Wavuta sigara tukutane hapa: unapenda sigara ipi, unapenda kuvutia mazingira yapi na una lipi la ziada ?

Zamani sigara zilikuwa zinavutwa na wazee wa kishua tu sahv hadi madogo wanavuta. SM ni sigara pendwa hasa ukiwa umelewa aisee ukipuliza unatoa moshi kama exost ya pikipik full burudani jamen
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16]
 
Upo kama mimi, nikiwepo home huwa naenda chimbo langu ni mwendo wa dakika 12 hivi, hako kachimbo kametulia sana kapo karibu na msitu, hakuna anaenijua wala jirani anapita huko.

Nikiwa mitaa ambayo najua hawapo ndugu ama marafiki ndio kidogo navuta hata dukani wanakouza ila kuwe na chumba cha kuvuta, nikiwa nje ya mkoa navuta kwa kujiachia
 
Hii kitu iliwai nipelesha ,nikaota moto chaga za kitanda
Umenikumbusha kitu wakati fulani kipindi cha ramadhani mefika DSM kwenye harakati za maisha nikafikia logde flani ipo manzese jirani na nefaland nilikuwa mechukua msosi wakawa wamenifungia ktk foili halafu wakatia ktk bahasha za karatasi...

Nikagonga diko kama kawaida napenda kuvuta nikiwa melala au mekaa metulia mwenyewe hivyo nikazima taa nikapanda bed nikasogeza dustbin ambayo nilishatupia ile bahasha ya karatasi nikawasha fegi mwisho nikatupa kipisi ktk dustbin nikavuta shuka nilale aiseee nikawa napata hewa nzito na harufu flani hivi nikawa najisemea moyoni hao ni waislamu wanachoma ubani nilipozidiwa nikaamua kufunua shuka nikawasha taa chumba kizima kimejaa moshi hewa nzito kumbe ile karatasi ilikuwa ikiungua bhana mewasha feni hamna afadhali nafungua madirisha hamna kitu nikafungua mlango moshi ukawa unatoka kama wa tanuru hahahaha mtu mmoja alikuwa anapita akaenda kumuambia muhudumu....


Dah nilifatwa kisoo soo ila Mungu mkubwa liliisha na kule chumbani sikuweza kuendelea kulala nikaenda kutulia nje kwanza nikichoma fegi siku hiyo nilitamani niachane nazo kbs lakn ile tabia ya kusema navuta Leo tu kesho naacha rasmi ikaniponza....
 
Niliwahi kuacha kipisi cha sigara niliyovuta kwenye shati la mfuko πŸ˜‚πŸ˜‚ aisee nlijifunza kwamba kipisi huwa kinanuka sana
 
Sitojaribu kamwe na sipendi ,mimi ninavyokijaki kinywa changu halafu nivute misigara kama mwehu ! hii haingii akilini kabisa .

Nawachukia sana wanaovuta hadharani na kuwapa kero wengine ,natamani niwapige shaba.
 
Kwa experience yangu! Kama umetoboa 25yrz bila kutumia vilevi means bhang, sigara na pombe usitumie kabisa wala usijaribu achana navyo vitakupotezea muda mwingi sana vitu hivi vinatabia ya kukuendesha kwanza kabla hujafikia kuviendesha, pia kuviendesha hivi vitu inategemeana na intelligent ya mtumiaji au kudra za mwenyenzi Mungu wengi ndio wanapoteleaga humu na kurecover inachukua mda
 
Nimeloa na manyunyu ya mvua nikavuta SM,kufika home mama ananiuliza kwangu unavuta?daah niliishiwa pozi.

Kwa Sasa najitegemea navutia chumbani sivuti ofisini,yaani kabla sijalala.

Huu mcharazo ninavyoucharaza nimeshika sigara.

Kinachovutia wavutaji wote ukimgongea mwenzio hakuulizi anakupa tu kiroho safi[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Kinachovutia wavutaji wote ukimgongea mwenzio hakuulizi anakupa tu kiroho safi
wavuta sigara tunapendana sana kwenye ishu za sigara,

binafsi sijawai kugongea lakini mtu akiniomba huwa navuta kama 60% namwachia iliyobaki
 
 
 

Attachments

  • 20221103_201256.jpg
    31.6 KB · Views: 10
wavuta sigara tunapendana sana kwenye ishu za sigara,

binafsi sijawai kugongea lakini mtu akiniomba huwa navuta kama 60% namwachia iliyobaki
Kuna siku ile tu nawasha sigara akalita jamaa kwenye gari lipo kwenye foleni akaigongea.
Halafu mataa yanaruhusu.
Nikamkazia.
Alianza kunitukana kinoma.
Hivi kwani lazima mtu akigongea umpe?

Nb:Nlishaacha kitambo
 
Mimi harufu ya sigara tu ni KERO kwangu,sijui wadada wenye mabwana wanaovuta sigara huwa inakuaje??halafu na joto la Dar ukutane na mvuta sigara aliyechapwa na jua,hiko kikwapa chake huwa hatari sana[emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…