Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Wezi wakuu halafu wakaaminiwa na Rais ili watumikie wananchi! Rudia kusoma ulichoandika
 
Ulisema haya kwenye ubunge tukakuona wajumbe wakikudhalilisha Pasco tunakufahamu vyema... ni vile hujapata wewe ukipata huwezi kataa.
 
Sasa unaitaki siasa ya nini kaka?
 
hao wapigwe chini wote walimu mnatuangusha watoeni hao watu nia zao sio nzuri kwanini wang'ng'anie hivyo hapo CWT kuna asali gani wameiona hapo.
Hao viongoz watatu wa CWT Rais, makamu, na katibu ili kuchaguliwa walizunguka nchi nzima wilaya zote kuomba kura. Hata gharama walizotumia wanaona hazijarudi. Ila wameshindwa kuona ya mbeleni.

Pili, kuna watu Tanzania hii hawana passion kabisa na siasa. Ama uongozi wa umma. Yaani hata ukimpa nini hagombei. Hata kama anajua fika atashinda kwa asilimia kubwa hagombei.

Ninashauri kuna vijana wengi wanapaza sauti zao na wana michango mikubwa sana kwa chama na karama za uongozi waangaliwe. Achaneni na kuwaangalia watu wenye vyeo na nafasi fulan kila siku. Ingawa Vitabu vitakatifu vimeandika mwenye nacho huongezewa.

Nawasilisha.
 
CWT siyo taasisi ya serikali. Ndiyo hapo tunaposema Katiba mpya ni muhimu. Rais anaingilia kila mahali na kila kona kama atakavyo. This is not right.

Kitendo cha Rais kuingia na kuwateua viongozi wa CWT ni njia ya kuwatishia na kuwapokonya madaraka yao kama wawakilishi wa Walimu.
 
Hii ni ramli chonganishi
 
Tunapomuomba Rais amfikirie Paschali katika teuzi zake hatutanii. Paschal ana sifa zote za kuwa kiongozi katika nafasi yoyote nchi hii: elimu, ujuzi, maarifa, uzoefu na udhubutu.
Ni kweli Ndg paschal ana mwelekeo sahihi. Pia ni mtulivu na mweledi. Tangu akiwa mtangazaji. Hii inatija kubwa sana sana.
 
Zamani nyakati za Nyerere mkuu wa Wilaya akiwa anaitwa Area Comissioner kilikuwa ni cheo chenye heshima sana. Mpaka mtu uteuliwe kuwa Area Comissioner lazima uwe ni mtu wa shoka sana. Lakini siku hizi, dah!
Nyerere alihakikisha wanakuwa watu wa zima wanaoheshimika. Aliwapeleka hata wazee wanaokaribia kustaafu waliokuwa matarishi ilmradi kukipe cheo heshima si kama siku hizi cheo hicho hakina maana kabisa ni kama cha vibaka kujifunzia uogozi wa umma.

Pia enzi za nyerere hakukuwa cheo cha DED, area commissioner ndiye alikuwa kila kitu akisisaidiwa na DAO-District Admin Officer.

Japo influence ya chama ilikuwa kubwa kupindukia
 
Mmesahau yule meneja wa Tigo nadhani kanda ya ziwa alichomoa UDC wa Ankali..?
huyo yuko sekta binafsi
Mwalimu mtumishi wa Umma unakataa uteuzi wa Mh Rais???!
Bossi wako?Mwajiri Mkuu wa Watumishi?
Wamedandia mtumbwi wa vibwengo vibaya mno

Kitawakuta kitu
 
kwani mshahara wa dc ni shilingi ngapi maana kwa tambo zao za kujiita waheshimiwa kama hawalipwi kuanzia 15mil nitashangaa sana
 
Kwa bahati nzuri sana safari hii wamepatikana watu ambao watakuwa mfano kwenye swala hili ili tusiendelee tena kuwa tunabishana bishan humu mitandaoni. Uteuzi wa mamlaka ya Rais huwa siyo hiari, ni lazima. Sema kuna ile room ya kuweza kutao udhuru na kuomba ateuliwe mtu mwingine ila SIYO KUKATAA. Bahati nzuri safari hii imepatikana sample ili tusiendelee tena kuwa tunabishana humu mitandaoni.
Baba nyumbani anakua-sign jukumu la kwenda shamba ukavune mpunga umekomaa, halafu wewe unakataa; unataka uende nani? Tupo wote, tutaona kitakachofuata baada ya hapo
 
Heri kuwa na kichwa kigumu kama changu kuliko kuwa kama unavyojidhania.
Ugumu wa kumshitaki utatoka wapi kwa kukataa teuzi?
Taratibu za uchunguzi hadi kushitaki zipo wazi kabisa, kama watachunguzwa au kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi ni lazima wakae Kando.
Kwamba mnaamini kuwa kwa kuendelea kubaki pale basi kama tuhuma ni legit bado hawatachukuliwa hatua?
 
kwa mshahara wa dc ni shilingi ngapi maana kwa tambo zao za kujiita waheshimiwa kama hawalipwi kuanzia 15mil nitashangaa sana
Kwa heshima ya ma DC naomba nisikutajie mshahara wao, utashangaa!. Mshahara wa top boss wao, rais wa JMT ni TZS. 9,500,000,
From DC to president kuna gap ya ngazi 10!. Mkurugenzi wa halmashauri ana mshahara mkubwa kuliko DC, mbunge ana mshahara mkubwa kuliko DC!. Hivyo kimshahara DC ni Bwana mdogo sana!. Mimi na kijikampuni changu cha PPR, namsaidia Samia kuwalipa mishahara ma dc wake kadhaa!. Ila pamoja na mshahara kiduchu wa DC, ana marupurupu mengi na posho nyingi zikiwemo posho za vikao, na posho za safari.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…