Watoto wawili wa familia moja wapotea baada ya kuaga wanakwenda shule Julai 24, 2024

Watoto wawili wa familia moja wapotea baada ya kuaga wanakwenda shule Julai 24, 2024

Vipato havilingani Bora huyo anaweza walikua daladala kuna wanaotembea kwa miguu tena umbali mrefu
Halafu ndo utaratibu (inavyoonekana) aliouzoea kuutumia wa kila siku kwa watoto hao. Hapo naona waulizwe vizuri konda na dereva wa hiyo daladala. Kama na hiyo daladala itatoweka/haitaonekana kwenye utoaji wa huduma, basi Tajiri/mmiliki wa hiyo daladala naye aulizwe.
 
Watoto wawili wa familia moja wamepotea katika mazingira ya kutatanisha mkoani Arusha, baada ya kuaga wanakwenda shule jana Julai 24, 2024, lakini hawakurudi nyumbani na mpaka leo hawajaonekana popote.

Watoto hao wanaosoma Shule ya Msingi Olosiva, wilayani Arumeru, wamedaiwa kupotea baada ya kupandishwa kwenye daladala wakielekea shuleni, lakini hawakufika shule na wala hawakurudi nyumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amethibitisha kupokea taarifa hiyo leo Julai 25, 2025 asubuhi na wameanza kuifanyia kazi.

“Tumepata taarifa hiyo leo asubuhi na tunaifanyia kazi, tutakapopata chochote cha kuwaeleza tutawaambia kesho,” amesema SACP Masejo.

Akisimulia tukio hilo leo Alhamisi Julai 25, 2024, mama mzazi wa watoto hao, Elizabeth Modesta (31), amewataja watoto hao kuwa ni Mordekai Maiko (7) anayesoma darasa la tatu na Masiai Maiko (9) anayesoma darasa la tano.

Amesema jana aliwaandaa kwenda shule kama kawaida na kwenda barabarani kuwapakia kwenye daladala kuelekea shuleni.

“Kawaida saa 9:30 hadi au saa 9:45 jioni wanakuwa wamefika, lakini jana hadi saa 10 walikuwa hawajafika. Niliamua kwenda shule saa 11 jioni kuulizia nikaambiwa tangu asubuhi watoto hao hawajaonekana shule. Nikachanganyikiwa na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi Ngaramtoni,” amesema mama wa watoto hao.

Amesema alipofika polisi walimtaka arudi nyumbani na kusubiri hadi saa 24 kama wasipoonekana ndio arudi kwa ajili ya kukata ripoti namba (RB Namba) na kuanza kutafutwa.

“Nilirudi nyumbani kulala na asubuhi nilikwenda tena shule kuulizia wakasema hawajawaona, ndipo nikarudi tena Polisi, nikapewa RB namba NGT/RB/1265/2024, wakataka picha za watoto, ili wasambaze mitandaoni na namba yangu, nikawapa, sasa nasubiri majibu,” amesema Elizabeth.

Mama huyo ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali na wananchi kumsaidia kuwapata watoto wake popote watakapoonekana.

“Kwa sasa napiga tu simu kwa marafiki wanisaidie kusambaza picha za wanangu, maana nimetembea kila mahala siwaoni. Naomba walimwengu wanisaidie, popote watakapowaona wanangu wanisaidie kuwapeleka polisi, maana nafsi yangu kwa sasa imeinama kwa kweli, namwomba tu Mungu wasidhurike huko walipo hadi niwapatikane,” amesema huku akilia kwa uchungu.

Mkuu wa shule ya msingi Olosiva, Mwenzine Msuya amesema tangu jana watoto hao wanajaonekana shuleni na leo wameuliza wanafunzi kwenye halaiki ya asubuhi (paredi), lakini wamesema hawajawaona.

“Hawa watoto hawana tabia ya kutofika shule kabisa na hata jana mama yao alipokuja kuuliza tukashangaa na leo asubuhi pia amekuja, hawapo. Tunaendelea kusambaza picha kwa ajili ya kutoa taarifa za kupotea kwao, yoyote atakayewaona awasiliane na mama yao au kituo chochote cha Polisi,” amesema mwalimu huyo.

Chanzo: Mwananchi
Nafill maumivu ya huyo mama
 
Mungu asaidie wapatikane wakiwa wazima.!!
Hii dunia sijui inaenda wapi?
 
Hii komenti yako imenifurahisha sana.

Hii komenti yako inadhihirisha kwamba,

Watu wengi mna mashaka na uwepo wa huyo Mungu mnaye aminishwa na kuhubiriwa kila siku kwamba ana upendo na ulinzi wa kutosha kwa watu.

Ilhali kiuhalisia hayupo, Ndio maana matukio kama haya hayawezi kudhibitiwa au kukomeshwa kabisa na huyo Mungu anaye aminiwa yupo mwenye ulinzi na upendo.
Cheka tena
 
Hii komenti yako imenifurahisha sana.

Hii komenti yako inadhihirisha kwamba,

Watu wengi mna mashaka na uwepo wa huyo Mungu mnaye aminishwa na kuhubiriwa kila siku kwamba ana upendo na ulinzi wa kutosha kwa watu.

Ilhali kiuhalisia hayupo, Ndio maana matukio kama haya hayawezi kudhibitiwa au kukomeshwa kabisa na huyo Mungu anaye aminiwa yupo mwenye ulinzi na upendo.
Mkuu; kumbuka Mungu hadhihakiwi. Ukipenda(sio lazima) kaisome Gal.6:7-9
Awepo au asiwepo ww una hasara gani? Wewe mwache Mungu aitwe Mungu ww katafute pesa -na Inatosha.
 
Mkuu; kumbuka Mungu hadhihakiwi.
Wewe ndiye unasema, haya ni maneno yako tu na vitisho mlivyo pumbazwa vizazi kwa vizazi.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe aseme hadhihakiwi.
Ukipenda(sio lazima) kaisome Gal.6:7-9
Awepo au asiwepo ww una hasara gani?
Sina hasara yeyote, Niko hapa kukosoa habari za uongo kuhusu huyo Mungu mnayedai yupo ilhali kiuhalisia hayupo.
Wewe mwache Mungu aitwe Mungu ww katafute pesa -na Inatosha.
Kwani aliyekwambia sina pesa ni nani?

Mpaka unasema nikazitafute, Au unadhani kila mtu ni maskini wa kumwambia akatafute hela?
 
Mkuu; kumbuka Mungu hadhihakiwi.
Wewe ndiye unasema, haya ni maneno yako tu na vitisho mlivyo pumbazwa vizazi kwa vizazi.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe aseme hadhihakiwi.
Ukipenda(sio lazima) kaisome Gal.6:7-9
Awepo au asiwepo ww una hasara gani?
Sina hasara yeyote, Niko hapa kukosoa habari za uongo kuhusu huyo Mungu mnayedai yupo ilhali kiuhalisia hayupo.
Wewe mwache Mungu aitwe Mungu ww katafute pesa -na Inatosha.
Kwani aliyekwambia sina pesa ni nani, Mpaka unasema nikazitafute?

Au unadhani kila mtu ni maskini wa kumwambia akatafute hela?
 
Watu wamegeuka kuwa ni zaidi ya Lusiferi. Hawana kabisa hofu ya Mungu na wala hawajiulizi kwamba "Hivi ingekuwa ni mimi ningefanyaje"? Hao watoto malaika/innocent hawana hata uwezo wa kujitetea wanadhulumiwa tuu.
Huruma sana
 
Watu wamegeuka kuwa ni zaidi ya Lusiferi.
Lusiferi hajawahi kuwepo na hayupo.
Hawana kabisa hofu ya Mungu
Huyo Mungu Alishindwaje kuweka hofu kwa kila kiumbe kiwe na hofu juu yake?
na wala hawajiulizi kwamba "Hivi ingekuwa ni mimi ningefanyaje"? Hao watoto malaika/innocent hawana hata uwezo wa kujitetea wanadhulumiwa tuu.
Hao watoto wanadhulumiwa kwa vile huyo Mungu mnayedai ni mwema, mwenye ulinzi, mwenye upendo na huruma kwa watu wake Hayupo.
 
Nilirudi nyumbani kulala na asubuhi nilikwenda tena shule kuulizia wakasema hawajawaona, ndipo nikarudi tena Polisi.
UNAPATAJE AMANI NA UTULIVU UKALALA, HUKU HUJUI WATOTO WAKO WAPI?


Hii sheria/utaratibu wa kusubiri yapite masaa 24, hatuwezi kuibadirisha hasa kipindi hiki cha wimbi la watoto kutekwa?
Hatua za mwanzo za kusmbaza picha za watoto zinge anza.
kukagua magari yote yanayotoka nje ya mji.wilaya, mkoa
Hii ni mbaya sheria za kikoroni hizi, hayo masaa 24 waarifu wanayatumia kuvusha watoto boda au kwenda nao mbali, wakati taarifa ingetolewa mapema pengine wangeonekana na kuokolewa
 
Bi mkubwa anasema hizo ni drama.

Huyu IGP kama anashindwa kulinda Raia ni wa kazi gani??
 
Wewe ndiye unasema, haya ni maneno yako tu na vitisho mlivyo pumbazwa vizazi kwa vizazi.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe aseme hadhihakiwi.

Sina hasara yeyote, Niko hapa kukosoa habari za uongo kuhusu huyo Mungu mnayedai yupo ilhali kiuhalisia hayupo.

Kwani aliyekwambia sina pesa ni nani, Mpaka unasema nikazitafute?

Au unadhani kila mtu ni maskini wa kumwambia akatafute hela?
min -me kumekucha kaka kashaanza huku
 
 
Hii Hali naona kama inataka kuzoeleka. Serikali hasa vyombo vya ulinzi na usalama visipokuwa makini raia watapata tabu sana.
 
Back
Top Bottom