mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Baaada ya kuona hali hiyo alijua mwisho wake hauko mbali miaka ya nyuma aligombana na mke wake na watoto sasa aliwatumia meseji kuwaomba msahamaha pia kuwaambia anaumwa hivyo anaomba msamaha.
Yale matoto yana roho ngumu yakamtumia zile meseji Mange Kimambi akapost kwenye ile app yake na Mange alifurahi maana watu hawa ni maadui akalipua hewani zile meseji.
Ila nadhani Le Mutuz alikuwa anaomba msamaha akijua tu huu mwisho wake umefika mara nyingi watu hupenda kuomba msamaha kabla ya mauti.
Watoto wa Lemutuz kama mnasoma ujumbe huu msameheni baba yenu aande kwa amani aliwakimbia marekani labda maisha yalikuwa magumu ....ASHAMPOO hapa.
Baraka za Mungu hupita kwa baba kwenda kwa mtoto
Na baraka sio pesa wala Mali, baraka ni maneno
Nilisikitika sana wale watoto kumtolea baba yao yale maneno na mama yao kukaa kimya
Wazazi, hata mzazi mwenzio akiwa mbaya kiasi gani kumbuka tuu watoto kumheshimu ni amri sio ombi. Tena ni amri pekee yenye baraka ndani yake. Ukimpenda mtoto wako jitahidi aheshimu watu wote haswa wazazi
Rest well Lembebiz