Watoto wa Lemutuz walikataa kumsamehe baba yao...

Yaan ile text lemutuz utafikiri alikuwa anamuandikia Rafiki yake
Ni kama hakujali maumivu ya binti yake na akagongelea msumali kuwa alishinikizwa yaani kama anamfanyia favour mumtafuta. Imagine baba yako akuambie hivii baada ya kupotezana muda mrefu huku ukiingia insta yupo viwanja 24/7. Watu hawaelewi, dogo wa kiume alizingua ila wa kike hakutendewa haki
 
Halaf eti watoto wapate laana. Baba akosee halaf watoto wapate laana
Laana my ass
 

Teh teh teh, wanawake (siyo wote) huwa hawajielewi. Mimi binafsi tatizo siyo kulea watoto wa wengine. Bali mimi nichepuke, halafu mtoto wangu alelewe na wengine. Halafu mbaya zaidi nijue, halafu nifanane naye. Ni uchungu mkubwa sana. Na ili niepuke hilo, sichepuki.
 
Dah kumbe tupo wengi,hawa akina mama ambao wako na watoto wetu always ni wagomvi na washari. Yaan unajiuliza, tatzo hasa ni nini? Huyu wa kwangu hata nikituma pesa ya mahitaji ya mtoto,hatoi mrejesho wowote.. muda wote ni mkali,
Aiseee poleni
Ukali sbb haumtaki ,afanyaje ss
 
Aiseee ila huyo mwanamke ni mpumbavu sana!
Mi nimekuelewa,si wanawake wakati mwingine πŸ™Œ
Ila I'm sure hatakaa awe na amani ni suala la muda tu
 
I see, wonders shall never end!
Ndo mzazi mwenzio? Ashukuru Mungu hata unamtumia ,wengine hawatumiwi kabisaa!
 
Afadhali,nilitaka kuandika hivi!
Ila huyo dada , Mungu anamuona.
Kumbe ni mbongo aliyepelekwa huko na jamaaπŸ€” nilidhani mzungu?πŸ™Œ

Kweli ndo maana wanaume wengine,hawataki kusomesha mke,kumfanyia Chochote kizuri maana haya ndo matokeo!
Upelekwe USA,na kazi upate Bado umnyanyase aliyefamya ufike hapo!?πŸ™ŒπŸ™Œ
Uko sahihi kabisa,watu hawaangalii deep inside
 
Hao watoto mijing maana washapandikizwa chuki na
Mama yao

Ova
 
Nafikiri kuna kitu wengi wetu hatukizangatii; ila huko mbeleni kinatucost sana. Pamoja na yote ni muhimu kuobserve emotional stability +emotional intelligence ya mwenzi wako. Hakuna mtu aliye emotionally stable atakayefanya jitihada za kuumiza wengine kwa sababu tu yeye ameumia.

There is no separation that doesn't hurt; uwe umemuacha mtu au ameachwa. What matters ni jinsi ambavyo tunadeal na maumivu yetu.

Sasa ukiachana na mtu ambaye ni unstable emotionally; anachokuwa anafanya ni kuwa anatafuta mtu wa kumuhamishia machungu yake. Na kwa case hiyo wewe mzazi mwenza ndiyo unakuwa 1st victim au hata mtoto wenu au mtu yeyote ambaye ataona anaweza kuwa victim wake.(Wapo wazazi ambao wanatengana halafu unakuta mzazi mmoja anahamishia uchungu wake kwa mtoto wakr; mtoto atachukiwa hadi ajute kuzaliwa). Anachotaka kuona ni kwamba unaumia zaidi; na njia rahisi ya kukuumiza ni kupitia kwa mtoto wenu.

Under normal circumstances; hakuna mzazi mwenye akili timamu atakayejisikia amani kumuona mtoto wake ananyong'onyea na kuishi kwenye upweke, questioning his/her worth kwa sababu mama yake amemwambia baba yake hamjali, hampendi, amemtelekeza; ilhali baba anajitahidi kwelikweli kupambana kuwa kwenye maisha ya mtoto wake. Nothing breaks a parent's heart like seeing your kid down. Humsaidii mtoto wako unapomjaza sumu kuhusu mzazi wake mwingine. Ndiyo maana wapo wazazi ambao wanaweza kumdanganya mtoto kuwa hiki kitu kakutumia baba yako; kumbe baba hana hata habari huko aliko. Mzazi mwenye akili timamu atahakikisha analinda hisia za mtoto wake at any cost. Mtoto kukua huku akiwa anajua kuwa mzazi wake mmoja hamtaki/amemtelekeza is so traumatic.....Humjengi mtoto kwa kumwambia mapungufu au kumpandikiza chuki juu ya mzazi wake mwingine; unamuumiza mtu vibaya mnoo

Huyo mzazi mwenzako amebeba uchungu wake wa kutosha juu yako. Yote anayofanya ni kuhakikisha tu kuwa anakuumiza na kufanya watu wengine wakuone huna maana. Sasa usikubali amtumie mtoto wako kukuumiza; na wala usikubali kumtelekeza mwanao kisa ujinga wa mama yake. Wanaume kataeni mambo ya "huyo mtoto akikua atanitafuta mwenyewe". It's high time you fight tooth and nail kwa ajili ya watoto wenu. Usimuache mtoto akue akiwa na ombwe nafsini mwake kwamba baba alinikataa. Itafaa nini mtoto wako aje akutafute akishakuwa ameharibikiwa kisaikolojia au kitabia beyond repair; kisa your absence?

Huyo baby momma wako mpeleke ustawi wa jamii; deal naye kisheria period. Huko mtapewa maelekezo jinsi ya kumlea mtoto jointly. Na mtoto akishaaanza kupata ufahamu (kama bado ni mdogo sana) utaanza kufanya naye mambo kwa pamoja ili kucreate memories na kubond naye. Aone baba akimnunulia nguo, akimlipia ada na mengineyo. In the meantime, keep records of each and everything. Kuna wanawake usipodeal nao ruthlessly; ni mtoto wenu ndiyo atakuwa affected zaidi mwisho wa siku.
 
Aaah bina kwenye malezi tu nakuaminia; sina shaka na wewe. Sijui mtu unapata faida gani kuona watoto wako wanabeba uchungu juu ya baba/mama yao. Na watu wenye daddy issues wanapitia mengi jamani
 
Yaani tutajilaumu mpaka kesho na keshokutwa kukupoteza shem. Dah! Majuto ni mjukuu wallahi!
 

Kama kawaida yako, umeongea maneno mazito na yenye busara sana Mama Mchungaji. Mungu na Atusaidie tuwe wazazi bora kwa hawa malaika ambao tumewaleta hapa duniani bila hata ridhaa yao. Ni wajibu mtakatifu sana ambao inabidi tuuchukulie kwa uzito wa kipekee mno hasa wakati huu ambapo kuna influences mbaya karibu kutokea kila kona. Ni kama vile ulimwengu umekula njama kuishambulia taasisi ya ndoa na familia ambayo kimsingi ndiyo msingi wa maisha ya kistaarabu katika jamii ya binadamu.

Asante Mama Mchungaji πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…