Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

CHEMA CHAJIUZA, KIBAYA CHJITANGAZA ....period!
 
Umesema ukweli mtupu Bro! Mimi mwenyewe kuna jamaa nilikutana nae kwenye bus la Tanga sasa akawa anankuliza maswali kuhusu Tanga nikawa namuelekeza nisijue jamaa anataka kuni tege kwenye biashara ya Forever wakati nipo likizo yangu ya Mwaka Dar jamaa akaning'ang'ania sana nihudhurie seminar ya ujasiriamali nikawa namzungusha maana niliuliza seminar ya nn haniambii inahusu nn sasa kuna siku nikaona ngoja niende labda natupa fursa niliyoletewa na Mungu nikaenda MILLENIUM TOWER Kwa kweli niliboreka sana sana saana sikutaka tu kumuonyesha ila niliapa sitarudi na akiendelea kuning'ang'aniza wallah namchana makavu watu tuna mambo mengi badala ya kukaa na kusikiliza nyimbo zao
 
niliwahi panda daladala kipindi flani na dada mmoja, alikua yuko vizuri sana.. kwa tafsiri ya msichana mzuri aisee alikua mzuri.. basi sina hili wala lile akaanza kunisalimia, na vicheko ata ishu haichekeshi sana anafurahia vibaya paka nikajiona comedian.. maswala, story kibao paka nikaona bora jam ya kwenda posta iendelee tu kuwepo tu.. tunakaribia posta akaniomba namba yangu... kutoka pale najiuliza mbona huyu dada yuko tofauti na wengine.. mawasiliano yakaanza ila mwisho wa siku ndo akaanza ishu izo, aliniudhi sana kwa kunionesha ananijali kumbe moyoni mwake ananiona kama "another deal to make".
ikifika mahali biashara inakosa utu, inakosa ubinadamu, inakosa aibu, inakufanya uone watu kama mizigo ya nyanya, inavuka mipaka.. hio sio biashara nzuri.
 
Habari za weekend.....

Wauzaji wa bidhaa za forever living, kwanza hongereni kwa kufanya hiyo biashara inayohitaji kipaji cha hali ya juu kuweza kuongea sana na kumshawishi mteja, ni kipaji kwakweli.

Back to topic, mmekua mnatumia mbinu za uongo na kulazimisha sana mteja ili mtangaze biashara aaagrrrr hii mbinu yenu Inakera sana,inaboa sana

Mfano 1: siku za karibuni nikialikwa mahali, nikaambiwa ni semina nauliza semina ya nini nikaambiwa semina tu nihudhurie napigiwa simu za kusisitiza nikaona isiwe tabu ngoja niende nikaahirisha vitu vya muhimu kwenda semina, kumbe ni kwenda nyumbani kwa mtu kuoneshwa bidhaa za forever, wtf? Kwanini umdanganye mtu? Can you imagine nilikua nafeel vipi wakati naoneshwa hizo bidhaa? Mxyu nilikua nimekasirika sana

Mfano 2: dada mmoja kwenye group la whatsapp alitoa mwaliko, jaman karibuni kwangu sehemu flani kuna shughuli, msosi na bia vipo mtakula mtakunywa mtasaza, tunauliza ni nini ubarikio, engagement au nini mchango vipi anakomaa nyie njooni tu eeeh walaji na wanywaji wakaenda eneo la tukio wamevaa suti kumbe ni kuoneshwa bidhaa za forever, Wiki nzima group kimya hakuna anaeongea kumbe watu wamenuna

Mfano 3: Wauzaji wa online, mtu anasema una mtaji wa laki njoo whatsapp tufanye biashara ukiuliza biashara gani unaambiwa njoo whatsapp, unaenda whatsapp anakutumia video la mb 100 kutangaza forever.

Hii ni mifano michache, hivii hamuoni mnakwaza watu? Hakuna mbinu nyingine za kutangaza bidhaa zenu bila uongo??? Au bila kudanganya hamuuzi? Mnakera sanaaaaa
Ni hayo tu
hawa jamaa wajinga kweli,nilipigiwa simu na mdada flani mshkaji wangu sana,eti kuna semina ppf house pale niskose kuhudhuria.duuh mchizi nikajitupia teh teh teh mida ya sa Nne kamili niko maeneo ya ppf house nampigia hyo dada akamtuma mtu aje anipokee looh naona jamaa ananipeleka kwenye kagofu flani ka gorofa moja kudadeki kuingia ndani hovyoo kumbe forever wakati nilijua naenda kupanda lift ppf house nika meet na ma CEO wa ukweli....... aaaagggggrrrrrrr
 
Tuambie kisa cha kuacha
Hakuna biashara ngumu kama hiyo, kwanza unatakiwa kuwa muongo yaani kusema mafanikio makubwa uliyonayo au aliyonayo mwingine ili umvutie kujiunga. Marafiki zangu wote walinikwepa, kila nikikutana nao wanajua nawapa stori za forever. Nikaona huu upuuzi tu, nikaamua kuachana nayo na sitaki hata kuisikia.
 
Haaaaa duh hongera sana kwa kuachana na uongo wa kujitakia
 
Hakuna biashara ngumu kama hiyo, kwanza unatakiwa kuwa muongo yaani kusema mafanikio makubwa uliyonayo au aliyonayo mwingine ili umvutie kujiunga. Marafiki zangu wote walinikwepa, kila nikikutana nao wanajua nawapa stori za forever. Nikaona huu upuuzi tu, nikaamua kuachana nayo na sitaki hata kuisikia.
Kuna mdada mmoja insta ndo ananipa sifa za iyo forever ni mzuri hatari ila mi nawaza tu jinsi ya kula tunda Lake
 
Hakuna biashara ngumu kama hiyo, kwanza unatakiwa kuwa muongo yaani kusema mafanikio makubwa uliyonayo au aliyonayo mwingine ili umvutie kujiunga. Marafiki zangu wote walinikwepa, kila nikikutana nao wanajua nawapa stori za forever. Nikaona huu upuuzi tu, nikaamua kuachana nayo na sitaki hata kuisikia.[/QUOTE
Lol
 
We acha tu, mtu unakuwa muongo mpaka kwa wazazi, Mara ukijiunga utapata gari, utajenga nyumba, utazawadiwa safari ya kwenda marekani kumuona Mkurugenzi wa kampuni, utapewa tiketi ya ndege kwenda south nk yaan uongo mtupu
Ulitoa kiingilio kujiunga
 
niliwahi panda daladala kipindi flani na dada mmoja, alikua yuko vizuri sana.. kwa tafsiri ya msichana mzuri aisee alikua mzuri.. basi sina hili wala lile akaanza kunisalimia, na vicheko ata ishu haichekeshi sana anafurahia vibaya paka nikajiona comedian.. maswala, story kibao paka nikaona bora jam ya kwenda posta iendelee tu kuwepo tu.. tunakaribia posta akaniomba namba yangu... kutoka pale najiuliza mbona huyu dada yuko tofauti na wengine.. mawasiliano yakaanza ila mwisho wa siku ndo akaanza ishu izo, aliniudhi sana kwa kunionesha ananijali kumbe moyoni mwake ananiona kama "another deal to make".
ikifika mahali biashara inakosa utu, inakosa ubinadamu, inakosa aibu, inakufanya uone watu kama mizigo ya nyanya, inavuka mipaka.. hio sio biashara nzuri.
Teh we ushajiandaa kivingine ye anakuja na habari za forever
 
hawa jamaa wajinga kweli,nilipigiwa simu na mdada flani mshkaji wangu sana,eti kuna semina ppf house pale niskose kuhudhuria.duuh mchizi nikajitupia teh teh teh mida ya sa Nne kamili niko maeneo ya ppf house nampigia hyo dada akamtuma mtu aje anipokee looh naona jamaa ananipeleka kwenye kagofu flani ka gorofa moja kudadeki kuingia ndani hovyoo kumbe forever wakati nilijua naenda kupanda lift ppf house nika meet na ma CEO wa ukweli....... aaaagggggrrrrrrr
Wanakera sana huu uongo uongo wao semina semina afu unaishia kuoneshwa makopo ya forever, hawaangalii hata aina ya wateja mtu wa kawaida sana unamwambia anunue chupa ya laki tatu forever living ovyo sana
 
Back
Top Bottom