Akihojiwa na
Sexless , mvuvi (jina kapuni) amesema "Sato na Sangara wana minofu mikubwa kutokana na maumbo yao. Mara nyingi wamekuwa wakioza wanaposafirishwa toka Mwanza mpk mikoa mingine kwa kuwagandisha na barafu".
"Lkn maji ya kuoshea maiti (chloroform) yakitumika samaki hao hufika popote bila kuharibika" aliongeza mvuvi huyo.
"Kabla ya matumizi ya chloroform Sangara/Sato walikuwa wakipata uvundo kwenye minofu na biashara yao kuwa mbaya" aliendelea kueleza mvuvi huyo wa Sangara/Sato.
Maoni yangu. Kilichofanywa na naibu waziri ni uhuni mkubwa. Anahatarisha afya za watanzania ili tu aendelee kulinda biashara ya samaki hao. Makamu wa rais ana taarifa nyingi na nyeti kuliko naibu waziri halafu kauli yake inazodolewa kizembe namna hii?
Endelea kula Sangara/Sato at your own risk.
Yule naibu Waziri, napenda kuheshimu utu wake, lakini majibu yale aliyoyatoa ni ya upuuzi mkubwa. Rais Samia anatakiwa kumfukuza mara moja, hastahili hata kujiuzulu.
Tuliopo Kanda ya Ziwa tunajua. Habari ya wavuvi kuvua kwa kutumia sumu na baruti, wavuvi kuhifadhi samaki kwa kutumia madawa ya kutunzia maiti, na baadhi ya wavuvi kununua barafu za kutoka kwenye majokofu ya kutunzia maiti, ni habari za kweli. Ndiyo maana, mathalani, mimi binafsi nina watu wangu ambao huwa wananiuzia samaki. Na kuna wakati narudi bila samaki, anakuambia kabisa kuwa hawa wa leo siyo wa kununua wewe. Akiniambia hivyo tu, naelewa: ama wamevuliwa kwa sumu au walivuliwa jana yake wakahifadhiwa kwa hayo madawa.
Wenye mashaka, nawahakikishia, kwa 100%, taarifa ya makamu wa Rais kuwa samaki wanahifadhiwa kwa kutumia madawa ya kutunzia maiti, ni ya kweli. Jambo ambalo hakuna uhakika, ni je, hayo madawa ndiyo yanayosababisha wagonjwa wa saratani, zaidi ya 60% watoke Kanda ya Ziwa.
WITO: KWA KUWA SERIKALI HAITAKI KUTIMIZA WAJIBU WAKE, MWANANCHI BINAFSI CHUKUA TAHADHARI KWAAJILI YA AFYA YAKO NA ZA WOTE WANAOKUHUSU.
Wala siyo samaki tu, hata kwenye nyama. Na siyo nyama na samaki tu, hata mahindi. Siku hizi kuna sumu kali kupindukia za kutoka China, zile za vidonge, ndiyo zinatumika kuhifadhia nafaka. Vidonge vile, vinarushwa ndani ya ghala, humo ndani kuwe na panya au mjusi au mdudu yeyote anakufa mara moja, anakauka kama jiwe. Siamini kama sumu zile ni salama kwa mtumiaji wa chakula.