Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,855
- 189,385
Sawa mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji38][emoji38][emoji38]Ayo mambo ya kiccm ..Mimi nimuhenga lakin siajapitia ayo mambo ...uku dar amnaga
Hatarkumaliza siku bila kipondo ni bahati
[emoji115] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mpaka mbavu zinauma. Umenikumbusha mbali sana, dah!1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa..
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila ya wakubwa,utachapwa
31.Ukinawa bila ya wakubwa,Utachapwa
32.Ukimaliza kula ukanyanyuka bila ya wakubwa,Utachapwa
33.Umechelewa kutoka dukani,Utachapwa
34.U..........
KAMA UMEPITIA MALEZI HAYA NA UKAKOSA HESHIMA BASI WEWE NI KONKODIII