Watoto wetu wa Siku hizi 'wamerogwa' au 'wamelaaniwa' na nani hasa kimalezi, kiuwajibikaji na kimaadili?

Umenikumbusha mbali jembe la kukota na ng’ombe unaamka saa 10 kufunga jeki unalima hadi saa tatu. Ni mwendo wa kuhemerya si ntugho 😀😀😀

Ukizembea unakutana na mujeledi kwenye mgongo..
 
Mada murua sana.. Mie watoto wote mpka wa miaka minne. Anakula na kutoa vyombo mwenyewe... Pia kazi ndogo kama kamwaga maji namuita kudeki...

Nadhani sie wazazi au walezi ndio tunaharibu watoto...


Napenda sana mada hizi.. Kongole...
 
Mkuu hata kama kuna Dada wa kazi hapo Nyumbani,lazima na Watoto nao wajuwe kuwajibika au kumsaidia Dada kazi, maana Dada nae ni Binaadamu anaweza uguwa! Je kwa hiyo shughuli za Nyumbani zitasimama hadi Dada apone wakati una vijana hapo Nyumbani!?
Do you think that 'authentic Moron' can understand you Chief?
 
Zamani hata mke wa kaka akifa dogo unachukua mzigo, Zamani machief wakifa tulizika na vigori wao wazima.... Zamani Baba na Mama wote walikuwa wakulima na hushinda nyumbani zaidi ya 50% ya maisha yao....

Bwana Genta, ni mfumo tu wa maisha kubadirika, ndio maana hata malezi yamebadirika... siku hizi mama muajiriwa, baba muajiriwa wote hurudi nyumbani saa moja usiku....
 


Wavulana Vs Wasichana
Vijana Vs Binti
 
Hii ya kudekeza watoto ni utamaduni mbaya sana, mtoto aliyekulia mazingira ya kujishughulisha kidogo huchangamka na kuwa imara sana linapokuja suala la kujitegemea.

Lakini hawa wanaodekezwa huwa hawana jipya sana, zaidi ya kuwa goigoi na hata kujitegemea kimaisha huwapa ugumu sana.

Wito wangu kwa wazazi hata Kama ni akina maisha Safi, Basi tujitahidi watoto angalau siku za weekend wamwagilie basi maua
 
Kwahili mkuu wazazi tunawajibika kubeba lawama, ndio maana tangazo la serikali mwezi December kupiga marufuku tuition wakati wa likizo kubwa nimeliunga mkono mia kwa mia, watoto wabaki majumbani wajifunze skills za kijamii.

Mimi baada ya hawa wadada wa kazi kuzinguwa sasa hivi sitaki dada wa kazi wa kukaa naye, kazi za nyumbani tunafanya wote, mimi Father house ni mpishi mzuri sana experience nimeipata wakati nabeba box ughaibuni, watoto wote wanajuwa kupika basic African food, mama yao anaingia jikoni anapotaka kutengeneza masotojo ya kufa mtu.

Nyumbani kwangu ni sheria ukimaliza kula osha vyombo vyako weka kabatini na mimi ndio namba moja katika hilo kuwaonesha mfano kwa vitendo, pili ukitoka chumbani zima taa, tatu ukiwa unaoga ukijipaka sabuni funga kwanza shower then ndio ufunguwe shower kujisuuza, mita ya Luku ikizidi unit 6 kwa siku lazima nipate maelezo ya kuridhisha imekuwaje.

Wife anamleta day waka wa kufanya usafi kwa wiki mara moja au kila baada ya wiki mbili huyu ndio atafanya usafi muhimu tu labda na kuosha masufuria na kufuwa nguo, mapazia na mengineyo analipwa chake anasepa mpaka tumpigie simu.

Lakini pamoja na yote hayo bado naiona gape ya kimalezi kwa watoto wetu wa sasa.

Na tatizo kubwa tumewaachia walimu mashuleni watulele watoto huku tukisahau walimu wenyewe nao wamejaa stress kibao.

Niko barabarani nitarudi hapa nilipoishia
.....
 
Wazazi wa siku hizi wamezidi upopoma aisee, ndio maana hata watoto wao wapo hovyo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama muajiliwa halafu bill zote kwa Baba, kama si uhayawani huu ni nini?

Kwa nini kina mama nao wasife mapema na hawapati stroke kama Wababa?
 
Mada murua sana.. Mie watoto wote mpka wa miaka minne. Anakula na kutoa vyombo mwenyewe... Pia kazi ndogo kama kamwaga maji namuita kudeki...

Nadhani sie wazazi au walezi ndio tunaharibu watoto...


Napenda sana mada hizi.. Kongole...
Actually haya mambo ya self reliance ndio ilitakiwa wafundishwe watoto wa kindergarten. Wajue kutandika vitanda vyao na kuosha sahani baada ya kula. Sio kuwabebesha marundo ya madaftari
 
Kwenye mabano yako (Vijana na Mabinti).
Ulilenga nini?
Means mabinti sio Vijana?
Hahaa! Mkuu ametumia maudhui ya kizamani, zamani mwanamke lazima atambulishwe kupitia jinsia yake.
ulikuwa uwezi kumwita mtoto wa kike kijana wangu. Hata kwenye vitabu vya dini mfumo huu umetumika sana.
Mf. kutoka 20:10, kutoka 32:2
 
Nimecheka sana hapo uliposema Mtu akioga anatakiwa akijipaka Sabuni Kichwani ahakikishe amefunga Bomba na siyo Kumwaga Maji hovyo.

Nahisi Maisha ya Kwako na ya Kumbi zetu za Mafunzo ya Kijeshi hayapishani sana. Yaani kila nikirejea Kusoma hii post yako navunjika tu Mbavu kwa Kucheka.
 
Hii ndilo tatizo..umaacha malezi yote kwa mdada wa kazi yeye ndie ajue kama mtoto anaumwa au la, mtoto amefanya kazi za nyumbani alizopewa shule au la, dada wa kazi ndie ajue mtoto anacheza wapi na nani? ndio maana siku hizi visa vya watoto wa kiume kuwa mashoga vimeongezeka, na watoto wa kike kuanza kujishughulisha na mapenzi wakiwa na umri mdogo..maana wazazi wako "busy" kutafuta maisha bora ya hao watoto bila kujali makuzi yao!

Mimi zamani watoto wangu ilikuwa ikifika wakati wa kula chakula watakuja mezani watapakuwa kisha kila mtu atatafuta sehemu yake anaenda kula...nilona hilo ni tatizo sasa hivi sote twala hapo hapo mezani....hii imeniwezesha kujua table manner zao lakini imenipa nafasi ya kuwa nasikiliza matatizo yao na pia kuwapa ushauri!
 
Hiyo ni new version tu, old version wakati tunaogea kopo wazazi walikuwa wanatunyowa nywele, tusifuge minywele ya kumaliza sabuni.

Kwa sababu tunapunguza bill ya Dawasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…