Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Mafuriko yanatokea pale maji yanapozidi uwezo wa eneo husika kuyashikilia. Hata miundombinu iwe bora vipi, yakizidi kipimo hakuna namna ya kuyazuia.
Tanzania hii Kuna miundombinu gani? No mipango Miji,watu wamejenga mabondeni tena sehemu zingine serikali imepima,Kuutupa taka hovyo,kulima kwenye mikondo ya maji,hakuna mifereji na upuuzi kama huo..

Acha inyeshe tujue inapovuja.
 
Mto msimbazi maji yake hutokea Kisarawe na maeneo jirani sio Morogoro. Maji ya Morogoro huingia mto Ruvu na kuelekea Bagamoyo na sio DAR
 
Usijichoshe ni hakuna,hapa Tanzania Kila kitu kinafanywa Kwa kubahatisha
 
Wacha inyeshe tutajua panapovija,watatoka tuu wenyewe huko
 
Kuna hili eneo pia la barabara ya Dodoma maeneo ya kanisani kabla hujafika mazimbu road maji yamepita juu ya barabara. Inabidi serikali ibomoe barabara hiyo iinuliwe juu au kuweka makaravati mengi kupitisha maji. Wahandisi wanelewa zaidi.
Vipi maeneo ya Mkundi?
 
Wewe chipukizi wa Chama cha Mambuzi acha uongo. Hapa Kihonda tuta la mwendo kasi ndio chanzo cha hayo mafuriko kwani maji yanashindwa kupita kwenye njia yake ya asili hivyo yanarudi mitaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…