Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Umesahau kosa la kupanga njama za kumteka mtu .
 
#HABARI Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba wanaotuhumiwa kumteka na kumtishia kwa Silaha Honey Noah (29) mkazi wa Masaki jijini Dar es salaam, ambaye walimteka akiwa ndani ya gari lake aina ya Rav 4 na kumshikilia kwa nguvu kwa kipindi cha siku nne wakidai kiasi cha Dola milioni 3.5 kwa baba yake.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro anasema kutokana na chunguzi za kisayansi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao mmoja wapo ni raia wa Canada mwenye asili ya Kisomali.

Aidha Kamanda Murilo anasema watuhumiwa wote siku ya Leo watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili za kumteka, kumtishia kwa silaha, kumshikilia kwa nguvu na kudai pesa kwa nguvu.
 
Penal code ilikuja na meli toka Uingereza.Hapa huwa tunafanya amendments za hapa na pale kama elimu ya Kubenea
 
jeshi letu limestaarabika sana. zamani walikuwa wakikamata majambazi kama hao, tunasikia tu wameshambuliwa wakijaribu kutoroka mikononi au wakati wa majibizano. of course utawala wa sheria ni muhimu kwasababu huko ndiko hata wasio na hatia walikuwa wanafutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…