Watanzania wengi maskini wanafia ndani kwa kukosa matibabu

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Jana nilitoka nje ya wilaya niliyopo kwa ajili ya jambo flan flan, sasa wakati nikiwa huko ugenini mwenyeji wangu alichelewa kunifuata baada ya kumsubiri kwa muda alikuja.

Basi akasema amechelewa kuna jirani yake anaumwa sana yupo nyumbani basi wakati tunaongea kumbe alisahau simu huko alikotoka ikabidi nimsindikize na hichi ndicho kilichonitoa machozi.

Mgonjwa yupo katika hali mbaya, ni mama mtu mzima ambae anaugua sukari, mguu mmoja waliukata tayari sasa huu mguu mwingine hali ni mbaya jamani kidonda kikubwa kimetokea karibu na unyayo kinazidi kusambaa na kutoboa mguu, isitoshe hiyo sehemu ya kidonda panavuja/panachuruzika
maji.

Na pia mguu wote umekuwa mweusi, basi nikauliza kwanini hajapelekwa hospitapi hadi sasa wanadai hali ni ngumu nyumbani hapo na watoto hawana pesa kwani wanaishi kwa vibarua vibarua tu. Wazazi hao ni wazee na walikuwa wakulima wadogo tu.

Na kwa sasa hata mifugo ndani hawana kwani imetumika kwenye matibu tangu mguu wa kwanza na sasa hawana chochote.

Ukweli ni kwamba huyu mama anateketetea huku anajiona kutokana na umaskini uliopo. Hali ni mbaya na watoto wao pia hawana namna kutokana na uduni wa maisha.

update;

asanteni na
nimesoma maoni yenu ,kesho ntajaribu kufanya mawasilino kama ataridhia nipate picha ya mgonjwa huyo.

hata hivo sijui kama kutakuwa na uwezekano wa kukata tena mguu wa pili ama lah maana inavyoonekana sukari imeshasambaa kote kutokana na kuwa akiwa kitandani asipogeuzwa basi hawezi kabisa kujigeuza hadi panakucha hata haja ndogo ni hapo hapo kitandani kwani wanadai viungo vya mwili vimekakamaa kutokana na kwamba sukari imeshaenea kote.
 
Jana nilitoka nje ya wilaya niliyopo kwa ajili ya jambo flan flan, sasa wakati nikiwa huko ugenini mwenyeji wangu alichelewa kunifuata baada ya kumsubiri kwa muda alikuja.

Basi akasema amechelewa kuna jirani yake anaumwa sana yupo nyumbani bas wakati tunaongea kumbe alisahau simu huko alikotoka ikabidi nimsindikize na hichi ndicho kilichonitoa machozi.

Mgonjwa yupo katika hali mbaya ,ni mama mtu mzima ambae anaugua sukari, mguu mmoja waliukata tayari sasa huu mguu mwingne hali ni mbaya jamani kidonda kikubwa kimetokea karibu na unyayo kinazidi kusambaa na kutoboa mguu, isitoshe hyo sehemu ya kidonda panavuja/panachuruzika
maji, na pia mguu wote umekuwa mweusi, basi nikauliza kwanini hajapelekwa hosp.hadi sasa wanadai hali ni ngumu nyumbani hapo na watoto hawana pesa kwani wanaishi kwa vibarua vibarua tu. Wazazi hao ni wazee na walikuwa wakulima wadogo tu. Na kwa sasa hata mifugo ndani hawana kwani imetumika kwenye matibu tangu mguu wa kwanza na sasa hawana chochote.
Ukweli ni kwamba huyu mama anateketetea huku anajiona kutokana na umaskini uliopo. Hali ni mbaya na watoto wao pia hawana namna kutokana na uduni wa maisha.
Ni muhimu sana kwa mwaka huu mpya kila moja wetu, kuhakikisha kuwa na Bima ya afya.

Inashangaza na kufedhehesha sana, mtu ana iphone ya 4m, na hana bima ya afya ya efu70.

Ni muhimu sana kuzipa umuhimu na kipaumbele cha kipekee sana afya zetu, vinginevyo uliyoyaeleza hayakwepeki 🐒
 
Matajiri hufia kwenye hospitali kubwa kubwa kwenye mataifa ya kigeni,kuketwa kama kifurushi na kuzikwa kwa taratibu zile zile!
Wee jamaa! Ni kama wale wale wa ukienda kazini na gari lako mimi nikapanda daladala wote si tunafika kazini? Ukila wali nyama choma mimi nikashindia mihogo kwa kushushia na maji shibe ni hilehile! Kalaghabaho!
 
Jana nilitoka nje ya wilaya niliyopo kwa ajili ya jambo flan flan, sasa wakati nikiwa huko ugenini mwenyeji wangu alichelewa kunifuata baada ya kumsubiri kwa muda alikuja.

Basi akasema amechelewa kuna jirani yake anaumwa sana yupo nyumbani bas wakati tunaongea kumbe alisahau simu huko alikotoka ikabidi nimsindikize na hichi ndicho kilichonitoa machozi.

Mgonjwa yupo katika hali mbaya ,ni mama mtu mzima ambae anaugua sukari, mguu mmoja waliukata tayari sasa huu mguu mwingne hali ni mbaya jamani kidonda kikubwa kimetokea karibu na unyayo kinazidi kusambaa na kutoboa mguu, isitoshe hyo sehemu ya kidonda panavuja/panachuruzika
maji, na pia mguu wote umekuwa mweusi, basi nikauliza kwanini hajapelekwa hosp.hadi sasa wanadai hali ni ngumu nyumbani hapo na watoto hawana pesa kwani wanaishi kwa vibarua vibarua tu. Wazazi hao ni wazee na walikuwa wakulima wadogo tu. Na kwa sasa hata mifugo ndani hawana kwani imetumika kwenye matibu tangu mguu wa kwanza na sasa hawana chochote.
Ukweli ni kwamba huyu mama anateketetea huku anajiona kutokana na umaskini uliopo. Hali ni mbaya na watoto wao pia hawana namna kutokana na uduni wa maisha.
Wee jamaa sijui una roho mbaya au vipi? Ulivyoona hivyo wewe ulitoa msaada gani? Kwa jinsi unavyojinasibu na kushangaa umasikini ningetegemea walau umpeleke hospitali na kugharamia japo huduma ya kwanza au toa basi 50k iwasaidie kumuuguza kuliko kuona ulichokiona na kubeza
 
Poleni Sana Ila Kama ungemfanyia utaratibu wa kumuombea msaada ingekuwa vizuri Sana.

Mpeleke hata hosptali kwanza then naamini anaweza kuchangiwa akapata matibabu

Binafsi nimeguswa na Kama kutakuwa na namna yoyote ya kumsaidia huyo mgonjwa utasema.
 
Poleni Sana Ila Kama ungemfanyia utaratibu wa kumuombea msaada ingekuwa vizuri Sana.

Binafsi nimeguswa na Kama kutakuwa na namna yoyote ya kumsaidia huyo mgonjwa utasema.
Mimi namuomba mleta mada arudi walau apige picha ya jeraha (hata picha nzima kama mwenyewe atakubali) alafu weka namba ya kumchangia watu wamtumie chochote
 
Ni muhimu sana kwa mwaka huu mpya kila moja wetu, kuhakikisha kua na Bima ya afya.

Inashangaza na kufedhehesha sana, mtu ana iphone ya 4m, na hana bima ya afya ya efu70.

Ni muhimu sana kuzipa umuhimu na kipaumbele cha kipekee sana afya zetu, vinginevyo uliyoyaeleza hayakwepeki 🐒
Unalo lisema ni la kweli lakini kuna kaya haziwezi kuipata hiyo 70 elfu hata wafanye, nafikiri kunapashwa kuwe na njia ya kuweza kuzisaidia kaya masikini hasa vijijini ili kuweza kufikia malengo ya kuwafikia wengi ktk Afya ya jamii.
 
Hiyo bima ya elfu 70K inaweza Ku-cover matibabu makubwa Kama kisukari , moyo, n.k.
Unalo lisema ni la kweli lakini kuna kaya haziwezi kuipata hiyo 70 elfu hata wafanye, nafikiri kunapashwa kuwe na njia ya kuweza kuzisaidia kaya masikini hasa vijijini ili kuweza kufikia malengo ya kuwafikia wengi ktk Afya ya jamii.
 
Nampa pole mgonjwa,, pia nakupa hongera kwa kuona robo ya halisi ya Tanzania na si Tanzania ile inayopambwa kwenye vyombo vya habari...... Ikiwezekana weka namba ya huyo mgonjwa anaweza saidika.
Kiuhalisia Tanzania Hali ni mbaya kuanzia kwenye umaskini wa kutupwa, ubinafsi,
Kuna mzee Kijiji sitakitaja anapigwa vita sana lakini aanatibu magonjwa ambayo mpaka sasa hayana tiba madaktari na wizara wanahitajika wafanye tafiti juu ya hizi tiba badala ya kuzipuuza ili maskini wakasaidike huko.... Ukipata namba mi ntasaidia pakubwa kama mtu asiejulikana akapte tiba hospitali.
 
Hiyo ndiyo inaitwa "Diabetic Foot Ulcer"..

Matibabu yake ni kukata mguu tu, hakuna option ingine maana mguu unakuwa umeshaoza kabisa.

Na level ya uozaji wake ndiyo itadetermine unakatiwa wapi, kama umeoza mpaka kufikia kiunoni ndo basi tena, hakuna namna ya kuukata.

Hayo ndiyo maisha yetu vijijini, huko huwa kuna option 2 tu ukiumwa, kama kuna pesa unapelekwa hospitali, kama hakuna basi watu wanasubiri nature i-take place.

Nakumbuka jinsi tulivyokuwa wadogo miaka ya 90, magonjwa kama malaria tulikuwa tunapewa miarobaini, mijohoro nk ndiyo tunaponea hiyo.

Nchii hii kuna umasikini usiomithilika, imagine enzi hizo tunasoma sekondari, ada ni 20k lkn unamaliza miaka 4 ukiwa bado una deni la ada.

Hii nchi siku watu wakiwa na access na mabomu wanaweza wakaanza kujitoa muhanga, maana kuna uchungu usioelezeka.
 
Dah!
 
Ni muhimu sana kwa mwaka huu mpya kila moja wetu, kuhakikisha kuwa na Bima ya afya.

Inashangaza na kufedhehesha sana, mtu ana iphone ya 4m, na hana bima ya afya ya efu70.

Ni muhimu sana kuzipa umuhimu na kipaumbele cha kipekee sana afya zetu, vinginevyo uliyoyaeleza hayakwepeki 🐒
Kwani bima ya afya ni Bure? Si mpaka uchangie kila mwaka. Mtu anakosa hela ya kula na umuongezee mzigo/mchango wa bima ya afya!
 
Back
Top Bottom