Watoto wawili wa familia moja wapotea baada ya kuaga wanakwenda shule Julai 24, 2024

Kwakweli umasikini usiwe kisingizio cha negligence ya kiasi hicho, mtoto wa miaka mi4 ni wa kumuacha akavuke barabara bila msimamizi? Hakafu likitokea la kutokea mtu analia kabisa yaan.., utadhani sio yeye aliyewaacha wajisimamie..
 
Mungu watunze hawa watoto. Tumeshindwa kuwatunza wanasakwa kama wanyama. Wanapotea kama pin. Watunze mwenyezi Mungu kama upo.
 
Hii sasa imeshakuwa zaidi ya hatari.
Nikijaribu kuwaza nje ya Box, nahisi huenda ni zaidi ya uchaguzi.
Huenda kuna kundi Fulani Lina interest na hawa watoto, linawatumia either kama nguvu kazi, au Kwa manufaa mengine.
Serikali tunaomba itilie mkazo.
 
Mbona watoto wake huyo mama kawaanzisha shule mapepo alikuwa anakimbilia nini?
Miaka 9 darasa la 5 hapo dogo anamaliza chuo akiwa mdogo hawezi kujipambania. Asipotafutiwa ajira na mjomba anakuwa mtoto wa kula andazi kwa mama huku ndani ana degree
 
Waanze na hilo daladala, waulizwe walipowashusha
Hii ni sawa. Naunga mkono hatua hii. Tena waseme walishuka na nani mahali ambapo sio shuleni?? Hapo waliposhushiwa na aliyeshuka nao pamulikwe vizuri.
Unamshushaje mtoto wa shule mahali ambapo sio shuleni?
 
Yaani shule ndio kwanza zimetoka kufunguliwa july hii ila kwa hali hii unatamani hata zifungwe tena mpaka uchaguzi uishe. Wanasiasa tunaomba watoto wetu wasome kwa amani plz,kama vipi toeni hao wa kwenu mliowazaa😡
 
Hii sasa imeshakuwa zaidi ya hatari.
Nikijaribu kuwaza nje ya Box, nahisi huenda ni zaidi ya uchaguzi.
Huenda kuna kundi Fulani Lina interest na hawa watoto, linawatumia either kama nguvu kazi, au Kwa manufaa mengine.
Serikali tunaomba itilie mkazo.
Hili linawezekana kabisa. Kuna mahali nilisoma article inasema watoto 7-14yrs. wanatekwa na huko wanakopelekwa huwekwa kama watumwa wa kingono, kutumikishwa kazi kandamizi e.g. majumbani, migodini au majumba ya starehe(Cassino) au kuuzwa kama bidhaa - kibiashara.
Mungu aturehemu na kutuepushia hii balaa. Inauma na kusikitisha sana.
 
Nilirudi nyumbani kulala na asubuhi nilikwenda tena shule kuulizia wakasema hawajawaona, ndipo nikarudi tena Polisi.
UNAPATAJE AMANI NA UTULIVU UKALALA, HUKU HUJUI WATOTO WAKO WAPI?

Hii sheria/utaratibu wa kusubiri yapite masaa 24, hatuwezi kuibadirisha hasa kipindi hiki cha wimbi la watoto kutekwa?
Hatua za mwanzo za kusmbaza picha za watoto zinge anza.
kukagua magari yote yanayotoka nje ya mji.wilaya, mkoa
 
Yaani shule ndio kwanza zimetoka kufunguliwa july hii ila kwa hali hii unatamani hata zifungwe tena mpaka uchaguzi uishe. Wanasiasa tunaomba watoto wetu wasome kwa amani plz,kama vipi toeni hao wa kwenu mliowazaa😡
Wahenga Walisemaga "Kikulacho ki nguoni mwako" Kama Usalama wa Raia wakichachamaa na kulikomalia jambo hili (wakilishikia bango)naamini watoto watapatikana. Vinginevyo washirikishwe (lakini kwa malipo)bodaboda na vijana wengine wanusaji.
 
Kwakweli umasikini usiwe kisingizio cha negligence ya kiasi hicho, mtoto wa miaka mi4 ni wa kumuacha akavuke barabara bila msimamizi? Hakafu likitokea la kutokea mtu analia kabisa yaan.., utadhani sio yeye aliyewaacha wajisimamie..
Saa ingine sjui ni Hali ya kutojalii sjui hata
 
Hii Sheria /Utaratibu (wanavyodai Polisi)ni kwamba wanakupa muda kwa wewe kujiridhisha kwamba fulani amepotea. Kwa upande mwingine hili sio sawa kwani ni kama kumpa nafasi mhalifu-mtekaji azidi kusonga mbele au kuficha uovu wake.
Kuibadilisha ni jambo jepesi sana. Ni Wakubwa watamke tu.
 
Serikali itangaze hali ya hatari na kufunga shule zote, watoto wetu hawapo salama.
 
Mungu watunze hawa watoto. Tumeshindwa kuwatunza wanasakwa kama wanyama. Wanapotea kama pin. Watunze mwenyezi Mungu kama upo.
Hii komenti yako imenifurahisha sana.

Hii komenti yako inadhihirisha kwamba,

Watu wengi mna mashaka na uwepo wa huyo Mungu mnaye aminishwa na kuhubiriwa kila siku kwamba ana upendo na ulinzi wa kutosha kwa watu.

Ilhali kiuhalisia hayupo, Ndio maana matukio kama haya hayawezi kudhibitiwa au kukomeshwa kabisa na huyo Mungu anaye aminiwa yupo mwenye ulinzi na upendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…