Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Hahaha mzee wangu na mama walitulea hivyo mi na mdogo wangu yaani ukikaa vibaya unachapwa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] Walipoacha hii kanuni kwa wadogo zetu wengine wamekuja kuwa wa ajabu sana wajeuri mno.
Sisi hadi sasa tukiambiwa kitu chaapu tunafanya na uzee wetu wale madogo watahoji hoji kama Chadema.
 
We jamaa noma sana
Sante mkuu
 
[emoji38]....ilikuwa ni balaaa ..
 
Kuchapa mtoto ni ujinga mwingine mwafrika anauendeleza.
No mkuu,inamsaidia kwa sababu usipomchapa utamwendekeza ujinga na atakudharau...coz kwa mtoto mdg nijuavyo mimi huwezi mshauri.AU UNASEMAJE WEWE,
 
[emoji38]..hongera nyingi zikuendee mkuu
 
Ukitumwa ukamaliza nusu saa utachapwa,

Ukienda kuzurula kwa jirani utapigwa tu,

Ukipanda juu ya miti narudia kusema utapigwa tu,

Usipokunywa dawa utapigwa tu..

Ikisadikika umetukana utapigwa tu hata mtu ukihisiwa,



Etc etc
 
Unacheza mpira au komborela mpaka giza linaingia,hamna anayekuuliza.

Ukirudi umejikausha ktk kochi unasubiri ubwabwa,huku na kibaridi kingi bimkubwa analiamsha dude.kosea useme maji ni ya baridi utalala vibaya siku hiyo,inabidi uende kinyonge kwenda kujipaka maji na kunawa miguu,ila ukitoka bafuni ukaguzi unakuhusu.
 
Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
dah aya mambo haya umenikumbusha mbali sana, nailikua ivyo kweli nilikua nakosa amani sana kukosa haki ya kujieleza, mpaka leo katika vyote hiki naonaga nilionewa sana bora makosa mengine nichapwe tu
 
Vitoto vya siku hizi kikiguswa tu kinakupeleka dawati. Tunajenga jamii gani. Ndio maana wengine wanashabikia maandamano bila kujua hata lengo la maandamano sababu hawakuchapwa.
 
Siku hizi haki za watoto zinazingatiwa sana...

Na pia utandawazi umepelekea hayo yote kuonekana ya kawaida...

Siku hizi unakuta mtoto anajibizana na baba au mama yake kisa remote ya TV...

Cc: mahondaw
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Siku hizi haki za watoto zinazingatiwa sana...

Na pia utandawazi umepelekea hayo yote kuonekana ya kawaida...

Siku hizi unakuta mtoto anajibizana na baba au mama yake kisa remote ya TV...

Cc: mahondaw
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…