#COVID19 Watendaji na walimu wakuu wanavyoenda kuteseka na fedha za COVID‐19 za IMF

Hivi akili yako ipo vizuri kweli? Tofali 500 zijenge darasa gani? Halafu usifikiri ujenzi wa serikali ni kama unavyojenga wewe lazima kuwe na ubora, unapotosha usichokijua.
We ni mpuuzi unadhani wewe ndiyo wa kwanza kujenga darasa?
 
Lakini bado 12M haitafika mkuu
Soma ile BOQ ya mdau hapo juu, hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako lakini baada kuingia kwenye kamati ya ujenzi wa madarasa mawili shule fulani niligundua hiyo pesa haitoshi, nilikuwa naenda hatua kwa hatua narekodi kila kitu, baada ya kupiga hesabu nikagundua ujenzi ule ni wa gharama.
 
Darasa la watoto 40 tunaongelea au godown? maana hii kazi nimefanya sana tena sna kwa miaka 3
 
Darasa haliwezi kuzidi milioni 12
Toadie mchanganuo hapa ili tuone sio porojo zisizo na facts.

Sema hapa gharama za darasa moja kuanzia
1. Uchimbaji wa msingi
2. Matofali
3. Mchanga
4.kokoto
5. Mbao
6. Bati
7.misumari
8. Milango na madirisha
9.Nondo
10.Maji
11.Waya
12.Tiles
13.Wavu
14.Alminium
15.ufundi
 
Ml 20 darasa 1 mbona nyingi sana

Upumbavu mtupu na kutupotezea muda bila sababu

Milioni 20 najenga madarasa matano na hela inabaki
Umewahi kujenga hata banda la kuku
 
Wizi upo wapi hapo, huo ni mchanganuo tu ili hela ibalancr. Matumizi halisi yanaweza kuwa chini ya hapo au juu kulingana na hali halisi site na bei halisi ya vifaa
Nimepitia kama transaction 3 nikakutana na bei mara ndugu kwa eneo nililopo


Wacha nimalizie utafiti wa bei kwa Tz kwa ujumla
 
Tofali 500 x 1200 = 600,000, mawe lori 5 x 120,000 = 600,000, nondo 30 x 22,000 = 660,000, bati 40 x 30,000 = 1,200,000, cement 50 x 17,000 = 850,000, mchanga lori 5 x 100,000 = 500,000, misumari 20kgs x 6,000 = 120,000, fundi 1,500,000, mlango 200,000, madirisha 5 x 150,000= 750,000, maji 100,000, kokoto 300,000, vioo na ufundi 300,000, rangi na ufundi 500,000, nauli vifaa 100,000 dharura 1,000,000 jumla 9,280,00 na chenchi inabaki mkuu
 
150,000÷30=5,000
200,000÷30=6,667


Kama hii kwako ni kubwa sana jitathmini upya
 
Darasa la watoto 40 tunaongelea au godown? maana hii kazi nimefanya sana tena sna kwa miaka 3
Tofali 500 zinatosha hasa kama msingi ni wa mawe. Sababu ni hall na sehemu kubwa ni madirisha na mlango

Hao ni wezi tu wa kodi za watu

Kuchimba msingi hata wanafunzi wanaweza kuchimba
 
Kila sehemu wizi wizi tu wa mali za serikali

Kwanza jkt wanakazi gani hasa? Si wangekuwa wanajenga mashule huko?

Hata jwtz wana kazi gani hasa zaidi ya kuchukuwa mishahara ya bure tu?
 
Kama kuna watu wameambiwa hayo ni wapumbavu Sana ,ngoja tuone watakaojitolea..

Yangu lini mil.20 ikatosha darasa la kisasa na la viwango tena lenye furniture? Watapata wapi mafundi wa kujenga wakati mambo za force account zimewadhulumu mafundi na wamepigishwa Kazi kubwa bila malipo?

Tangu Lini mil.80 ikatosha bweni la watoto 80 tena likiwa limekamilika na vitanda vyake,umeme,mfumo wa maji taka na maji safi? Fundi yupi atakubali kukitolea?

Kuna wengine eti watatumia magereza na JKT.. Serikali iache utani ,hadi tunakwenda mitamboni suppliers na mafundi watadhulumiwa hadi akili zikae sawa.

Siwezi shiriki Kazi ambazo zitadhulumu.Kwa uzoefu wangu darasa moja angalau linaweza kamilika kwa mil.25 na bweni kwa mil.100 ,,niliofanya hizi Kazi nikaona kinyume na hapo ni kuzulumu sappliers wa vifaa vya ujenzi,kudhulumu mafundi na kulipua ujenzi kuwa chini ya viwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…