Watanzania wasema Rais Samia anatosha na hakuna sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais 2025

Nimefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa Ni makundi yote yanaridhishwa na utendaji kazi na uchapa kazi wa Rais Samia na kuhitaji Rais Samia abakie ikulu kwa ajili ya kuwatumikia
 
Hata mm natamani iwe hivyo, lakini katiba inasemaje?
Katiba inaruhusu Rais Samia kutuongoza Hadi 2030 na ndio maana Watanzania wanaendesha kampeni mitaani ya kutaka mama aendelee kuungwa mkono ili asalie ikulu kutuongoza na kututumikia watanzania maana ameonyesha dhamira ya dhati katika kuijenga nchi yetu
 
Luca,ukishashiba makatapera unakuwa mjinga sana.Hapo unapiga mbwewe tu.
😆😆😆😆 Mimi naongea ukweli tu na kuwakilisha sauti nazozisikia kutoka mitaani zinavyozungumza juu ya kiu Yao ya kumhitaji mama Samia Kuendelea kuwa Rais wao mpaka 2030
 
Rais Samia Anatosha Kuendelea kutuongoza maana ameonyesha uwezo mkubwa wa kiuongozi,Sauti ya watanzania na chaguo lao ni mama Samia tu,hawahitaji Jambo lingine Zaid ya mama yao mama Samia aliyeonyesha kuwajali kuwapenda kuwasikiliza na kuwaongoza kwa unyenyekevu na uungwana huku akijenga umoja wa kitaifa ulioimara
 
Bila katiba mpya 2025 hakuna hata haja ya uchaguzi, aendelee tu regardless ni kweli ama sio kweli.
Hata ije katiba itakayo andikwa na madaktari wa sheria kutoka chuo Cha Havard au Oxford au Udsm bado Rais Samia atashinda kwa kishindoo asubuhi na mapema sanaaa
 
mimi sipingani na hoja yako ila naomba uweke reference ya reseach uliyofanya na methodogy uliyotumia hadi ukajiridhisha kuwa unaweza kuisemea Nchi (Watanzania)
Unajua unaongelea mada ya kubadilisha katiba ambayo sio rahisi kiivyo
Anaanzaje kujua,
Ni mwendo wa kuandika bila prove yoyote.

Kwako Mwashambwa kwa nini utusemee uongo?
 
Mie kwa sehemu nilizo pita hapa Tz sijaona sehemu yoyote wanayo unga mkono haya uyasemayo. Kiufupi huu utawala ni moja ya utawala mbovu ambao unapingana n maendeleo yaliyo achwa na uongozi wa magufuli.
Huyu mama kaweza ku invest kulipa watu kuweza kumsifia mitandaoni tu 😂
Hii ni ajenda mbovu sana
 
Hv braza Unalala Lumumba au wamekuwekea Mlinzi akusimamie muda wote uposti upupu ?
 
Kakutuma, unajituma au kujipendekeza. Kwanini usifiche ujinga na kuonyesha ujuzi. Nenda kasome katiba kabla ya kuleta huu utoporo
 
Kakutuma, unajituma au kujipendekeza. Kwanini usifiche ujinga na kuonyesha ujuzi. Nenda kasome katiba kabla ya kuleta huu utoporo
 
Nimefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa Ni makundi yote yanaridhishwa na utendaji kazi na uchapa kazi wa Rais Samia na kuhitaji Rais Samia abakie ikulu kwa ajili ya kuwatumikia
Kama ni hivyo basi umefanya kitu kizuri sana. Lakini nakusihi utoe takwimu za kitafiti ikiwa kama sehemu muhimu ya kimantiki katika mada yako uliyoileta, ili wafuatiliaji wa hoja yako wapate kushawishika zaidi na madai yaliyopo ndani ya maudhui uliyowasilisha hapa jukwaani.
 
Kakutuma, unajituma au kujipendekeza. Kwanini usifiche ujinga na kuonyesha ujuzi. Nenda kasome katiba kabla ya kuleta huu utoporo
Katiba inamruhusu na watanzania wameshaisoma na ndio maana ya uamuzi huo na kiu hiyo ya kutaka Rais Samia Kuendelea kuwaongoza
 
Rais Samia anakubalika na kupendwa Sana na watanzania wa vyama vyote na makundi yote na Wala hawezi kumlipa mtu kumsifia maana mambo aliyotufanyia nchi yetu Ni makubwa Sana na yakuacha Alama kwa miaka mingi Ijayo yataendelea kubakia katika mioyo ya watanzania
 
Kweli katugusa wote: kwa tozo, makato benki, mikopo imetupunguzia bei za bidhaa mitaani, watu wanajenga majumba kilao kona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…