Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ila tumechapwa aiseee duuu,nikikumbuka sina hamu kabisaaaa.

Hawa wa sasa hivi mayai tu!
 
Mithali 22:15

Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

Ama kweli wazazi wetu walikua wacha Mungu sana.
 
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.

Mhenga Ongezea...
umenikumbusha kwao na mshikaji wangu before hawajatenga msosi kama Mzee wao yupo wanaanza kumuimbia alikuwaga anajiita gadafi.
 
ukimgegeda mtoto wa jirani utachapwa
ukichelewa kuhesabu namba shule utachapwa
ukichelewa kuingia darasani baada ya break utachapwa
 
í ½í¸í ½í¸í ½í¸ mkuu ongeza mtu mzima akijamba sawa ila wewe ukijamba una hatua na lazima uchapwe tu.
 
Back
Top Bottom