Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Nasikia wakatoliki ndio wametengeneza hiyo biblia unayo refer. Thibitisha mtumishi.
 
Ukizungumzia wafu,ukumbuke hata Yesu alikufa.Sasa sijui utakunywa mchuzi wa maharage pekee au utabugia na maharage kabisa?
 
Kuabudu masanamu inahitaji uvumilivu sana
Ni nani aliyekudanganya Wakatoliki wanaabudu sanamu?

Kwa nini muwawekee watu maneno mdomoni?

Hebu pandisheni mizuka na muongee maneno yenu ya uongouongo.Eti...kundaraa bashartaayaaa kurduuum...!

Uongo mtupu kujidai mnanena kwa lugha.😂😂😂😂
 
Hapo ndipo umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu unapoonekana.
Labda nikuulize swali.
Bikira Maria hakuna na watoto wengine wa kumlea Hadi akabidhiwe Yohana?

Angalizo.
Naomba hili swali lisijibiwe na Mkatoliki.
Naomba niongezee maneno baadhi kwnye swali lako ili ajibu vizuri zaidi..... '' bikra Maria hakuwa na watoto wengine mpk amkabidhi kwa Yohana ilihali pia mumewe Yusufu alikuwa bado yu hai? chapwa24
 
Walau nakushukuru Kwa kukiri kwamba Kanisa Katoliki ndilo alilolianzisha Yesu.
 
Sijaona kwenye hili andiko wanapokutaza kusali Rozari wala kumtumia Bikira Maria atuombee Kwa Mwanae.
Ninachokiona hapo ni Kuabudi miungu.
Yaani hairuhusiwi kukipa kiumbe chochote hadhi ya Mungu kama walivyofanya waisrael walipochonga Sanamu ya ndama na kusema ndio Mungu wao aliyewatoa utumwani misri.
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Unadharau makanisa ya mabati, hujui ibada unaweza fanya hata chini ya mti. Nani alikudanganya Mungu anapatikana kwenye makanisa ya maghorofa tu.
 
Siyadharau. Mungu anakuumba na akili timamu kabisa. Unaweza kujenga nyumba ya kuishi, unaweka fence, na kufuga mpaka mbwa kukulinda, lakini ibada unaona ukaifanye kwenye kanisa la mabati machakavu?

Watu mnapenda kufanya utani sana na imani.
Asante rafiki
 
Hapana mkuu ubatizo kwa Kiebrania maana yake ni kuzamisha. Sasa ukibatiza kwa kikombe maana yake hujazamisha mwili. Hata Yesu alizamishwa mwili katika maji na Yohane mbatizaji.
We anzisha uzi mwingine sio kudanganya watu hapa
Kwanza lugha ya hivo vitabu vilikuwa ni vya kiebrania au unakariri tu
 
Hata imani yako ni potofu according to imani zingine
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Je wewe kuna kanisa hata moja zuri ulilojenga ukakabidhi watu wakaanza kuabudu?
 
Kuwepo kwa sanamu katika nyumba za ibada kulianza hata kabla ya kuja kwa Yesu
Rejea waamuzi 17&18


Haya rejea tena[emoji116][emoji116][emoji116]

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)“

Ukipata mda tena rejea tena wakati sulemani alipokuwa akijenga hekalu mbona masanamu yalikuwepo 2Nyak 3&4

Na wakati wa kubariki hilo Hekalu, Mungu alilibariki likiwa na sanamu humo ndani
 
Watakwambia hiyo ilikuwa agano la kale.
Kwamba agano la kale Mungu alikuwa anakubali Sanamu ziabudiwe.
Ndio maana wakatoliki wanawapuuza na kuamua kukaa kimya.
 
Wasabato wao mafundisho yao makuu ni kumpinga papa na kumuita mnyawa wa chapa 666
 
Haya maneno tumeshaambiwa sana na walokole,wasabato lakini kwanini haya mantiki yoyote kwa wakatoliki?
Ni kwa sababu ya msingi imara wa imani uliojengwa kwenye mioyo yetu.
 
Ukizungumzia wafu,ukumbuke hata Yesu alikufa.Sasa sijui utakunywa mchuzi wa maharage pekee au utabugia na maharage kabisa?
Mkuu Yesu alikufa, akafufuka halafu akapaa mbinguni. Huyo Yesu alie katika wafu mpaka sasa siyo Yesu huyu tumzungumziaye Yesu Mnazareti
 
Walau nakushukuru Kwa kukiri kwamba Kanisa Katoliki ndilo alilolianzisha Yesu.
Hilo ni kweli na asiyekubali hilo ni kwamba tuu hajui. Ni kanisa la kwanza aliloliacha Yesu lakini lilipata mkengeuko
 
Waislamu siwezi kuwasemea lakini Wakristo wengine wanawashutumu Wakatoliki kwa sababu wanafundisha mambo ambayo ni unbiblical na mambo ambayo yalirithiwa kutoka katika desturi za Dini za Kipagani za Kirumi na Kiyunani
Mbona wao wakatolik hawawashutum hao wengn.. wako kimya tuu na wapole.. kwa akil ya kawaida unaona din ya kwel hapo ni ipi.. ile ya kusimanga wengne au?.. hahah.. ila pia akil.. wakatolik weng wana akil
 
Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu
Mungu sio maskini msimshushe Mungu wetu hata sehemu ya kumuabudu lazima iendane na utajiri wake
Mungu hana shida na utajiri wa mfuko wako, Mungu anachotazama haswa ni roho yako jinsi ilivyopondeka mbele zake.

Mahekalu makubwa na minara na nakshi za dhahabu siyo ishu saana kwake.

Unafikiri Nuhu alikua kwenye kanisa lenye mnara mkuubwa alipotoka kwenye gharika na akamfanyia Mungu ibada ya shukurani akatoa na sadaka? Building ni muhimu lakini siyo ishu saana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…