Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Mkuu Pascal Mayalla hongera sana kwa hii makala, hakika wewe ni resource muhimu ndani ya jamii na JF.
Kiuhalisia, Mh. Mpango kaingia chaka sana ktk kulishughulikia hili suala.
Na kibaya kajibambanua kusema haogopi? Eti haogopi? Haogopi nini? Hamuogopi rais? Au?
Suala la walimu kwa Tanzania ni tete sana, lina maslahi mapana sana hasa kwa wapiga kula na zoezi la upigaji kura.
Mh. Mpango hajui iwapo hayo makontena yatapigwa mnada na walimu wakakosa hizo thamani maana yake itakuwa ni kete ya wapinzani kusema "walimu serikali haiwajali".
Mh. Mpango nadhani anajipalia makaa ya moto, very soon Naibu wake anakuja kuwa Waziri kamili wa Fedha!
Pumba.hujui hata tofauti ya "samani" na "thamani".hoja mwanasesere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
suala la kusema eti " wamezuia kwa kuwa wameendika jina la makonda" limenifanya kuona bandiko hili linaegemea upande flani

kwa nini aliandika jina lake, je hayo ya mwanzo yaliyo pita yalipita vp kwa nini haya hawakupenda yafate njia ya mwanzo yakapitia njia yake

hapa kulikuwa na dhamira ya kutaka kujinufaisha mtu
Hakuna kontena lilitolewa bandarini... yaan makontena yalipaswa kuwa 36 ila yaliyofika ni 20 tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika mle ndani kuza furniture tuu? Hujui kuwa makonda ni mshirika mkubwa wa wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya? Kama hujui kuwa huyu kijana ni jambazi jaribu kuchunguza mali anazomiliki kama zinaendana na kipato chake
 
Waziri amezungumza vizuri sana kuhusu kufuata sheria. Tatizo kubwa ni kuwa anayewateua wao hafuati sheria kabisa na sheria mojawapo asiyoifuta ni sheria mama yaani katiba ya nchi na pia kufanya maamuzi nje ya bunge. Hivyo si ajabu waziri akapata madhara kutokana na kusimamia sheria. Bashite ni kipenzi cha namba moja hivyo atalindwa kwa namna yoyote ile
 
Mkuu tumia busara tukiruhusu kila mkuu wa mkoa aingize msaada kwa mtindo huo itakuaje?Gambo nae ana misaada lukuki ya wamasai loliondo.Naomba jibu juu ya hilo.
Pia serikali ilishakataa kuingiza thamani toka nje ili viwanda vidogo vidogo kama keko wauze.

Pascal Mayalla
 
Mkuu Pascal Mayalla rekebisha andiko lako, kuna sehemu unasema kontena 16 zimetolewa tayari.... wakati uhalisia ni kwa kwamba hizo 16 hazijawasili kabisa nchini ila zinaonekana kwenye makabrasha....hivyo hakuna mzigo wowote wa Paul Makonda uliokwisha tolewa.

Au mimi ndio sielewi kuhusu hili saga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu Pascal Mayalla nimekusoma vizuri. you have got a point. but just.

tatizo hili kwa Makonda limekuwa self inflicted na yeye mwenyewe..... amesababisha maswali mengi kuliko majibu:

  • notice ya TRA ilipotoka mwanzoni kabisa, Makonda aliruka kimanga, hakutaka kuhusishwa na makontena yale. why?
  • makontena yalikuja kwa jina la Makonda binafsi na si kwa taasisi ya RC. again...why?
  • inaonekana Makonda hakumshirikisha yoyote serikalini kabla ya kuagiza haya makontena. begs the question...why?

there's only one explanation - Makonda is after glory. alitaka ionekane ni juhudi yake yeye binafsi.
huyu dogo asipopigwa break na ninyi Watanzania, mimi nakwambia awamu ijayo anaweza kuja kurithishwa kile kiti cha mfalme.

embu tuwe objective kama professionals. kusamehe ushuru kwenye makontena ambayo yamekubikwa na kiwingu cha maswali hayo hapo juu ni kutaka kuweka precedence mbaya sana kwenye utawala wa sheria, which is what my learned brother Dr Mpango anachokisema. Mpango ameongea very emotionally (inaelekea amechukizwa mno). japo amejitahidi kui contain hasira kidogo lakini there was this snarl on his lips and that twitch on the forehead which have given him away!
 
Kaka Paschal Afrika ni bara ambalo halina maarifa ya kutumia hazina za vipaji tulivyojaliwa na Mungu.

Ndio maana hata michezo tu inatuumbua. Itazame Ufaransa ya 1998 na hii iliyotwaa ubingwa kule Russia, ndio utagundua jinsi gani bara hili lilivyo jeusi.

Kuna yule profesa wa kisukuma alitoka Marekani akaja bongo kwa nia njema tu ya kuendeleza matibabu ya moyo. Akaja hapa akawa-discouraged mpaka akafa, hakupewa ushirikiano aliyostahili kuupata.

RC wa Dar kafanya aliyofanya kwa nia njema kabisa, jamaa zetu wa Diaspora wamefanya waliyofanya kwa nia njema kabisa.

Lakini upuuzi wa siasa zile zile za Afrika, ni adui mkubwa wa maendeleo yetu.
 
makonda kapokea maelekzo na mpango pia kapewa maelekezo na the same person,lengo ni kuwafanya watanzania wasihoji ishu nyengine wawafatlie ugomvi wao utaishia wapi,na mwisho itakuja kauli ya raisi huku mambo muhimu yakiwa yashatupita
 
Serikali moja, watumishi wote mali ya serikali kodi ni mali ya serikali na inakuja kutumiwa Na serikali ikiwa ni pamoja na samani hizi za mkoa wa Dar kichekesho ni pale serikali yenyewe inajifitini!

Waziri mpango hajitambui kabisaa na ni vzr akapimwa akili yake itakuwa na kasoro. Mbona juzi juzi tu walisamehe kodi kwa watu binafsi? Sheria ya kusamehe kodi pale serikali inapoona inafaa huwa inasamehe iweje kwa Vifaa vya shule za serikali za mkoa wa Dar inakuwa ngumu? Sitaki kuamini kwamba hapa pana chuki binafsi na siyo sheria,,maana sheria ya msamaha hapa inafanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichotakiwa baba k angepitisha bakuli kwa wadau wa elimu wachangie huku akiomba mda kila ikipatikana hela chache zinakombolewa,au angeziaddress hizo contena kupitia wizara ya elimu ili ziombewe msamaha,kuliko kupitia jina binafsi badala ya ofisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimsikiliza waziri mwenye dhamana, naona kama kuna contradiction ya ndani kwa ndani kama unatowa bn 20 kwanjiri ya shule hizo hizo, na umeakiki hizi samani nimisada na pia zinaenda pale pale unako paleka bn 20 kwanini unazikataza......hapo tatizo liko personal hataki mtoto teule aendelea kupata popularity nakupendwa na baba. Waziri kazi yake ingekua simple tu ni kusimamia kuona kwamba vinaenda kwa walengwa tu... aache kubishana na ujinga kasha boronga uchumi anafikiri watzn watampenda anajaribia kama alivo fanya kwenye korosho......watu wengine hawanaga maona anasema sheria ila azisomi zina sema je kuhusu misada kwajiri ya umma? Viongozi wa Africa wakipata madaraka wanakosa logic.

Sent using Jamii Forums mobile app
Je kila Mteule au Mpaka Mafuta kama awaitavyo Pasco atatumia cheo chake kupata Msamaha katika maswala yanayogusa idara yake hii nchi itapata mapato kweli?

Tukubali kwamba ni lazima nchi iongozwe kwa sheria tulizojiwekea.

Tukianza kuachana achiana mianya ya namna hii ndipo wapigaji huibukia humo.

Kama mzigo ulikuwa na malengo hayo na si kujitakia umaarufu wa kisiasa kwa nini haukuandikwa OFISI YA MKUU WA MKOA DAR na kuandikwa jina la mtu binafsi?

Dr. Mpango yupo sawa kabisa. Kama argument ya Pascali ni juu ya serikali kutoa bilion ishirini kwa ajili ya Elimu, na kuzuia samani ambazo zinaenda kusaidia elimu bure inamashiko basi hata hii ya mwanamchi kuchangia Sh. 20,000 kama kodi na serikali kupeleka miradi ya mabilioni fa fedha zaidi ya alichochanga mwananchi basi nayo ingekuwa ya mashiko!

Hawa wapakwa mafuta lazima nao watambua aliyewapaka naye anamoyo, anaweza kuwachoka kama alivyowahi kuwachoka na kuwatumbua wenziwe!
 
Hizo container 16 zilitokaje je nazo zilitumwa kwa jina binafsi la bwana yule? Je vifaa viliwafikia walengwa?

Usikute Dr Mpango ana full details za kuhusu container 16 ambazo zilitoka ndo mana hizi 20 zilizobakia wamezizuia na kukataa kuzipa msamaha wa kodi
 
Back
Top Bottom