Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

MaDC wengi njaa tupu na ombaomba wa kutupwa. Wengine wanatembeza bakuli kwenye NGOs kuomba hela ya mafuta na service ya gari.

Kwa mtu mwenye steady stream(s) of income hawezi kukubali uDC tena huko nanjirinji ndanindani.

UDC sio kazi ya heshima maana unaweza kufutwa suddenly tena bila hata kuambiwa kwanini umefurushwa
 
Hiyo ya Malecela yalitokea lini?
 
CHAMA CHA WAALIMU WASHINDANA NA "RUHANI" ?

15 December 2022
Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre
Dodoma, Tanzaniap

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CCM Bara : Vurumai CWT, Mndeme awalipua " Msikubali kutumika na wenye nia mbaya "


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CCM Bara, Christina Mdeme amewataka walimu kutokubali mtu kuwaingilia na kuwavunjia umoja walionao. Mdeme ameyasema hayo leo Desemba 14,2022 wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) unaoendelea jijini Dodoma. “Mwalimu ni mzalendo namba moja, walimu tuendelee kusimamia uzalendo kwa manufaa ya Taifa, tusikubali mtu akatuchonganisha na tusikubali mtu akatuingilia na kutuondolea umoja wetu,”amesema Mdeme na kuibua shangwe kutoka kwa walimu hao
 
UDC? Hapana bhana.Atapelekwa Chaka balaa

Tunapomuomba Rais amfikirie Paschali katika teuzi zake hatutanii. Paschal ana sifa zote za kuwa kiongozi katika nafasi yoyote nchi hii: elimu, ujuzi, maarifa, uzoefu na udhubutu.
 
Kusema kweli anayeteua Wakuu wa Wilaya wala siyo Rais bali chawa! Ndiyo maana maadili siyo kigezo tena cha uteuzi.
 
Ukuu wa wilaya hauna dili?

Je , hawataki kufanya kazi dhuluma?

---
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.
 
Wanataka kuua chama cha waalimu.au hao jamaa ni mwiba.yaani wakireport tuu halafu wanatenguliwa.kazi inaishia hapo
 
Ndo madhala ya kuteua watu wenye ma vitengo yao tayari ya kupiga fedha (MICHANGO ya walimu nchi nzima) .
Kwani yeye ndo anafaa kuliko vijana wengine. Mtu mmoja anacover sehemu mbili as if nchi ina underpopulation ya skilled people. NDO maana watu wanataka kuchagua upinzani sio kwamba wao ni wema watatutendea mema la hasha tunataka kubadili walaji wa mali za nchi hii Kupitia KOFIA ya siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…