Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Mafuriko yanatokea pale maji yanapozidi uwezo wa eneo husika kuyashikilia. Hata miundombinu iwe bora vipi, yakizidi kipimo hakuna namna ya kuyazuia.
Tanzania hii Kuna miundombinu gani? No mipango Miji,watu wamejenga mabondeni tena sehemu zingine serikali imepima,Kuutupa taka hovyo,kulima kwenye mikondo ya maji,hakuna mifereji na upuuzi kama huo..

Acha inyeshe tujue inapovuja.
 
Mara nyingi mto msimbazi hujazwa na maji toka mvua za morogoro, hivyo, daresalamu inaweza isinyeshe mvua kubwa lakini mto ukajaa, tena kwa bahati mbaya haya hutokea usiku wakati watu wamelala, tuwe makini sana sisi wakongwe wa jiji tunafahamu hili sana.

==== ====

Mvua kubwa iliyonyesha usiku kuanzia majira ya saa nane hadi alfajiri, imesababisha mafuriko na kuleta hofu kwa madereva kuendesha magari katika maji hayo yanayokatisha juu ya barabara ya Morogoro - Dodoma.

Chanzo: ITV
Mto msimbazi maji yake hutokea Kisarawe na maeneo jirani sio Morogoro. Maji ya Morogoro huingia mto Ruvu na kuelekea Bagamoyo na sio DAR
 
Fair enough, tujadili kwa facts mafuriko haya ya Morogoro, kwanza tupate kiwango cha mvua iliyonyesha,pili tuangalie hili jiji Lina drainage systems inayofanya kazi? Wakazi hawajajenga kwenye njia asili za maji kupita? Ule mfereji mkuu unaopita Morogoro umesafishwa? Wakazi wana uelewa wa kutotupa uchafu kwenye mifereji na chemba?Je jiji lilishajiandaa kukabiliana na mvua? Tuyajadili haya ili tuone mafuriko haya tungeweza ku limit athari zake au la
Usijichoshe ni hakuna,hapa Tanzania Kila kitu kinafanywa Kwa kubahatisha
 
Kuna maeneo ya Mkundi Watu wamejenga kabisa kwenye Mkondo wa maji na wamejiami kwa kujenga kuta. Maji ata ikipita miaka 100 ipo siku lazima yapite Njia yake Original ndo kilichotokea Morogoro leo. Akuna cha serikali wala nini. Watanzania wengi awajiongezi kwenye mambo mengi. Aingii akilini na mapori yote yaliopo TZ mtu akajenge mabondeni au pale Jangwani
Wacha inyeshe tutajua panapovija,watatoka tuu wenyewe huko
 
Kuna hili eneo pia la barabara ya Dodoma maeneo ya kanisani kabla hujafika mazimbu road maji yamepita juu ya barabara. Inabidi serikali ibomoe barabara hiyo iinuliwe juu au kuweka makaravati mengi kupitisha maji. Wahandisi wanelewa zaidi.
Vipi maeneo ya Mkundi?
 
Kuna maeneo ya Mkundi Watu wamejenga kabisa kwenye Mkondo wa maji na wamejiami kwa kujenga kuta. Maji ata ikipita miaka 100 ipo siku lazima yapite Njia yake Original ndo kilichotokea Morogoro leo. Akuna cha serikali wala nini. Watanzania wengi awajiongezi kwenye mambo mengi. Aingii akilini na mapori yote yaliopo TZ mtu akajenge mabondeni au pale Jangwani
Wewe chipukizi wa Chama cha Mambuzi acha uongo. Hapa Kihonda tuta la mwendo kasi ndio chanzo cha hayo mafuriko kwani maji yanashindwa kupita kwenye njia yake ya asili hivyo yanarudi mitaani.
 
Back
Top Bottom