Watu 7 mbaroni tuhuma za kumteka mwanamke Dar wakitaka kupatiwa dola milioni 3.5 kutoka familia ya mhanga

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa saba kwa tuhuma za kupanga njama, kumtishia kwa silaha, na baadaye kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashilia watuhumiwa saba kwa madai ya kupanga njama, kumtishia kwa silaha na kumteka mwanamke aaliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29), mkazi wa Masaki.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro leo Oktoba 30, 2023 amesema tukio la kumteka binti huyo lilitokea Oktoba 16, 2023.

“Tukio hili limetokea Oktoba 16, 2023 saa nne asubuhi wakati Hani Hussein akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Rav4, ghafla akiwa eneo la Msasani Village alisimamishwa na sehemu ya kundi la watuhumiwa hao na kuingia ndani ya gari, kumtishia kwa silaha, kumteka na kuelekea maeneo ya Mbezi Beach mtaa wa ujirani ambako walimshikilia kwa nguvu kwa siku nne huku wakidai fedha kwa vitisho kwa baba wa mtekwaji kuwa asipotoa kiasi cha Dola za Marekani 3.5 milioni mtoto wake angepoteza maisha.

"Baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji wa na Oktoba 19 tulifanikiwa kumuokoa na kuwakamata watekaji wote wakiwa na gari walilomteka, pamoja na silaha ilyotumika Pistol Glock 19 iliyotengenezwa Austria ikiwa na risasi 4," amesema Kamanda Muliro.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hassan AbusherNur (39) raia wa Canada mwenye asili ya Somalia na mkazi wa Msasani, Nathan Lungumisa (27), Fredick Chahonza (49), Assad Abdurasur (43), Fahad Mussa (32), Ilfan Saleh (41) na Nicolas Nilay (39).

Aidha ameeleza kuwa tayari upelelezi na watuhumiwa wote watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa hatua zaidi za kisheria.

MWANANCHI
20231031_054347.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah. Jamaa wana kesi nzito.
Armed robbery 20 years without parole.
Car jacking 15-20 years without parole.
Kidnapping I dont know how many years.
Hapo pia wataongezewa na Attempted rape
Pia wataongezewa attempted murder
Wataongezewa bodily harm.

Duh. Hapa hawachomoki hawa maharamia.
Yani. Hivi kale kakitabu ka Penal code alikatunga nani! Kana adhabu kali kali kweli.
Ubaya sasa hapo tayari walikuwa na fikra zile wakizipata hizo pesa huyu ataenda huku, huyu atanunua hiki, huyu mtaa watamkoma mwisho wa siku kuozea jela maana baba wa binti anaonekana sio wa kitoto.
 
Naona yupo na Nicolaus wengine ni wa baba mdogo.

Hilo ndilo jeshi la polisi siyo lile tulilolizoea.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa saba kwa tuhuma za kupanga njama, kumtishia kwa silaha, na baadaye kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashilia watuhumiwa saba kwa madai ya kupanga njama, kumtishia kwa silaha na kumteka mwanamke aaliyefahamika kwa jina la Hani Hussein (29), mkazi wa Masaki.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro leo Oktoba 30, 2023 amesema tukio la kumteka binti huyo lilitokea Oktoba 16, 2023.

“Tukio hili limetokea Oktoba 16, 2023 saa nne asubuhi wakati Hani Hussein akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Rav4, ghafla akiwa eneo la Msasani Village alisimamishwa na sehemu ya kundi la watuhumiwa hao na kuingia ndani ya gari, kumtishia kwa silaha, kumteka na kuelekea maeneo ya Mbezi Beach mtaa wa ujirani ambako walimshikilia kwa nguvu kwa siku nne huku wakidai fedha kwa vitisho kwa baba wa mtekwaji kuwa asipotoa kiasi cha Dola za Marekani 3.5 milioni mtoto wake angepoteza maisha.

"Baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji wa na Oktoba 19 tulifanikiwa kumuokoa na kuwakamata watekaji wote wakiwa na gari walilomteka, pamoja na silaha ilyotumika Pistol Glock 19 iliyotengenezwa Austria ikiwa na risasi 4," amesema Kamanda Muliro.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hassan AbusherNur (39) raia wa Canada mwenye asili ya Somalia na mkazi wa Msasani, Nathan Lungumisa (27), Fredick Chahonza (49), Assad Abdurasur (43), Fahad Mussa (32), Ilfan Saleh (41) na Nicolas Nilay (39).

Aidha ameeleza kuwa tayari upelelezi na watuhumiwa wote watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa hatua zaidi za kisheria.

MWANANCHI

Matatizo ta kuangalia movie haya, Mnapiga simu kwa Mzazi kawaida kwa kutumia data na minara ya Tanzania. Lazima washikwe, jinga kabisa hizi. $3.5m sio mchezo, eneo lenyewe Mbezi beach, watasota ndani sana.
 
Daah. Jamaa wana kesi nzito.
Armed robbery 20 years without parole.
Car jacking 15-20 years without parole.
Kidnapping I dont know how many years.
Hapo pia wataongezewa na Attempted rape
Pia wataongezewa attempted murder
Wataongezewa bodily harm.

Duh. Hapa hawachomoki hawa maharamia.
Yani. Hivi kale kakitabu ka Penal code alikatunga nani! Kana adhabu kali kali kweli.

Punguza kuangalia ID extra
 
Kweli ana asili ya kisomali.

Lakini msomali mwenye akili akishapata uraia wa Canada atakua kashafungukiwa sana kimaisha.

Sasa huyu sijui kimemkuta nini au tusubiri upande wa pili washilingi, aseme lengo la kufanya hivyo ni nini.
Hata Ulaya wazungu wanateka watu na kisha wanadai pesa.
 
Huyu baba yake ni tajiri ndo mwenye lile Jengo la Baraka plaza lilipakana palm village pia Ana apartment nyingi tu mjini anamiliki machine za MRI&CT scan
 
Back
Top Bottom