Watoto wa Lemutuz walikataa kumsamehe baba yao...

hapa duniani, baba anayekupenda ni mtu wa muhimu sana hata kama ana mapungufu yake. kuna watu wanatafuta hiyo opportunity hawaipati kwasababu aidha walikua bial bila baba, alifariki n.k. pia, hata Biblia inasema waheshimu baba yako na mama yako, tena unconditionally.
 
Nilitaka kuandika hivi pia. Le mutuz alikuwa na chance kubwa ya kufix mahusiano yake na binti yake. Japo binti alikuwa na uchungu wa kutelekezwa na baba; still kwenye maandishi ulikuwa unaona kabisa angeweza kukaa chini akamsikiliza baba yake juu ya nini kilichotokea. Hata kama mama alikuwa ameshawapa version yake nyingine ambayo naamini ilikuwa inamkandamiza Le mutuz zaidi. Lakini yeye kujibu eti amemtafuta tu kwa sababu ya kushinikizwa na marafiki so hatohangaika tena daaah. So all this while yeye alikuwa anaona ni sawa tu kutokuwa na mahusiano mazuri na watoto wake.
All in all ni vyema kutafuta kuwa na amani na watu wote; hakuna kitu kinaumiza kama ushindwe kufix mahusiano yako na mtu then aje afariki... Ni kitu kibaya sanaaaaa
 
Thank you.
 
Huki choz likidondoka 😂😂😂😂 huchomoiii
 
Mi nishajionea hilo, wamama wanapenda tenganisha watoto na baba zao.
Wakikaa nao wanawalisha maneno mabaya mno
Mwisho mtoto naye anakuona mbaya.
Mi ndo maana nina utaratibu wangu, mtu akijifanya anamtaka mtoto akamhudumie kabisa, sitaki usumbufu
Watakuja nao kujionea maana wataoa wanawake kama mama zao ndipo wataelewa baba zao wanapitia nini.
 
Sasa unawafikiaje watoto mama mtu amewakumbatia masaa 24 na matoto yalivyo majinga sasa yanaona yakiwa na mama yao yanakuwa safe hayajiulizi yakianza kudindisha nani atayafundisha kuishi kiume kama sio baba yao. Badala yamtafute baba yao. Mapumbavu wahedi.
 
Dah kumbe tupo wengi,hawa akina mama ambao wako na watoto wetu always ni wagomvi na washari. Yaan unajiuliza, tatzo hasa ni nini? Huyu wa kwangu hata nikituma pesa ya mahitaji ya mtoto,hatoi mrejesho wowote.. muda wote ni mkali,
Kausha kaa kimya endelea kutoa matumizi. Save hizo sms. Akifika miaka saba nenda pale mahakamani kaombe mtoto wako. Sema mama ana influence mbaya kwa mtoto wako anamharibia ustawi wake kwa kumjaza masumu na kuongea vitu vya kumharibia mahusiano yenu yaani wewe na mtoto. Unataka mtoto wako ukamlee na mke mwingine.
 
Jitahidi kuweka kumbukumbu ya kila muamala unaofanya. Usimpe cash wala kununua vitu; tuma miamala tu. Atakayekulalamikia, mpe uthibitisho wa miamala. Wanawake wengine ni washenzi; anafikiri anakukomoa wewe; kumbe anamuumiza mtoto wake.
 
Jitahidi kuweka kumbukumbu ya kila muamala unaofanya. Usimpe cash wala kununua vitu; tuma miamala tu. Atakayekulalamikia, mpe uthibitisho wa miamala. Wanawake wengine ni washenzi; anafikiri anakukomoa wewe; kumbe anamuumiza mtoto wake.
nitatunza miamala mpaka lini mkuu,nimeamua itavyokuwa na iwe tu roho yangu imeanza kupata kutu.mwanzo nilikuwa namtumia kila week...ikaja tokea kuna week sikutuma na nilimpa sababu kwanini sikutumaa aisee nifuatwa ofisini nikafanyiwa fujo aisee nilishindwa vumilia nilimpa vitasa akanipeleka polisi nilazwe ndani bahati nzuri kile kituo wale polisi wananijua...anawalazimisha polisi nisweke ndani wakamwambia rudi nyumbani kesho utamkuta mtuhumiwa wako lock up oyrsterbay hahaha daaah hapo ndio akapata amani ya roho... wanawake wengine ni wametumwa kuharibu maisha ya wanaume
 
shida ya watu wengi mliolelewa na mama kama wewe, akili zenu zipo kama za wanawake, hata hamna tofauti.

Ungenijua ungefuta hiyo kauli, nina uhakika umelelewa mapajani mwa mama yako huku baba ako akitoka asubuhi na kurudi jioni unamuona.. Hujui lolote wala hujawahi kuvaa viatu vya hao watoto ila unajikuta una audacity ya kuhukumu..
 
Exactly na hicho ndo wengi wanafeli kuona, yule binti alikuwa anatamani kutengeneza bond na mzee wake ila pride ya le mutuz ilimuumiza zaidi. Watu hawajui kumkosa mzazi hata kwa miaka mitano inaumiza kiasi gani halafu umtafute au akutafute na kisha akuoneshe kuwa you are worthless in their lives, walahi vile vidonda vote vinaamka upya.
All in all naamini huyo binti hana shida sana labda huyo mtoto wa kiume alijibu shit
 
Sasa ndo wamtukane matusi kama suck my dick you ass nigga. Kweli mzazi hata kama kakukosea aje hilo sio tusi la kumpa
Nilishangaa sana mtu anamwambia mzazi wake hivyo .Yule bado mdogo akija kuoa akapitia changamoto ya kugawana mali au child support ataelewa.Na Mar nyingi haya mambo hujirudia alichofanya/kupitia mzazi na mtoto nae anaweza pita kulekule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…