Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Msomali mwenye uraia wa Canada. Wamezoea kuteka meli na kushikilia mateka wakdiai walipwe naona alitaka kuja kuapply hiyo formula hapa
Kweli ana asili ya kisomali.

Lakini msomali mwenye akili akishapata uraia wa Canada atakua kashafungukiwa sana kimaisha.

Sasa huyu sijui kimemkuta nini au tusubiri upande wa pili washilingi, aseme lengo la kufanya hivyo ni nini.
 
Kweli ana asili ya kisomali.

Lakini msomali mwenye akili akishapata uraia wa Canada atakua kashafungukiwa sana kimaisha.

Sasa huyu sijui kimemkuta nini au tusubiri upande wa pili washilingi, aseme lengo la kufanya hivyo ni nini.
Yah wengi wakienda canada wanatoboa sana.
Easy money, huenda walitazama movie. 3.5 milion dollars si mchezo
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa saba kwa tuhuma za kupanga njama, kumtishia kwa silaha, na baadaye kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashilia watuhumiwa saba kwa madai ya kupanga njama, kumtishia kwa silaha na kumteka mwanamke aaliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29), mkazi wa Masaki.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro leo Oktoba 30, 2023 amesema tukio la kumteka binti huyo lilitokea Oktoba 16, 2023.

“Tukio hili limetokea Oktoba 16, 2023 saa nne asubuhi wakati Hani Hussein akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Rav4, ghafla akiwa eneo la Msasani Village alisimamishwa na sehemu ya kundi la watuhumiwa hao na kuingia ndani ya gari, kumtishia kwa silaha, kumteka na kuelekea maeneo ya Mbezi Beach mtaa wa ujirani ambako walimshikilia kwa nguvu kwa siku nne huku wakidai fedha kwa vitisho kwa baba wa mtekwaji kuwa asipotoa kiasi cha Dola za Marekani 3.5 milioni mtoto wake angepoteza maisha.

"Baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji wa na Oktoba 19 tulifanikiwa kumuokoa na kuwakamata watekaji wote wakiwa na gari walilomteka, pamoja na silaha ilyotumika Pistol Glock 19 iliyotengenezwa Austria ikiwa na risasi 4," amesema Kamanda Muliro.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hassan AbusherNur (39) raia wa Canada mwenye asili ya Somalia na mkazi wa Msasani, Nathan Lungumisa (27), Fredick Chahonza (49), Assad Abdurasur (43), Fahad Mussa (32), Ilfan Saleh (41) na Nicolas Nilay (39).

Aidha ameeleza kuwa tayari upelelezi na watuhumiwa wote watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa hatua zaidi za kisheria.

MWANANCHI
Napendekeza kunyongwa hawa watu, wasituletee ugaidi hapa Tanzania.
 
Mara paaap

Mwendesha mashtaka hana nia ya kuendeles na kesi. Basi case closed

Waliotunga hiyo sheria na kumpa raia mmoja nwendesha mashtaja madaraka makubwa hivyo walikosea sana

Too much room for corruption
 
Daah. Jamaa wana kesi nzito.
Armed robbery 20 years without parole.
Car jacking 15-20 years without parole.
Kidnapping I dont know how many years.
Hapo pia wataongezewa na Attempted rape
Pia wataongezewa attempted murder
Wataongezewa bodily harm.

Duh. Hapa hawachomoki hawa maharamia.
Yani. Hivi kale kakitabu ka Penal code alikatunga nani! Kana adhabu kali kali kweli.
Armed Robbery hapo inaingiaje mkuu!
 
Kweli ana asili ya kisomali.

Lakini msomali mwenye akili akishapata uraia wa Canada atakua kashafungukiwa sana kimaisha.

Sasa huyu sijui kimemkuta nini au tusubiri upande wa pili washilingi, aseme lengo la kufanya hivyo ni nini.
Hapa kuna story nyuma ya pazia, huyu binti anatoka familia ipi? Hawa watekaji walimjuaje? Huyu raia wa canada alifikaje nchini?
 
Kweli watekaji wakamatwe tu ka machinga? Kusiwepo hata kurupushani za mmoja kuliwa ya kichwa?
 
Back
Top Bottom