Watanzania wawili wakamatwa India kwa usafirishaji wa kilo 1.5 ya dawa za kulevya

Pesa haijawahi kujaa na kumtosha mtu,kama ukishaingia kwenye hayo mambo,hutaacha kirahisi hivyo,ndio maana wengi huwa wanaishia kukamatwa...
 
Cover up tu hiyo biashara sio yao.

Hao wataozea jela na unga utachukuliwa .
Ila hatujiulizi kwanini biashara itaendelea.

Sababu wenye biashara hawaguswi.
 
Kumbuka unafanyia kazi hyo watu, hawawezi kubali uache hv hv
 

Kwanza nitoe ushuhuda , nimewahi ishi India zaidi ya miaka kumi wakati nilienda soma miaka ya 90 katikati mpaka 2000. Unzi hizo balozi alikuwa mzee Kiwanuka na baadaye alikuja Marehemu mama Eva Nzaro. Wakati huo kulikuwa na mchezo ambao walikuwa wanakamatwa Watanzania lakini mwisho wa siku ukienda unakuta siyo.

Watanzania walikuwa na mchezo wa kuazimisha Passport wakati huo kabla ya hizi za sasa kwa Wanaigeria kwa utaratibu waliokuwa wanaojua wao wenyewe.Sasa bahati mbaya wakishikwa ilikuwa inaonyesha Watanzania ila ukiwakuta hata kiswahili hawajui zaidi wanaongea Kinaigeria. Nachelea kusema isije kuwa yakawa hayo hayo japo naamini Pasport zetu zipo vizuri kiusalama. Ila nilichoandika ni hali ilivyokuwa miaka hiyo wakati nikiwa huko na Paasport za watanzania zilikuwa dili zuri sababu tuliaminika sana kulinganisha na wakenya au wanaigeria. Watanzania wengi wao biashara hii sana wanafanyia Afrika ya Kusini. Inasikitisha sana watu kujiingiza biashara hii mbona zipo biashara halali za kufanya
 
Wakati huo waliokutumia wamekaa kimya?
 
Tunafungua nchi hilo nalo mkalitizame vizuri
 
Umepiga hesabu ya faida tu bila mtaji na expenses nyinginezo,hapo labda faida au labor charge isizidi 10m.
 
Fanya tafiti hata wanaokamatwa hapa bongo ambao tunaowafahamu wanayofanya biashara hizo za ngada , fuatilia Imani zao, au wale wazamiaji wa Afrika ya kusini wanao uza ngada huko wapeleleze ukikuta 100 basi 90 ni WA kwenu
hata maeneo wanayotoka wanajulika ni wapi
 
Nipe mchongo wa biashara moja ya halali itakayoweza kunitoa kimaisha,mtaji usizidi 20m,ntashukuru sana.
 
Kama walitokea Tanzania, ichunguzwe ndege waliyoondoka nayo ilikuwa wakkati gani, askari, usalama wa taifa, watu wa forodha waliokuwepo siku hiyo wote ni wahusika. Waliowasindikiza pia waytaonekana kwenye cctv, wote wamo hao.
Utawafanya nini wakati the whole system is corrupt.Hiyo movie Dr.Mwakyembe ameshawahi ishuhudia akiwa Waziri wa Uchukuzi awamu ya nne na hakuna kitu kilifanyika kwa wahusika.
Wauza ngada wana watu kuanzia Polisi, TISS, DPP,Mahakamani,Bungeni mpaka Ikulu,utawaambia nini?
Rais aliyethubutu kuwanyoosha ni Magufuli tu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…