implicit memory
JF-Expert Member
- Nov 14, 2024
- 806
- 926
Mkuu unajua leo hii hali, mbona sasa imezoeleka!!?,,nikujihangaikia si wenyewe kadri tuwezavyo na mungu muweza anatulinda.Jana nilitoka nje ya wilaya niliyopo kwa ajili ya jambo flan flan, sasa wakati nikiwa huko ugenini mwenyeji wangu alichelewa kunifuata baada ya kumsubiri kwa muda alikuja.
Basi akasema amechelewa kuna jirani yake anaumwa sana yupo nyumbani basi wakati tunaongea kumbe alisahau simu huko alikotoka ikabidi nimsindikize na hichi ndicho kilichonitoa machozi.
Mgonjwa yupo katika hali mbaya, ni mama mtu mzima ambae anaugua sukari, mguu mmoja waliukata tayari sasa huu mguu mwingine hali ni mbaya jamani kidonda kikubwa kimetokea karibu na unyayo kinazidi kusambaa na kutoboa mguu, isitoshe hiyo sehemu ya kidonda panavuja/panachuruzika
maji.
Na pia mguu wote umekuwa mweusi, basi nikauliza kwanini hajapelekwa hospitapi hadi sasa wanadai hali ni ngumu nyumbani hapo na watoto hawana pesa kwani wanaishi kwa vibarua vibarua tu. Wazazi hao ni wazee na walikuwa wakulima wadogo tu.
Na kwa sasa hata mifugo ndani hawana kwani imetumika kwenye matibu tangu mguu wa kwanza na sasa hawana chochote.
Ukweli ni kwamba huyu mama anateketetea huku anajiona kutokana na umaskini uliopo. Hali ni mbaya na watoto wao pia hawana namna kutokana na uduni wa maisha.