizi wa fitina upo hapo; usiri unapelekea watu kupitisha mambo yao au kutokuwajibika na vilevile ukizingatia hizi mali ni za wananchi huwezi ukasema wananchi wakae gizani alafu walinzi tu ndio wajue wanakubaliana nini kwa niaba ya hao wananchi - Na haya madudu sio Tanzania ni dunia nzima Tax Payers wanapigwa (Bora Jeshini wanajilinda kwamba ni usalama wa Taifa hivyo kupiga pesa no questions asked) Kwa ku-refer A Case on Point kuna kampuni ya ENRON ilivyomu-lobby George Bush wakabadilisha sheria ya Energy isiwe regulated, matokeo yake wakatumia loopholes waka-cook the books kampuni ikafilisika pamoja na lifetime savings za ma mamilioni ya wananchi....

Moral of the Story ni kwamba people are corrupt hata hao ambao tunaona wapo safe na taasisi imara bado mlungula unapita kwa faida ya wachache to the detriment ya Taxpayers - the only cure ni Transparency..... (Hata kama hakuna anayefanya sisi tufanye sio kwenye mali binafsi za watu bali kwenye mali za UMMA)
 

Wewe Dalali hata sijui kama unaelewa chanzo cha waTZ kulalamika.

Tatizo ni mkataba wa Kichifu mangungo ambao unazipiga mnada bandari zote za ukanda wa bahari na ziwa.

Hatuna shida na performance ya DPW ,High Tech ila msiongepee wananchi ,ni kama Nape alivyoongopea waTZ kwamba wamefuta TOZO bila kuweka wazi wamefuta tozo gani ,baada ya kuwapa za uso ndiyo msigwa amekuja mbio mbio kuweka wazi...WaTZ wa sasa siyo wajinga wana uelewa kuliko hata nyinyi viongozi mnaolishwa matango pori.
 
Hayo ndiyo tunatakiwa tuyafanye. tymejifunza kwa TICTS sasa tumekuja kivingine, tujifunze kwa DP World ili wakati uyapofika tuje kivingine, au sisi wenyewe au tutakae vunja nae chawa.

Siku zingine weka post moja swali moja. Unatuchosha .
Wala hayo hayakuwa maswali yalikuwa ni mapendekezo yangu kwa mtazamo wangu. Kukuuliza wewe maswali unless wewe ni SAMIA takuwa ninakuonea sababu wewe mwenyewe ushasema na umesema kwamba usiri katika mikataba lazima uwepo (sasa tunajadili mambo ya Siri) na kesho wakija wakasema huo mkataba mnaodhani mkataba ni Fake mtasema nini ? Au wakiubadilisha alafu ukabadilishwa tena ?

Na wewe majibu unayotoa unayatoa kwenye siri au uliachoambiwa kwamba kipo ? Na ambacho haukuambiwa kama kina impact zaidi na negative connotations ? What then ?

Sasa hilo ndio swali baada ya mapendekezo yangu....
 
1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Kuna anayejadili mkataba wa IGA (watetezi wauita makubaliano) anasema DPW au Dubai wanaendesha bandari? Mimi sijaona hoja humu JF au mitandao mingine ya kijamii. Labda wewe
 
Kuna makubaliano = Agreement.

Kuna mkataba = Contract.


Tusiyachanye hayo mawili. Niayaonayo mimi mpaka sasa ni makubaliano, bado sijaona mkataba. Ndiyo nikasema:

Naamini wewe, katika maisha yako ulikwisha na unaendelea kufanya makubaliano na mtu au kikundi cha watu, hata Taasisi. Ni makubaliano ndio huzaa mkataba. Km unahitaji kumwajiri mtu, mnakubaliana kwanza, au?

Kwa hoja yangu hiyo, makubaliano hayo ya uwekezaji yaliyofanywa na Rais, kwa niaba ya JMT, yakapelekwa Bungeni na kuridhiwa, yana vifungu tatanishi visivyokubalika. Sasa hiyo mikataba itaandaliwaje nje ya makubaliano (IGA)?
 
Kama unawapenda sana kaolewe huko uarabuni urudishwe utumwani kama mwenzako [mention]Icebreaker [/mention]

Wazee wa ukaririshwaji mpo tu, wazee wa chuki mpo tu, wazee wa ubaguzi na ukabila mpo tu, wazee wa udini mpo tu 😄 aise Mungu aniepushie mbali watu wa namna hiyo, aleyommba gekke bhabhaa Mungu aniepushie mbali watu wa namna hiyo
 
Makubaliano yamesema ukomo ujadiliwe na uainishwe kwenye mikataba ...

Hiyo mikataba ndiyo inajadiliwa hivi sasa, na Waziri Mkuu kishatangaza, kasema mkataba wa uendeshaji utakuwa na ukpmo, hautakuwa bila kikomo kama wengi walivyoaminishwa.

Kwa nini mnaotetea IGA kuwa ni makubaliano tu na mikataba ndiyo kwanza inajadiliwa? Hoja siyo tofauti ya "Makubaliano" na "Mkataba" ila baadhi ya makubaliano hayo (Vifungu vya IGA) ni batili.

Makubaliano ndio msingi wa mkataba na si vingenevyo. Hata vile tunazo Sheria, Kanuni na Taratibu za uwekezaji, kwa nini hazitumiki kwa suala la uwekezaji kwa bandari?
 
huo mkataba umesainiwa lini?
Unakodishwa kwa muda ghani?
Na inatoa shingap kwa mwaka?
Na vipi hatia ya wafayakazi wa tanzania wasije wakajaa mashehe bandarini

Chuki mbaya sana, hebu tuambie tangu uwachukie waarabu/waislamu umefaidika na nini! Kwani akiajiriwa mwarabu/muislamu inakuuma nini! Mbona nchi za kiarabu waafrika wengi tu wameajiriwa!
 
Nitatafuta muda tuongee juu ya haya uliyoyaandika hapa mkuu 'Logikos', kwa sababu ninakubaliana nawe vizuri kabisa.

Kwa kifupi tu kwa sasa niseme haya machache: kwa viongozi hawa tulionao sasa hivi, na hivi vyama vilivyopo nchini, sioni hata mmoja anayeweza kutekeleza 'transparency' unayoisemea hapa. Hakuna.

Ni nadra sana, tena kwa bahati ya ajabu sana taifa kumpata kiongozi (hata kama mikataba haiwekwi wazi kwa matakwa ya wawekezaji), anayesimama kidete akitetea maslahi ya nchi yake katika mikataba hiyo. Kwetu hapa sasa hivi ninawajua wawili tu, Mwalimu Nyerere na John Magufuli (huyu kapakwa matope sana, na mengine kayaruhusu mwenyewe).

Kwa hiyo, njia ninayoona labda inaweza kupunguza ulafi wa hawa viongozi wetu wengi ni kubadili kabisa mwelekeo tulionao kwa sasa hivi; tukianzia kwenye kutengeneza Katiba Mpya, ambayo itatamka wazi kwamba hakuna kiongozi yeyote atakayepewa kinga ya kuingia mikataba mibovu inayoleta hasara kwa nchi. Na matokeo ya sheria zitakazotokana na Katiba hiyo, ziseme wazi watakavyoshughulikiwa viongozi wa namna hiyo, wakiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.
 
Ni kweli usemayo watu na utamaduni wa sasa imekuwa sifa kujitumikia wao (ubinafsi na sio mapana ya nchi na vizazi vijavyo) wizi umekuwa ni sifa na hili siwaulama wao tu angalia leo watu wanacheka familia ya Nyerere kwamba alikuwa mjinga- kuna watoto ndugu na jamaa zake ni masikini (sasa unategemea huyu mtoto anayemcheka leo Nyerere kwamba hakulimbikiza mali za kuwasustain mpaka vitukuu akipata nafasi ataangalia Taifa au atafanya chini juu asiwe kama Nyerere) ?

Ndugai alivyokuwa Spika alihakikisha wabunge so called anawatengenezea mambo mazuri (tena kwa siri) unategemea huyu hata asingemtetea mtanzania wabunge wenzake wangemtupa ? Lilipokuja suala la Posho za vikao ni wabunge wangapi walikuwa upande wa kuzifuta na waliopinga hilo wakaonekana kwamba wanatafuta kiki na political mileage....

Ingawa mimi naona hawa wabinafsi wanajiona wana akili lakini hawajui kula na vipofu (hili gap la umasikini na utajiri) linavyozidi kuwa kubwa hata kama sio wao tu huenda wakawaletea vitukuu vyao shida sababu wananzengo watasema shida tunazozipata leo ni upuuzi waliofanya wazee wenu na kila mlicho nacho ni zao la unyonyaji wa wazee wenu.....

Kwahio mimi njia hio nimesema sio kwamba inawezekana lakini ndio njia ya uhakika ninayoona mimi itaondoa huu ujinga (hata kwenye maisha ni kweli kuchunguzana na kuwekeana camera CCTV mtaani huenda tukaita ni police state) ila sababu tunajua binadamu huwa wanaiba basi uwepo wa hio camera hapo utawazuia kuiba kwa wakati huo - kwahio since mali ni ya mwananchi basi mikataba ya mali hio mwananchi ajue kila kinachoendelea hata kama asiposoma lakini kiwepo sehemu wazi akitaka akasome..
Huko tunapoelekea dunia ya machawa / udini na ukabila - Usishangae kabisa mtu akashikwa kwa kutenda maovu ila jamii yake aliyokuwa anakula nayo / kudhani alikula nayo ikamtetea kwamba alikuwa msafi (refer ukabila wa Kenya na yule Gavana mla mrushwa ingawa watu wake wanamtetea sababu ni kabila lake) - Au kama kweli unaamini Trump alikiuka sheria ama la ; ila wafuasi wake wanaona kwamba ni propaganda za watu....., Au Upinzani wa Brazil ambao watu wapo so divided ambapo ukimshika kiongozi wa upande mmoja hata kama kweli alifanya kosa itaonekana ni politically motivated hence nchi kuchafuka - Utaona kwamba kwa hayo yote hata mahakama itapata kigugumizi cha kufanya maamuzi na hata maamuzi yakifanyika itakuwa after the fact (tumeshapigwa) pia mbuzi wa kafara huwa hakosekani....

Hivi katika mambo ya Escrow, Dowans n.k. instigators walikuwa ni kina nani ? Na wote walishikwa na kukemewa au baadhi walitolewa kafara and we don't even know what happened anyway...., Na kina Balali Je ?
 
Again, sina tofauti ya msingi na maandishi yako. Sote tunalenga sehemu moja ya manufaa kwa wananchi wetu.

Kwa kuepuka kuandika maneno mengi sana ngoja nitumie mifano miwili hapa itatosha.

Hakuna anayeweza kusema nchini Marekani hakuna rushwa na mambo mengi ya hovyo yanayoendana na hali hiyo ya kimaisha.
Lakini kwa mfumo wao wa serikali, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kufanya madudu kama tunayoyaona hapa kwetu, halafu akaendelea kuwachekea wananchi kama hakuna baya lolote lililotokea.

Samia angekuwa ni kiongozi wa nchi hiyo ya Marekani, wakati huu hata sijui angekuwa katika hali gani.
Mfumo wao hao Marekani umewafikisha hapo. Huo ni mfano wa kwanza.

Mfano wa pili, mara nyingi huwa nasema humu jukwaani kwamba waChina kwa kawaida yao ni wezi sana. Hii ni kutokana na jinsi wanavyojionyesha wanapokuja huku kwetu na kutaka kukwapuakwapua kila kinachopita mbele yao.
Lakini kule kwao ni nadra sana kusikia wakifanya kama wanavyofanya wanapokuja huku kwetu. Ina maana kuna kitu kinachowafanya wasijihusishe na ukwapuaji huo.
Pamoja na kuwa mfumo wao wa kisiasa ni tofauti na ule wa Marekani, lakini kiongozi wa China ukisikia kajihusisha na mambo kama haya wanayoyafanya akina Samia, hawezi kamwe kubaki salama.

Kwa hiyo, kwa mifano hii miwili, utaona kwamba viongozi wa nchi hizo wanabanwa, hawana wigo wa kufanya maamuzi mazito yanayoweza kuleta maafa kwa nchi zao kwa kutaka kujinufaisha tu wao wenyewe.

Swali linalopashwa kuulizwa ni kwa nini isiwezekane nasi kuwafunga gavana hawa wapuuzi wetu hapa?
 
Sasa uongo wangu ni nini?

Unaota?
Hujauliza vizuri swali lako.
Hakuna mahali watu wamehoji uwezo wa DP World kwa ubora wa utendaji wake.
Jibu ni Kwamba DP World wana uwezo mkubwa katika shughuri za kuendesha Bandari.

Na wanafaa sana kuboresha Bandari yetu.
Sasa usikilize kwa makini Wananchi wanachokilalamikia na uulize tena swali lako.
 
Miezi miwili sasa hakuna walichokisema wanachi ambacho hakijajibiwa na serikali.

Sasa imefikia uhasama wa kiimani umeanza kupamba moto. Au hulioni hilo wewe?
 
Kati ya mwarabu na mchina nani ana uwekezaji mkubwa,ajabu wanaweka syllabus ya lugha ya kiarabu badala ya kichina.Pole tanganyika evil is stalking you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…