Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Namkumbuka Kuna jamaa alikuwa anaitwa" Dibro dibara double D ,D kubwa mbili zenye ujazo" alikuwa lazima atume salamu kituo cha redio Ebony Fm
 
Huyu wa kuning'inia kwenye Tawi la mchicha nimecheka sn asee[emoji28]..alafu siyo tu ananing'inia,bali pia bingwa wa kuning'inia' ahahaha

Time is fleeting!!


Maanake huwenda kuna wengine wakawa wanajaribu jaribu kuning'inia kwenye tawi la mchicha,sasa mwamba ndo alikuwa bingwa wa hayo makarateee😂😂😂😂😂😂
 
Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news' , Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani

Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km clouds mfano kuna heri dereva babaji,shangwe dereva babaji, Daudi wakota nk

Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa,kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka,yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni,fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni kigoma

Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya
Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es salaam

Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi.Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake
Bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana

Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana.Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi,wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sn Enzi hizo

Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
Kuna yule alikuwa Radio free wakuitwa mwili obareeee
 
Maanake huwenda kuna wengine wakawa wanajaribu jaribu kuning'inia kwenye tawi la mchicha,sasa mwamba ndo alikuwa bingwa wa hayo makarateee😂😂😂😂😂😂
Dah🤣🤣
 
Wapiiii jimmy shirikisho raisi wa mwenge,sharo ganstar,zibwalabwatah,mtoto wa vitoto,
Sharo gangster wa juzi huyu,wenzie kina shangwe dereva bajaji,king majuto, na daudi wakota kabla hajachukuliwa clouds media
 
Hapana, huyu alikuwa akianza kuitika inabidi na muziki uzimwe studio. Alipenda sana kupiga simu RFA ila siku moja nikamsikia Radio One. Naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam
Hiyo naam imezidi kwa urefu. Jamaa siku hizi simsikii kabisa
 
Kuna huyo mdada alikuwa anaitwa Manka Mushi alienda wapi? Sema huyo Baba Mzazi Baba kutoka Makongorosi Chunya nampenda Sana na Mungu amzidishie huwa anasaidia wenye uhitaji kupitia redioni.
Manka Mushi bado yupo sana anaendelea.
 
Lawena Msonda

Huyu jamaa kuna muda mpaka nikahisi ni watangazaji wenyewe wanajitekenya na kucheka
Baba mzazi baba eh baba naachia laini. Nampenda sana huyu jamaa ni burudani kumsikiliza.
 
Kuna huyo mdada alikuwa anaitwa Manka Mushi alienda wapi? Sema huyo Baba Mzazi Baba kutoka Makongorosi Chunya nampenda Sana na Mungu amzidishie huwa anasaidia wenye uhitaji kupitia redioni.

Huyu yupo pia radio maria,ila waanzilishi ni ni sisi mwaka 1996 enzi za Askofu Norbert Mtega
 
Back
Top Bottom