Wavuvi: Hii habari ya Sangara/Sato kuhifadhiwa na chloroform ni ya kweli

Tusubiri timu ya wataalamu watakuja na jibu
 
Pia watafiti waangalie pia ni saratani gani i.e. katika sehemu gani ya mwili na kufuatilia vyanzo vya saratani katika sehemu hizo za mwili e.g. koo, njia ya hewa, tumbo, mapafu, shingo la kizazi, damu n.k. huweza kusabababishwa na vitu gani na je, visababishi hivyo vimeshamiri zaidi maeneo ya kanda ya ziwa hususan Mwanza?
 
Kwahili naweza kukubaliana na wewe..mana saratani haiji siku hiyo hiyo..hutokea baada ya exposure ya muda mrefu.

Kwasasa hii imebaki kuwa nadharia though sio 100%.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na ndio maana niliweka neno hapa. Badala ya kukamata mTanzania anayetoantaarifa walitakiwa kutafuta ukweli wa hili jambo lakini waliita mtu Mchochezi huyu Waziri husika anatakiwa ajipumzishe mwenyewe Kwa manufaa ya afya za waTanzania na dunia kote wanaokula samaki Hawa.
Viongozi Hawa ndio walenwalioko bungeni na kujifanya bunge kuwa ni dhaifu. Hawatufai hawatufai.!

Serikali ije na majibu kamilifu Baada ya huyu kujiachia mwenyewe.!
 
Kwaiyo naibu waziri anampinga makamu wa rais?

Ulega anatoa wapi kiburi?
 
Chloroform or trichloromethane is an organic compound with formula CHC13 and is a common organic solvent.
Mimi ni mvuvi huku hilo suala ni geni mno na siwezi katu kuamini uzushu huu, nina jua mambo mengi kadhaa za mbinu nyingi, ila haya c kweli kabisa.
 
Hiyo dawa uliyoitaja (chloroform) haihusiani na kuhifadhi maiti
Hawa watu wanashangaza mkuu, tangu lini chloroform ikahifadhi maiti.....chloroform haiwezi kuhifadhi hata maiti ya mjusi itakuwa kuhifadhi samaki, tatizo hadi laymen wanajikuta wataalamu...​
 
Ila na sisi Watanzani tumezidi ujinga, kama hao Samaki kwa siku za nyuma wamekuwa wanafika wakiwa wameanza kuvunda kwa nini hatukuhoji kinachofanyika sasa mpaka wafike wakiwa wazima na wabaki wazima kwa muda mrefu?.
Utamuuliza nani
 
Sinunui tena milele Sato au Sangara, nitanunua wakufugwa tu, sitakaa ninunue tena Samaki wa Ziwa Victoria, mara maji ya maiti mara Mercury.. Sitanunua tena samaki wa Ziwa Victoria, nimeogopa sana, Cancer ni kifo aisee
 
Yule naibu Waziri, napenda kuheshimu utu wake, lakini majibu yale aliyoyatoa ni ya upuuzi mkubwa. Rais Samia anatakiwa kumfukuza mara moja, hastahili hata kujiuzulu.

Tuliopo Kanda ya Ziwa tunajua. Habari ya wavuvi kuvua kwa kutumia sumu na baruti, wavuvi kuhifadhi samaki kwa kutumia madawa ya kutunzia maiti, na baadhi ya wavuvi kununua barafu za kutoka kwenye majokofu ya kutunzia maiti, ni habari za kweli. Ndiyo maana, mathalani, mimi binafsi nina watu wangu ambao huwa wananiuzia samaki. Na kuna wakati narudi bila samaki, anakuambia kabisa kuwa hawa wa leo siyo wa kununua wewe. Akiniambia hivyo tu, naelewa: ama wamevuliwa kwa sumu au walivuliwa jana yake wakahifadhiwa kwa hayo madawa.

Wenye mashaka, nawahakikishia, kwa 100%, taarifa ya makamu wa Rais kuwa samaki wanahifadhiwa kwa kutumia madawa ya kutunzia maiti, ni ya kweli. Jambo ambalo hakuna uhakika, ni je, hayo madawa ndiyo yanayosababisha wagonjwa wa saratani, zaidi ya 60% watoke Kanda ya Ziwa.

WITO: KWA KUWA SERIKALI HAITAKI KUTIMIZA WAJIBU WAKE, MWANANCHI BINAFSI CHUKUA TAHADHARI KWAAJILI YA AFYA YAKO NA ZA WOTE WANAOKUHUSU.

Wala siyo samaki tu, hata kwenye nyama. Na siyo nyama na samaki tu, hata mahindi. Siku hizi kuna sumu kali kupindukia za kutoka China, zile za vidonge, ndiyo zinatumika kuhifadhia nafaka. Vidonge vile, vinarushwa ndani ya ghala, humo ndani kuwe na panya au mjusi au mdudu yeyote anakufa mara moja, anakauka kama jiwe. Siamini kama sumu zile ni salama kwa mtumiaji wa chakula.
 
Unazungula, unajichanganya.

Umesema matumizi ya Chloroform madhara yake ni baada ya muda mrefu. Halafu unasema ilikuwa inatumika miaka ya 2000. Halafu eti kwa sababu siku hizi haitumiki, basi haiwezi kuwa sababu ya Kanda ya ziwa kuwa na cases nyingi za saratani.

Kama ilikuwa inatumika miaka 2000, na madhara yake ni baada ya muda mrefu, si ndiyo unathibitisha kuwa madhara ya matumizi ya madawa yaliyokuwa yakitumika hapo zamani, ndiyo yanaonekana sasa?
 
Nasikia hata Maharage hutiwa Paracetamol ili yaive haraka hii ndio Dar bhana 😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…