Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Wewe ndio mshamba.
Huna hoja.
We hoja tuone akili zako.

Unafrikiri kila mtu anatamani siasa mkuu.
 
Ibrahin Ajib "Kadabra" Anasema kama unaona kwenda ulaya ni kitonga, basi nenda wewe.

Jamaa ni haki yao kukataa, mambo mengine wawe wanauliza muhusika kwanza, siyo kupelekeshana

Mimi nawapongeza kwa misimamo hiyo.
 
Kwa kweli bila kupepesa maneno, cheo cha ukuu wa wilaya kwa sasa mhh...kama mtu una madili yako ni bora ukatae uteuzi uendelee kupiga misele yako tu, usije ukapata pressure bure
Zamani nyakati za Nyerere mkuu wa Wilaya akiwa anaitwa Area Comissioner kilikuwa ni cheo chenye heshima sana. Mpaka mtu uteuliwe kuwa Area Comissioner lazima uwe ni mtu wa shoka sana. Lakini siku hizi, dah!
 
Lugha Kali Sana Kwa kiongozi wako wa inchi
 
Hata mafuta ya kwenda kukagua miradi mbalimbali ya serikali inabidi kumpigia magoti mkurugenzi, mkuu wa wilaya anaweza kupata oc ya sh 1,500,000 baada ya miezi 3
 
Mungu wangu, daah. Watu mnakua na akili za ajabu sana, Kwanza usiseme naongelea juu ya waalimu kukataa uteuzi. Nilipoongelea waalimu kukataa uteuzi ni kwenye nyuzi zinazohusiana na hilo, sasa sijui ulitarajia ni comment kitu gani?
Pili, utaratibu siyo tu kuandika barua ya kuandika barua kuitikia wito/uteuzi bali unaweza pia ukaukataa wito huo.

Kingine, unaposema ukiona mtu anakataa uteuzi basi ujue pale alipo pana maslahi zaidi, kwani kuna shida gani pakiwa na maslahi zaidi?
Kwani utaratibu ni lazima kukubali hizo teuzi?
 
Aliyewaambia wanataka kuwa viongozi wa kisiasa ni nani? Haya maisha jifunze kuwa huru usipende kuburuzwa kipumbavu. Nafasi ya hawa viongozi wa CWT kiajira wao ni walimu hawakwenda SONGEA TTC kusomea ukuu wa wilaya walienda wawe walimu na kazi zote za majukumu ya ualimu, Kugomea teuzi sio kosa kisheria kama ni kosa Nipe kifungu sio maneno matupu.

Mwajiri wa mwalimu ni mkurugenzi maana wapo chini ya serikali za mitaa (halmashauri) na sio Rais acheni ubabaishaji hakuna Mwajiri namba moja Wala namba kumi Mwajiri ni mmoja tu MKURUGENZI nahakuna kipengere chochote cha mkataba kinasema ni kosa Kugomea uteuzi bali Kuna kipengere kinasema utakuwa tayari kufanya kazi ya ualimu na majukumu mengine utakayopangiwa maana ake yale tu ndani ya proffesion na uwanja wako wa kazi kama kuwa mtaaluma, mkuu wa shule na mengineyo
 
Nani aliyekwambia kukubali uteuzi ndiyo kunamuweka huru dhidi ya shutuma alizo nazo? Tangu lini wakuu wa Wilaya wana kinga ya kutoshitakiwa?
Kwani ni kipi kilichomtokea aliyekua Mkurugenzi wa Halmashauri huko Ruangwa? Alipiga hela alipokuwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Baadaye akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, juzijuzi tu hapa TAKUKURU wamemfungulia Mashitaka akiwa kwenye nafasi yake ya ukuu wa Wilaya hali iliyopelekea rais kutengua uteuzi wake.

Au kama ana hizo shutuma halafu akang'ang'ania kubaki kwani kunampa kinga ya kutochunguzwa na kushitakiwa?
Mbon tunaongea vitu bila kutumia vyema ufahamu wetu?
 
Vyovote iwavyo hili swala me nalichukulia kama ni mpango wa kukiyumbisha na kukiharibu hicho chama Cha maticha.

Huwezi kwa wkt mmoja kuwaondoa kwenye nafasi zao katibu, Naibu katibu pamoja na Rais wa hicho chama kwa kigezo Cha uteuzi tena wa ukuu wa wilaya.

Nikweli inaweza ikawa sio vyema sn kukataa uteuzi wa Rais lkn tuangalie nyuma ya pazia uteuzi huo una agenda gani ya Siri nyuma yake kwa chama Cha maticha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…