Watu wanajihusisha na mambo yao; Ni wewe tu unawawazia

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Ukitaka kufahamu uhakika wa kichwa cha habari nilichoandika tafakari juu ya mtu anapokufa waliobaki huwa wanafanya nini? (Jiulize tu kwa dhati ya moyo wako na ujijibu). Jibu la swali hilo ndiyo uhakika wa maisha yalivyo.

Ni wewe tu umekaa unawawazia wao ila kwa hakika watu wana mawazo yao na huenda hawana mapango wowote na wewe. Watu wanakutumia kwa uhitaji wao rahisi na siyo kwa ajili yako " for inconvenience". Hayupo mtu mwingine kwa ajili yako isipokuwa wewe.

Hayupo anayeelewa maumivu unayoyapitia isipokuwa wewe, hayupo anaeifahamu gharama yako zaidi yako. Watu wanaangalia unawaongezea nini katika thamani yao na siyo thamani yako. Thamani yako siyo suala lao ila ni lako, wao wataiona wanapohitaji kuinua thamani zao na siyo kuinua yako.

Usipotenga muda wa kukaa na wewe watu watakaa na wewe. Watu hawakai na wewe kwa ajili yako ila wanakaa na wewe kwa ajili yao. Siyo vibaya na wala siyo kosa watu kuwa hivyo kwa sababu ndivyo uumbaji ulivyo.

Unaweza kuumia sana ndugu lakini ukweli ni kuwa watu ni walewale . Kumbuka maisha yapo katika mkao wa upekee na siyo ujumuifu, unayeishi katika Dunia hii ni wewe na siyo wao kwa sababu wao nao wanishi katika Dunia yao kimtazamo wao.

Watu wana mambo yao na wewe una yako, haujawahi kuona watu wakiwa na furaha halafu Kuna wengine ni kama hawapo kabisa katika eneo hilo la furaha?.Hatuishi kwa namna moja usujiumize kufikiri kila mtu anawaza kama wewe.

Kaa tulia, jiangalie wewe kwa kina. Ah..ah..ah...inauma sana pale unapogundua kuwa mtu unayemuwazia namna fulani anawaza vingine tofauti kabisa na unapogundua jambo kumbuka unakuwa umeshachelewa "delayed reality". Jipe nafasi kubwa Ili uweze kuwapa wengine nafasi, tatizo tunawahi kuwapa wengine nafasi kabla ya sisi kuwa na nafasi.
 
Back
Top Bottom