Watanzania tusijiaibishe. Tunamtetea anayejichukulia sheria mkononi kuua polisi?

Yaani ukashitaki kwa aliyekudhulumu..!?
 
Wewe ndio tukushangae, sasa wanasiasa wa upinzani unawalaumu badala ya kuwalaumu wanasiasa wa ccm kuua polisi, tamko la chadema kama chama cha siasa ulilisikia?
 
Yaan ,kama siasa za kina Heche zimekuwa za matukio na tena za kulazimisha uongo uwe ukweli.Basi hivi vyama vimeshakufa
 
Hii nchi inahitaji kina hamza kama mia hivi...Police wanaua sana watu...wafe tu hakuna namna wamezidi mazoea yakichoko...homie sent a msg it was well derivered, ndio mana kubwa jinga limefreak out..anaongea upuuz tu analaumu wazazi kwa kumzaa jamaa what a shame..
 
Ndata hata akiwa ndugu yangu huwa simuamini, siku ukiingia kwenye kumi na nane zao ndo utaelewa.

Kama ni kweli alihusika na mauaji ya wale askari, atakuwa kateleza (kwa ninavyofikiri) kimatendo, ila ujumbe alioufikisha Bwana Hamza juu ya polisi nimeuelewa.

Watu tusisahau, msingi wa AMANI katika nchi yetu ni HAKI.
 
Haki na usawa ni mapacha daima hivi vitu vikikosekana hakuna amani wala furaha kwa Watanzania wengi Hamza amekuwa shujaa kwani jeshi letu la polisi mara nyingi hutimiza wajibu kwa maslahi ya viongozi na hasa wanasiasa na kuacha kundi kubwa ambalo ni wananchi na sio police tu

Leo nilikua Tunduma nadhani mlisikia kuwa maafisa kadhaa wa mamlaka ya mapato walifariki kwenye ajali siku kadhaa sasa kule wananchi ni furaha tu wanasimulia wanacheka wanaona mungu kasikia kilio chao mnakumbuka Kigoma wananchi waligoma kutoa ushirikiano wakishinikiza maafisa kadhaa wahamishwe hawawataki je unadhani ilikuwa kwa bahati mbaya?
 
hiyo habari hata haikuvuma maana watanzania hawana habari nao kabisa. Yaani ndio kusema " acha wafe"
Hawa maafisa baadhi yao wametumika sana kubambikia watu kesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…