Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna cha mchezo mchezo wala nini.habari ndio hiyo kuwa Watanzania wanamhitaji Mheshimiwa Paul Makonda awe Rais wao.
Sema baadhi ya watanzania watokanao na chama cha mapinduzi. Jifunze public writing and speaking because it is both science qnd arts
 
Tangia lini na wewe umekuwa CCM na mwana CCM Ndugu yangu msanii
Nimezaliwa na wazazi ambao ni makada nguli wa CCM, nimekulia humu tangu chipukizi, uvccm hadi leo nipo wazazi na Taifa. Nalipia ada zangu za uanachama tena hivi sasa kwa kadi ya elecytonic. Ingawa mnakusanya hela zetu kila wakati kwa hadaa ya kadi za electronic ambazo tangu zoezi lianze hatujawahi luziona wala kusikia zipo zaidi ya kupewa namba tu.

Ninaipinga CCM kwa sababu imeamua kukumbatia majizi, mafisadi, wezi na wahalifu kwa kuwapa nafasi kushika nafasi za juu za chama.

Chama kimetumia rasilimali zake kuasisi ukombozi wa Afrika na kilichoambulia ni kuoga yale yote iliyoyapinga enzi za ukoloni, ubeberu na ubaguzi.

Unadhani Tanzania ipo huru chini ya CCM? Hapana hata kidogo.
Angalia sheria zinazozuia raia kukosoa viongozi wanapofanya vibaya. Wale wanaosifia na kuwatukana wasio viongozi wanapewa kipaumbele na teuzi juu.

Sitoki CCM, nitaipinga nikiwa humu humu
 
Hiyo misaada na mikopo ya masharti nafuu nikatika kuongezea na kukamilisha pale tulipoanza na kuhitaji kwenda kwa kasi zaidi. Pia tambua yakuwa huwezi kupewa mkopo au mikopo kama huaminiki na huna uwezo wa kulipa mkopo husika. Tanzania tunapewa mikopo kwa kuwa tuna uwezo wa kulipa mikopo tunayokopa kujenga miradi ya kimkakati na miradi ya huduma za kijamii kwa ajili ya watanzania.

Makonda ndiye Rais wetu kuanzia 2030
 
Mzee umepuyanga,kazi ya hamasa na kujenga chama annaiweza ila sidhani kama mamlaka zinataka kurudi awamu kama ya 5 bila kujalisha nyie Wanyonge mnataka au laa.

Na hapo unakuwa humpendi huyo Makonda Kwa sababu watu wenye kaliba yake ya msimamo mkali na wasiopenda kukosolewa Huwa ni disaster sana na hawadumu eg Lumumba,Sokoine, Mwendazake etc.


They are more emotionally unstable
 
Hujajibu hoja mzee naona unaendelea na ngonjera- na kwakua hujui hata kanuni za chama unaamua kuanza kampeni mapema wakati hata (the sanctioned hajaota hizo ndoto) meanwhile kasome katiba sifa za mtu kuwa Rais wa JMT- kwahiyo tunapopewa msaada kwenye elimu Bure sisi tulianza kuotoa bure eti? Au hujui kwamba hizo ni fedha za msaada! Tunapopewa msaada wa condom sisi tulianza eti? Bushi alipotusaidia hela za vyandarua na kutujengea kiwanda sisi tulianza eti! Unajua vyanzo vya mapato ya serikali kwanza au unadhania Dhani tu! Mtafute kafulila alufundishe namna ya kuandika mada mtandaoni zikubalike na zipate critical comments and constructive comments. Vinginevyo utaendelea kuwalamba miguu ukidhani wanakuona
 
Huoni kuwa unajichanganya sana rafiki yangu.unasema hakuna uhuru halafu hapo hapo unasema utaipinga sana CCM ukiwa ndani humohumo.sasa kungekuwa hakuna uhuru ungepata wapi nafasi ya kupinga? Kwanini unakuwa na mawazo ya namna hiyo ya kujichanganya kama nyumbu wa CHADEMA?

CCM na serikali yake imefanya kazi kubwa kubwa sana katika kuliletea maendeleo Taifaetu .kuanzia Katika Elimu, afya, maji, umeme, barabara,ajira,n.k.jiulize wakati tunapata uhuru tulikuwa na shule ngapi za sekondari na leo zipo ngapi jiulize hali ya barabara za lami zilikuwahe wakati huo na leo hali ipoje? Jiulize tulikuwa na wasomi wangapi wa shahada na vyuo vikuu vilikuwa vingapi na leo hali ipoje? Jiulize vijiji vingapi vilikuwa na umeme na leo hali ipoje? Jiulize ulikuwa unatumia muda gani kutoka Mbeya mpaka Dar au Mbeya mpaka rukwa na leo unatumia muda gani?
 
Kungekuwa na uhuru nisingetumia ID ya Msanii Kuibua hoja zangu.

Ndo maana nakwambia chagua akili kwanza kisha mengine utaongezewa
 
Kauli kama hizi sio sawa

View: https://www.instagram.com/reel/C2bv1lJCZcs/?igsh=cXQ4Y25uZWNoY2tq
 
Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko!

Naomba mwabia Dada Mwashambwa kuwa ccm imetunga sheria kuifanya TISS kuwa Jeshi kamili- Mwambie ccm imetunga sheria ya kinga ya kutoshtakiwa na viongozi wa umma wenye maamuzi yanayoliangamiza taifa kwa ubadhirifu- Mwambie serikali ya ccm imetunga sheria ngumu za habari kuunyima umma kureport mambo nyeti yanayofanywa na serikali ambayo hayana afya kwa nchi! Mambo ni mengi!
 
Mheshimiwa Makonda atatufaa sana rafiki na ndugu yangu choice variable.suala la kudumu hapa Duniani linabaki mikononi mwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.maana unaweza usiwe na msimamo wa kizalendo na bado ukafa mapema kabisa na kuwaacha wengine. Lakini ni bora ukafanya kazi kubwa na ya kizalendo na kuandikwa jina kwako kwa wino wa dhahabu katika mioyo ya watu na kukumbukwa vizazi na vizazi.

Naomba pia tuendelee kumsemea Rais wetu mama Samia kwa kazi kubwa anazofanya hapa nchini .bila kumsahau dada yetu wa Taifa Mheshimiwa Dr Tulia Acksoni Mwansasu kiboko ya yule mhuni Sugu aliyekuwa amelichelewesha jimbo kwa maendeleo.

Ila usijali choicevariable mimi na wewe tuendelee kukisemea chama chetu na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na chama na serikali yetu .ambapo sasa amekuja Mwamba Mwenyewe Paul Makonda.
 
Labda nikusaidie ametumia jukwaa huru la jamii Forums ambalo "we dare to talk" kesho kamwambie Rais analea wabadhirifu uone kama utakaa uraiani! Wewe ni mjinga na sijui kwanini huwa hufikiri! Moja wapo ya ahadi za mwanaccm ni kuwa "Binadamu wote ni sawa'" sasa unapoita kundi la watu fulani Nyumbu kisa hamfanani mtizamo na itikadi hufai kuwa hata mwanachama wa ccm. Kwa maana unapomfananisha binadamu mwenzio na mnyama ni rahisi kuutwaa uhai wake! Na tukisema ninyi ni miongoni mwa kikundi cha watu wachache ndani ya chama kisichothqmini uhai wa binadamu hili linajidhihirisha wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…