Watu watatu wafikishwa kortini wakikabiliwa na shitaka la kusafirisha Dawa Za Kulevya aina ya Heroine Kg 30

Watu watatu wafikishwa kortini wakikabiliwa na shitaka la kusafirisha Dawa Za Kulevya aina ya Heroine Kg 30

kuna mdau kasema street value ya kilo moja ya cocaine bongo ni usd 8500 sasa ukipiga mara 30 ni usd 255,000 ambayo ni milioni 591..siyo hela nyingi kwa wauza unga ma don so it is possible kuwa na mzigo huo ndani.kumbuka walikamatwa na kama usd 12,000 cash na millions kadhaa za kibongo hizo walikuwa wamepokea hela za mauzo ya rejareja mtaani
Ila hawa wamekamatwa na Heroin sio Coca
 
mrangi hao wajomba watatoka na hutaamini, ni watoto wa mtu hapa town sio rahisi kuwafunga ila jamaa anafanya biz kisenge sana. Keshawaharibia madogo ila enewei mfanyabiashara kapata hasara tu hapo
Mh ngumu mjomba kesi za madawa sahvi zimebadilika siajabu huyo mjomba sahv kawazimia sim

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hii kesi kuimaliza rahisi sana,hapo unayajenga na mpelelezi,uchunguzi uendelee hata miezi sita,badala ya kilo 30,unapoteza zote unaacha nusu kilo,unachanganya na ngano,Kwanza ni kosa lao kwanza,hapo Hakimu anapunguza miaka mnapigwa,miaka 15!ila kifungo Cha nje,
 
Bado maisha ya ujanja ujanja matamu halafu mafupi sasa yupo nyuma ya nondo ,hakuna kukaa kwenye balcony 1st floor kula upepo,hakuna kwenda shopping malls ,hakuna ac ya Range Rover ,hakuna bata kule ni kulala mchongoma.
Hao madogo tangu juzi nlipata code zao kudakwa sehemu yenyewe yenyewe walipookotwa nyuma ya mwanamboka sheli
Kwa akili zao sijui walijiamini vp kwenda pande zile...ila ushamba na mawenge tu
Acha wanyooshwe

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mkazi wa Mbezi Tangibovu Said Mbasha(24), na wenzake watatu, wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 30.

Wengine ni Joseph Dalidali(27) maarufu Kama Mbezi Tangibovu; Allu Murugwa( 24) mkazi wa Kijitonyama na Fatima Shomari(24).

Akiwasomea mashtaka yao, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakim Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya, alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao, Machi 3, 2021 katika eneo la Kijitonyama Wilaya Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 30.6, wakati wakijua ni kosa kisheria.

Pia, Dalidali na Shomari, wanadaiwa Machi 3, 2021 katika eneo la Kinondoni mtaa wa Kasaba , washtakiwa hao wanadiwa kukutwa na gramu 2.63 za bangi, wakati wakijua kufanya biashara hiyo ni kosa kisheria.

Upelelezi haujakamilika na Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 24, 2021 itakapotajwa.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

View attachment 1722917
View attachment 1722918
Nani yupo nyuma ya huo mzigo? Maana hao machalii lazima Kuna connect ambaye Ni Papa mkuu. Wamtaje. Wamezipataje kilo zote hizo? Kuna mtu hapo mwenye jina lake na pesa zake akamatwe Kama kweli Wana Nia ya kumaliza hilo suala.
 
Sisi sio producers wa hayo mambo hivyo haiwezi kuwa na bei ndogo kiasi hicho kuliko USA ambapo ni pua na mdomo.

Pia Tz hakunaga cocaine mzigo mkubwa hivyo maana watumiaji wa cocaine hawapo

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
Kwa tz street value ya midevu inacheza 2300000
Kwa kg sasa kwa ulaya huko sijajua
Kwa heroin lazima mzg uingie mwingi maana si unakuja kwa majahazi mpaka tani hapo sasa kuna watu wanakuwa na mizigo yao kuchkua
Yule kg 20 mwingine 50 mwingine 100 etc

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kuna dada mmja namjua alipigwa maisha
Alizimiaa mahakamani alafu hyo dada mjini alikuwa maarufu tu
Kesi sahv hzi hazijakaa poa bora mtu ukalime matikiti tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Afadhali kupiga mbanga nyingine, kuliko hizo mambo lakini watu hawaelewi na walivo wajinga watoto wa kino wanajiachia kama nchi yao ni kupost Hennessy iko juu ya swimming pool, wakati wenzao hua hawaachi alama ukiambiwa mwenyewe una sanda, hivi shamimu mwasha na Nsembo bado hukumu yao?
 
Mtu anafanya biashara kama hiyo anajimwaga mtaani kama vile anafanya biashara halali kweli hawa vijana wanaonekana bado wana ujinga na ushamba mwingi! Apo watatoka jela wakiwa pengine na miaka 50
Naomba unitumie picha ya huyo dada wa miaka 24, atapotoka akiwa na hiyo 50, hatokuwa na mizinga ya kutuma na kuyatolea. Askari magareza tunaufidigi pisi mya hiyo 😀😀
 
Mauritius kule nihatari ukikamatwa ni life sentence
Hakuna life sentence kwa madawa kule.

Mwaka 2009 kuna bondia wa Tanzania alikamatwa pale,

Alikula 15 net..nadhani kishatoka.

Tanzania ndy inchi pekee yenye mazingira tata ya hukumu za madawa.
 
Eti viduka uchwara! Sema nao wamezidi sana kukariri mambo, yaani kila muuza ngada utakuta anazugia kwenye kuuza nguo, simu au vigari kadhaa vya kuzugia, mbona huwa hawadeal maybe na viwanda vidogo vidogo au vitu vingine?
Viwanda vitawapaka grease..
hii biashara ya dawa za kulevya bado inaendelea?

mamlaka husika wanapaswa waamke, maaana inaonekana wauza madawa ya kulevya wamebuni mbinu nyingine.
miaka mitano iliyopita kulikuwa shwari kabisa lkn hivi sasa wameanza kuibuka tena.

tafadhali vunjeni mtandao wote wa wauza madawa, mtandao unafahamika, kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya tafadhali inaonekana kama mmepunguza moto.
hii biashara ya dawa za kulevya bado inaendelea?

mamlaka husika wanapaswa waamke, maaana inaonekana wauza madawa ya kulevya wamebuni mbinu nyingine.
miaka mitano iliyopita kulikuwa shwari kabisa lkn hivi sasa wameanza kuibuka tena.

tafadhali vunjeni mtandao wote wa wauza madawa, mtandao unafahamika, kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya tafadhali inaonekana kama mmepunguza moto.
Nani kakwambia kulikua shwari? nchi kama Tz haiwezi dhibiti biashara hii bali ni mbwembwe za kujisifu tu.
Imagine pamoja na sheria kali za china au arabuni na bado watu wana smuggle mizigo,sembuse nchi ya wala rushwa hii? think twice.
 
daladala nazo baadhi zipo kwenye hii biashara nawashtua tu watu wenye kudhibiti, wanapeana mizigo kimyakimya walivo vaa kama masikini lakini ni mbinu tu za kipigaji kama za waokota machupa mtaani, na wanafunzi wadogo wa primary na vyuo vya ....kumbe wanamizigo, mtu anachukua mzigo kama utani vile ningekua ... jana ninge kamata kiulaini tu watuhumiwa, #okoa vijana nguvu ya taifa madawa yanaua.
 
Back
Top Bottom