Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Hapo ndipo wakatoliki wanapowazidi,ina maana kama hao mitume hawajamtaja nyie binadam wa leo hamuwezi kuona kama alistahili heshima kwa kuwazalia mkombozi wenu?
hakustahili heshima yeyote special. Yesu alikuwepo hata kabla yake. endeneeni kumwabudu kama ana mbingu ya kuwapeleka.
 
Waislamu siwezi kuwasemea lakini Wakristo wengine wanawashutumu Wakatoliki kwa sababu wanafundisha mambo ambayo ni unbiblical na mambo ambayo yalirithiwa kutoka katika desturi za Dini za Kipagani za Kirumi na Kiyunani
Huenda umesimuliwa tu na elders wako kwa maslahi yao, lakini hujahudhuria wala kuona mafundisho ya Roman Catholic church, yaani The Church. Halafu kuna watu hawajui kuwa Biblia haikuandikwa immediately baada ya kila tukio, hawajui iliandikwa kutokana na mapokeo pia

Yohana 21:25
25 Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
 
Sawa umesimulia agano la Kale. Biblia yako haina agano jipya labda tuone kama Bikira Maria hajaandikwa?
 
Daaa asante mkuu umemaliza kila kitu ,nilitaka nimueleze hivyo hivyo. Barikiwa saana mkuu, taji yako inang'ara
 
Roho Mtakatifu hajawahi kushuhudia watu wafuate desturi hizo za kikatoliki za kina maria na watakatifu waliokufa. ni kweli kuna mambo mengi sana ambayo hata yasipoandikwa Roho Mtakatifu anaweza kukufafanulia kuwa hili ni dhambi na hili sio dhambi. Roho Mtakatifu anashuhudia kuwa kuabudu wafu na kureplace kuomba kwa Jina la Yesu na jina la maria na mitume ni dhambi na chukizo kwa Mungu.

waongozwao na Roho ndio wana wa Mungu. awaye yote asipokuwa na huyo Roho wa Kristo huyo sio wake. wakatoliki mmekataa wokovu, mkakataa Roho Mtakatifu, mmekubali kufuata desturi za dini na akili za kibinadamu ndio maana kila siku tunawashauri jaribuni hata mara moja tu kuokoka muone utofauti wake. mtakuja kutushukuru.
 
Comment ya kijinga sana hii unaweza kuthibitisha humu unabenefit nini na assets za kiroma?
Upo sahihi mkuu kuna uwezekano mimi ni mjinga.

Mkuu mimi nimezaliwa na wazazi wanaoabudu kanisa la Roma kwa hiyo kama ni kutumia assets za kiroma basi ndo zimenikuza na kunifikisha hapa nilipo.

Nimezaliwa katika hospital ya Huruma inamilikiwa na shirika la Roman Catholic la ma sister wa st Joseph Rombo.

Nimesoma shule ya st Ritaliza primary school Kilimanjaro.



Secondary nikasoma st Amedeus Kilema Kilimanjaro mpaka advance.



Chuo kikuu nikasoma The Catholic University of Health and Allied Sciences - Bugando (CUHAS-BUGANDO)

Kituo changu cha kazi ni Consolata Hospital Ikonda-Makete.

Mke wangu na yeye alilelewa kituo cha watoto yatima St.Francis Boma Hai.



Kanisa la Roma ni zaidi ya kusali. Ni sehemu ya maisha ya waumini wake.



Kanisa la Roma halina ule utaratibu wa maombi na kununua mafuta.ila ukiumwa utaelekezwa hospital. Na kanisa hili lina hospital za kisasa nchi nzima. Ni kanisa linalosimamia misingi ya sayansi kuliko unavyoweza kufikiria.



Kanisa la Roma pia linaamini sana katika elimu. Kanisa hili limeweza ku survive miaka yote hii kwa sababu ya kuwekeza katika elimu. Ndo maana inavyuo mbalimbali nchi nzima

SAUT, ST.JOHN DODOMA ETC.



Kanisa hili pia halipo nyuma katika financial institutions lina MKOMBOZI BANK.



Kanisa Catholic halikusimamii wewe kwenda mbinguni tu ila linahitaji pia kuhakikisha unapata mahitaji yako muhimu kwa ubora kabisa.

 
Heee,Yesu alikuwepo kabla ya mama yake?
Nitaendelea kuwa na Kanisa Takatifu la Roma kwa comment za aina hii.
huwa hamfundishwi hivyo? soma Yohana 1 yote utajua Yesu alikuwepo tangu enzi. alifanyika mwili tu (reincarnate) ili afanyike kafara la dhambi zangu mimi na wewe na wengine wote dunia nzima.
 
Wapo mapadri wengi tu wanaombea watu,tatizo lenu nyie so called religious fanatics mnajifanya kujimilikisha roho mtakatifu.
 
huwa hamfundishwi hivyo? soma Yohana 1 yote utajua Yesu alikuwepo tangu enzi. alifanyika mwili tu (reincarnate) ili afanyike kafara la dhambi zangu mimi na wewe na wengine wote dunia nzima.
Heeeeeeeeee
 
Wapo mapadri wengi tu wanaombea watu,tatizo lenu nyie so called religious fanatics mnajifanya kujimilikisha roho mtakatifu.
wanaombea kwa jina la nani kati ya Maria, watakatifu na Yesu Kristo? ni jina lipi limeonekana kuwa na nguvu ya kuponya kati ya hayo.hahahaha.
 
hakustahili heshima yeyote special. Yesu alikuwepo hata kabla yake. endeneeni kumwabudu kama ana mbingu ya kuwapeleka.
"Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa". Kama unaheshimu vitabu vitakatifu basi hiyo sentensi iko kwenye biblia ndugu.
 
"Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa". Kama unaheshimu vitabu vitakatifu basi hiyo sentensi iko kwenye biblia ndugu.
kwahiyo kama maria amebarikiwa, mimi naanzaje kuomba kupitia yeye wakati Yesu Kristo aliyenifia msalabani aliagiza tuombe sio kwa jina lingine ila kwa Jina la Yesu tu. kwani maria ana nguvu gani kunisaidia? alimwaga damu na yeye ili awe tofauti na mimi?
 
Heee,Yesu alikuwepo kabla ya mama yake?
Nitaendelea kuwa na Kanisa Takatifu la Roma kwa comment za aina hii.
Aaa mkuu sasa Yesu si ni Mungu, inamaanisha kua alikuwepo kabla ya mama Maria kuumbwa.
John 1:1-5
[1]In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[2]The same was in the beginning with God.
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
[3]All things were made by him; and without him was not any thing made that was made.
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
[4]In him was life; and the life was the light of men.
Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
[5]And the light shineth in darkness; and the darkness comprehended it not.
Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…