Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,869
- 29,059
Pia kwanini mwanzo aliyakana tena kwa press conference kabisaHapo labda itumike ile lugha yetu ya nyumbani na usemi wa kijana wa nyumbani,lakini vinginevyo huyo bashite ni mpiga dili tu,kwa nini makontena yaje kwa jina lake?
Kama Ana details za hizo samani za containers 16 zilipokwenda na kama havikuwafikia walengwa aweke wazi.Vinginevyo ni Ujinga kuvizuia Vifaa hivyo.Hizo container 16 zilitokaje je nazo zilitumwa kwa jina binafsi la bwana yule? Je vifaa viliwafikia walengwa?
Usikute Dr Mpango ana full details za kuhusu container 16 ambazo zilitoka ndo mana hizi 20 zilizobakia wamezizuia na kukataa kuzipa msamaha wa kodi
Thubutu kwa taarifa yako mtanzania umtumie Hela kwa mradi wa maendeleo??? Hela yote atakula,Hawa jamaa wa marekani badala ya kununua vitu na kusafirisha tanzania kwanini wasingetuma ela kwenye mfuko wa kuchangia elimu madawati,Meza na viti vikatengenezwa hapa Tanzania, wanafunzi na walimu wakanufaika na ajira za kutengeneza zikapatikana?
Kuna mdau hapo juu kauliza,kama kila kiongozi katika Taasisi anayoiongoza akipewa zawadi iandikwe jina lake halafu ipite free bandarini,si itakua ni vurugu?Ukimsikiliza waziri mwenye dhamana, naona kama kuna contradiction ya ndani kwa ndani kama unatowa bn 20 kwanjiri ya shule hizo hizo, na umeakiki hizi samani nimisada na pia zinaenda pale pale unako paleka bn 20 kwanini unazikataza......hapo tatizo liko personal hataki mtoto teule aendelea kupata popularity nakupendwa na baba. Waziri kazi yake ingekua simple tu ni kusimamia kuona kwamba vinaenda kwa walengwa tu... aache kubishana na ujinga kasha boronga uchumi anafikiri watzn watampenda anajaribia kama alivo fanya kwenye korosho......watu wengine hawanaga maona anasema sheria ila azisomi zina sema je kuhusu misada kwajiri ya umma? Viongozi wa Africa wakipata madaraka wanakosa logic.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mie naona mpango ange hoji RC kwanini katumia majina yake badala ya kitumia office yake.....ila la maana kama Waziri ana mashaka na hiyo msaada aukabidhi wizara ya elimu ili iugawe kwa hizo shule kuliko kuazisha mgogoro, na wahisani watatushangaa kama kweli huo ulikua msada kwa ajiri ya shule zentu zenye hari mbaya.Kuna mdau hapo juu kauliza,kama kila kiongozi katika Taasisi anayoiongoza akipewa zawadi iandikwe jina lake halafu ipite free bandarini,si itakua ni vurugu?
Pamoja na nia njema yoyote,serikali inafanya mambo kwa taratibu mahsusi,vinginevyo uholela ungetamalaki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inaitwa nyoka kameza mkia wake.