Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Tafuta na wewe Tawi lako uangue maembe.
Vinginevyo itaumiza kichwa chako bure Kwa kuwaza
Hikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!

Huu ni wizi wa mchana kweupe!

Mama yetu mpendwa anza na hawa nyani vinginevyo tutavuna mabua. Usiwahurumie hata kidogo. Kwa kuwa wao hawana huduma na kodi zetu,tengua viuno wote,including waziri wao kama hatachukua jukumu la kujiuzulu mwenyewe.
 
Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Mimi nazani hata waziri mkuu ajiuzulu huu wizi haikuanza awamu ya 6, ulianza awamu ya 5 na muasisi wake ni Doto James mpwa wa Mwendazake. Lakini alikuwa hana Ubavu wa kumgusa.
Nakumbuka Mange Kimambi alishaga onyeshaga vocha za malipo ya kazi maalumu na list ya majina ya watu. Doto akiongoza kwa kulipwa pesa nyingi. Waziri mkuu alikuwepo, Dr. Mapango Makamu alikiwepo mbona hawaku fanya chochote?.

Najua hata fanya uchungizi wa huko nyuma sababu ya kurindana.
 
Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ni dagaa? Yeye ndiye atajua vya kujibu maana sheria zote za matumizi ya fedha za serikali anazijua.

Ukisoma ile taarifa ni wao kwa wao ndiyo wanajilipa na utakuta kwenye kila malipo yeye pamoja na muhasibu majina yao hayakosekani.
Mara nyingi huu huwa ni mchongo tu hakuna kazi yeyote iliyofanyika au kazi wanafanya watu wawili ila kwenye kwenye malipo wanaandikana majina 20 ili kila mtu apate.
 
Nyie moderator wa JF acheni mambo ya ajabu. huu mtandao wenu ni user generated contents, Sasa kama kila tukipost humu mnaishia kufyeka contents zetu basi tuwaachie mtandao wenu muwe mnapost vile vinavyowapendeza nyie
 
Posho ya kuandaa ripoti ya mwaka hahahaaa
Kama waziri mkuu Kassim Majaliwa alikuwa hajui huu utaratibu basi inabidi ajitafakari sana. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa watumishi wa serikali kulipana posho kwa kazi nyingi za ofisini kama kuandika taarifa za mwezi na mwaka, kuandika hotuba za bajeti, kuandika taarifa mbalimbali za utendaji kazi zao nk.

Hakuna kazi serikali inayofanywa bila posho na hii imesababisha ugumu kwa viongozi katika kuwasimamia watumishi walio chini yao kama hakuna fedha. Bila posho kazi itafanyika kwa mbinde sana au huyo boss atoe ahadi ya posho pindi fedha itakapopatikana, na ahadi yenyewe iambatane na kuandikwa kwa vocha.

Kwa hiyo hii hatua anayotaka kuichukua waziri mkuu haitafanikiwa kwani posho hizi zilikwisha halalishwa wizara zote na watumishi wanajua kuwa ni haki yao. Vinginevyo asubiri mgomo baridi na ufanisi hafifu kutoka kwa watumishi.
 
watumishi wote wa Hazina wanatakiwa wawe waadilifu kwa kiwango cha juu.
vinginevyo watakausha hazina yetu
 
Katika mambo ambayo nilimshangaa mama,ni kumteua Mwigulu kuwa waziri wa fedha.Hapo nilikata tamaa kabisa na kuona mama hayuko serious.

Wizara ya fedha unataka mtu ambaye yuko committed, asiyekuwa mwamasiasa,mtendaji muadilifu asiyechoka.Si mpenda sifa na utukufu bali mnyenyekevu anayemcha Mungu.Mwigulu hana sifa hizo japo kidogo.

Nakuombea rais wangu Mungu awe nawe kwani najua kazi uliyonayo ni ngumu,ijapo sie tunaiona rahisi.

Kumbuka huyo ni mgombea urais.Atafanya chochote apate pesa ya kuandika maandishi ya kampeni kwenye mawe yote nchi nzima
Nakuunga mkono. Mwigulu anawaza jinsi ya kupata pesa za kuandika mawe na madaraja yote Tanzania.....hana kabisa uchungu na wananchi.
 
Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
What if yeye ndo ka blow hyo whistle
 
Wizarani kutamu
Hii inatisha sana!!!
wakati baadhi ya watumishi wanadai haki zao za malimbikizo ya mishahara tangu mwaka 2018 kumbe kuna watumishi hazina wanajilipa mamilioni kwa wiki mbili!!!
haki za watu wamezikalia, kwa hili Mungu hawezi kuwasamehe.
 
Sasa niulize nakumbaliana kwanza na maoni yako 10000% prof mussa assad cag retired apewe hii kazi, kile naona kaa sijakuelewi ni kutaja ummy mwalimu, je huyu mama ako na experience ya kuhandle financial matters, ile wizara sio kaa wizara zingine kaisa, infact katika mataifa yalioendelea au yanayojitambua waziri wa fedha ni kaa no 3 yaani president, vice , next ni finance chief, hii wizara inataka sio tu maswala ya hela ile vision and ability to negotiate na watu kaa world bank, imf and donors, hii sio wizara ya kuchezea, unaona kipindi cha mweda zake vile kina dotto waliichezea.lakini mimi naona uchafu ulikuweko wingi tena wakati wa dr mpango, kubuka mama samia kasema anataka report ya hela toka bot from jan- sijui april sikubuki, je wajua ni kwanini ile report haijawekwa hadharani????? a word to the wise is enough
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
Maana yake Dotto James anatakiwa kuhojiwa,maana nadhani kuna sahihi yake hapo.

by the way,nadhani wazirudishe hizo fedha kama malipo hayo hayako kwenye utaratibu kuliko kuwafukuza kazi.Ukifukuza kazi au kuwafunga ni hasara zaidi
 
Inapofika mahali waziri mkuu anaongea mambo ambayo waziri wa hiyo wizara angeongea maana yake huyo waziri hafai...tatizo mama yuko bize mitandaoni
 
Unaandika utopolo Dkt Mwigulu amekaa muda gan paleee???this is utter nonsense unayoongea
Wewe kama ni hawara wa Mwigulu Nchemba shauri yako, imekula kwenu.
Unachoweza kuandika ni vineno vya kiingereza tu!!

Unasema utter nonsense eti Mwigulu amekaa muda gani hapo?

Kumbe unakiherehere kama una tumbo la period huku una ahadi ya kutiwa na Mwigulu.

Sasa rudi kasikie kwanza clip ya PM Majaliwa iko YouTube. Majaliwa anasema wakiwa Mwanza sherehe za Mei Mosi, hao wafanyakazi wamelipana posho.

Sasa niambie nani alikuwa Waziri wa Fedha Mei 1, 2021?

Haya kavae pedi ulale
 
Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Assad ni kijana?
Uzi ulianza vizuri mwisho ukaonyesha unoya wako tena
 
Back
Top Bottom