Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Wiliobale na RFA miaka hiyo, 2020 nikaja kukutana nae kagongwa-kahama ni dalali wa maroli ya mizigo
 
Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news', Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani.

Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km Clouds mfano kuna heri dereva babaji,shangwe dereva babaji, Daudi wakota n.k

Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa,kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu.

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka,yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni, fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni Kigoma.

Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya.

Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es Salaam.

Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi.Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana.

Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana.Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi, wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sn Enzi hizo

Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
Kuna jamaa alikuwa akitaka kutuma salamu clouds FM alikuwa akianza na neno Niambiiiiiiieee!!
 
Imakulaya -Mwananyamala kwa kopa sela sela nukta nukta.
John Zenze
Baba Dulla One Majani Mapana - M.A.P
Manase R. Muhaha Ng'hambako kutoka Lumumba DSM
Salumu Chumu

Kwasasa kuna Magufuli Jikono Jandama - RFA Huyu Kwenye kipindi cha Hakuna Kulala Na Faustine Stephano
Dah nilitaka nishangae mtoa mada kataja wote kasahau dullah one[emoji38][emoji38][emoji38]...
Bado mutala tala venture wa msasani..
Watu majina makubwa kuliko maisha yao[emoji23]
 
Mwingine enzi hizo nipo shule ya msingi namsikia "Kapama wa Kapama"kutoka kiloleni tabora.
 
Yupo kagongwa kahama ni dalali wa maroli nimeanza kumsikia tokanipo chali hadi nimekuwa mtu mzima mara ya kwanza naonana nae 2020 hadi saiv nina number yake
Alafu unakuta mtangazaji anataka Kwa kujaza hiyo KAGONGWA KAHAMA 😅😅
 
Imakulaya -Mwananyamala kwa kopa sela sela nukta nukta.
John Zenze
Baba Dulla One Majani Mapana - M.A.P
Manase R. Muhaha Ng'hambako kutoka Lumumba DSM
Salumu Chumu

Kwasasa kuna Magufuli Jikono Jandama - RFA Huyu Kwenye kipindi cha Hakuna Kulala Na Faustine Stephano
Wewe mkongwe sn mkuu
 
Baba mzazi baba eh baba naachia laini. Nampenda sana huyu jamaa ni burudani kumsikiliza.
Na kuna mmoja alikuwa anaitwa masumbuko shombe sijui kama unalikumbuka hilo jina
 
Back
Top Bottom