Watoto wa Mzee Malecela hawana bahati na Siasa kama ilivyo kwa Wana wengine wa viongozi wa CCM

Watoto wa Mzee Malecela hawana bahati na Siasa kama ilivyo kwa Wana wengine wa viongozi wa CCM

Ni mzee Malecela pekee katika wale wakongwe wa CCM ambaye hana mtoto mbunge.

Le mutuz aligombea ubunge wa Afrika Mashariki akafeli.

Ipyana RIP naye hakufika mbali.

Mwele tena mshumaa umezimika

Yule Anna Kilango alikuwa mwanasiasa kabla ya kuolewa na mzee Malecela, nakumbuka mwaka 2000 alimgaragaza mzee Keenja rip kwenye kura za maoni pale Ubungo sema tu Mkapa akaingilia kati Keenja akatimba bungeni

Ukifika bungeni utawakuta akina Jr kibao, kwa mfano Kawawa Jr, Nnauye Jr, Kikwete Jr, Mwinyi Jr, Makamba Jr, Lowassa Jr, Ditopile Jr nk...nk. amekosekana Le mutuz na Kinje tu.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Jumaa kareem.
Yupi kati ya hao aligombea na kushinda kihalali?
 
Alitokea udsm kama lecturer(academician) tatizo yeye alichagua uchumia tumbo kuliko proffesionalism na madhara yake hatodumu katika siasa na uenda huu ndo ukawa ubunge wake wa mwisho
Hakika hata mimi nimeona ilo na mama ameshamkataa
 
Wazee hawa walioishi kwenye nadharia za ujamaa kindakindaki , hawakuwekeza zaidi kwenye elimu na urithi wa watoto wao. Mifano ni mingi hata Mwl hakuwekeza huko zaidi ya ikulu kuwabeba.

Rip. Mwele, nakumbuka kisa chake na marehemu Maghufuli
Kuhusu kuwekeza kwenye Elimu Mzee Malecela muondoe. Hakuna mtoto wake asiye na Elimu ya chuo. Mwele amefariki akiwa Dr. utasemaje baba yake hakuwekeza kwake kielimu?
 
Ni mzee Malecela pekee katika wale wakongwe wa CCM ambaye hana mtoto mbunge.

Le mutuz aligombea ubunge wa Afrika Mashariki akafeli.

Ipyana RIP naye hakufika mbali.

Mwele tena mshumaa umezimika

Yule Anna Kilango alikuwa mwanasiasa kabla ya kuolewa na mzee Malecela, nakumbuka mwaka 2000 alimgaragaza mzee Keenja rip kwenye kura za maoni pale Ubungo sema tu Mkapa akaingilia kati Keenja akatimba bungeni

Ukifika bungeni utawakuta akina Jr kibao, kwa mfano Kawawa Jr, Nnauye Jr, Kikwete Jr, Mwinyi Jr, Makamba Jr, Lowassa Jr, Ditopile Jr nk...nk. amekosekana Le mutuz na Kinje tu.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Jumaa kareem.
Mzee Msuya , Mzee Salim, Mzee Warioba , Mzee Sumaye sijui Mzee Pinda, ila kuna familia nyingine siasa kwao siyo kipaumbele siyo lazma urithi kazi ya baba unaweza kurithi ya mjomba pia tena zaidi.
 
Back
Top Bottom