Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa saba kwa tuhuma za kupanga njama, kumtishia kwa silaha, na baadaye kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashilia watuhumiwa saba kwa madai ya kupanga njama, kumtishia kwa silaha na kumteka mwanamke aaliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29), mkazi wa Masaki.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro leo Oktoba 30, 2023 amesema tukio la kumteka binti huyo lilitokea Oktoba 16, 2023.

“Tukio hili limetokea Oktoba 16, 2023 saa nne asubuhi wakati Hani Hussein akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Rav4, ghafla akiwa eneo la Msasani Village alisimamishwa na sehemu ya kundi la watuhumiwa hao na kuingia ndani ya gari, kumtishia kwa silaha, kumteka na kuelekea maeneo ya Mbezi Beach mtaa wa ujirani ambako walimshikilia kwa nguvu kwa siku nne huku wakidai fedha kwa vitisho kwa baba wa mtekwaji kuwa asipotoa kiasi cha Dola za Marekani 3.5 milioni mtoto wake angepoteza maisha.

"Baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji wa na Oktoba 19 tulifanikiwa kumuokoa na kuwakamata watekaji wote wakiwa na gari walilomteka, pamoja na silaha ilyotumika Pistol Glock 19 iliyotengenezwa Austria ikiwa na risasi 4," amesema Kamanda Muliro.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hassan AbusherNur (39) raia wa Canada mwenye asili ya Somalia na mkazi wa Msasani, Nathan Lungumisa (27), Fredick Chahonza (49), Assad Abdurasur (43), Fahad Mussa (32), Ilfan Saleh (41) na Nicolas Nilay (39).

Aidha ameeleza kuwa tayari upelelezi na watuhumiwa wote watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa hatua zaidi za kisheria.

MWANANCHI
Kwani hao jamaa hawamiliki silaha zingine mafichoni kisha wakaenda kuwaonesha polisi halafu wakachoropoka kutaka kutoroka ili risasi zitakazopigwa hewabi ziwapate kwa minajili ya kesi kuwa closed?

Polisi wanaijua sana hii tuition lakini kama wamejisahau vile
 
Halafu hadi leo watekaji wa Roma, Mo Dewji , Aliyemtishia Nape bastola,na waliopiga risasi Tundu Lissu wapo mtaani wanatesa tu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hili jeshi hili
 
Utekaji wowote haukosi sababu ???

Inawezekana kuna fedha baba wa mtoto huyo alikuwa anadaiwa
Kuna uwezekano ikawa mambo ya biashara pia

Ova
 
Daah. Jamaa wana kesi nzito.
Armed robbery 20 years without parole.
Car jacking 15-20 years without parole.
Kidnapping I dont know how many years.
Hapo pia wataongezewa na Attempted rape
Pia wataongezewa attempted murder
Wataongezewa bodily harm.

Duh. Hapa hawachomoki hawa maharamia.
Yani. Hivi kale kakitabu ka Penal code alikatunga nani! Kana adhabu kali kali kweli.
Eti wameandika barua kwa DPP kukiri kosa kwa nia ya plea bargain, watekaji wenyewe inaonekana ni wakishua, ngoja nione serikali chini ya DPP itaamua nini
 
Kwani hao jamaa hawamiliki silaha zingine mafichoni kisha wakaenda kuwaonesha polisi halafu wakachoropoka kutaka kutoroka ili risasi zitakazopigwa hewabi ziwapate kwa minajili ya kesi kuwa closed?

Polisi wanaijua sana hii tuition lakini kama wamejisahau vile
Inaonekana watekaji ni wakishua pia, washaomba plea bargain soon utawaona wapo mtaani
 
Inaonekana watekaji ni wakishua pia, washaomba plea bargain soon utawaona wapo mtaani
Hii imekaaje kwamb watapigwa faini au, ila walikuwa wazembe wamekamatwa ka kuku labda gari ina gps au mawasiliano yao na walitaka kutumiwaje
 
Polisi wamekosea sana!
.
Hao ilitakiwa wawahoji huko huko chimbo walikokutwa, baada ya mahojiano wanamchukua, bint wale jamaa wanakula vyuma vya kichwa kila mmoja kisha wanakuja mbele ya kamera wanasema tumeua majambazi yaliyomteka binti maana yalianza kuturushia risasi basi.

Habari ya upelelezi na mavi mengine yanayofanana na hayo ni kupoteza rasimali za taifa.
 
Back
Top Bottom