Wazazi, acheni kuwapotezea muda watoto wa kiume kuwafundisha kupika!

Wazazi, acheni kuwapotezea muda watoto wa kiume kuwafundisha kupika!

Kuna wazazi wanazingua Sana!

Wako bize na wanao wa kiume kuwafundisha kupika!
Mwanaume amepewa jukumu kubwa mno la kuitawala Dunia. Jukumu hili linamtaka mtoto wa kiume awe strong mentally and physically!

Mtoto wa kiume achukue muda mwingi kujengewa misingi ya uongozi, utawala, ubunifu na ujenzi wa maisha

Upishi ni advantage ktk maisha ya mtoto wa kike si wakiume
Mtoto wa kiume hatashindwa kupika ktk maisha ya baadae Kama akiamua kuwa mpishi! Kwa sababu upishi ni Sanaa ambayo imeanzishwa na mwanamume hapo kale! Ikumbukwe hakuna jambo hapa duniani, iwe Sanaa, sayansi, falsafa ama ufundi ambalo limeanzishwa na kuletwa na mwanamke!

Yote yanayoendelea duniani Ni Mali ya mwanamume, na mwanamke anashiriki kuyafanya Kama mshirika na msaidizi wa mwanamume!

Kuna mtu atasema hapa eti Ni dhana ya mfumo dume, khaa, Sasa ulitaka mfumo jike? Hii Dunia imeumbwa kwa mfumo dume shosti!
Wanawake wabuni sayansi, teknolojia, falsafa, ufundi, biashara Kisha waanze kudai usawa!

Mwanamke ana haki ya kudai UPENDO kutoka kwa mwanaume na si HAKI SAWA!
Kwetu tarime mtoto wa kiuume haruhusiwa kupita karibu na jiko lilipo
siku moja babu mzaa mama almanusura awchomee moto watoto wake wa kiume alipowakuta jikoni wako na mama yao
alifunga kamlango akawasha moto, bahati yao kamlango kalikuwa weak
 
Kwetu tarime mtoto wa kiuume haruhusiwa kupita karibu na jiko lilipo
siku moja babu mzaa mama almanusura awchomee moto watoto wake wa kiume alipowakuta jikoni wako na mama yao
alifunga kamlango akawasha moto, bahati yao kamlango kalikuwa weak
Ni kwa nini hamna hiyo ruhusa? Mna amini nini mwanaume akiingia jikoni???
 
Katika kitabu cha mithali kinasema hata mjinga akinyamaza uhesabiwa hekima.

Kwanza katika maisha ya kisasa hakuna jiko la kukalia kigoda ni majiko unapika ukiwa umesimama.

Kama ni mpenzi wa mpishi ya nazi siku hizi masoko yote wana mashine za sido za kukunia nazi unalipa sh 100 tu.

Humu comment za vijana kula kulala kuweka bundle kushinda mitandaoni utazijuwa tu.
Nakuona ndugu mpishi, unapambania upishi!
Mbunge ameshasema mume atatawala mwanamke kwa fedha sio upishi!
 
Wanaopika kwenye mahoteli ni akina nani?
Ile Ni kazi!
Wapo wanaume wengi wanafanya kazi mbalimbali ktk nyanja mbalimbali na hawakufundishwa utotoni
Kwani madereva barabarani walifundishwa utotoni?
Kwani hao wapishi hotelini wote walifundishwa utotoni?
Mwanaume yoyote hashindwi kupika pale atapoamua kupika, na si kupambana nae utotoni eti unamfundisha kupika
 
Humu kuna wachangiaji wengi ni kula kulala tena wengine wanaishi kwa shemeji zao hamna walijuwalo.

Kwa mfano mimi binafsi hawa tunaowaita wadada wa kazi wamenisumbuwa sana achilia mbali kuwabadirisha au anakuja huyu anakaa wiki anataka kuondoka kumbe ulitumioa tu kumleta mjini na saa nyingine unatuma nauli unaliwa vilevile, sasa nimeamuwa hivi.

Watoto wakubwa wako boarding, mtoto mdogo yupo day lakini anashinda shuleni anarudi jioni kabisa kwahiyo nyumbani tunapika usiku tu au nanunuwa take away hakuna kupika.

Sihitaji wala sifikilii kuleta house girl, usafi ni mara moja kwa wiki anakuja dada anafuwa anaosha vyombo anapiga deki nyumba namlipa cash yake anatambaa, siku za kawaida kufagia nyumba hakunishindi nafagia mimi au wife yeyote atakayehisi kuna michanga ndani.

Kwahiyo kwangu wala hatuhitaji mpishi na wakubwa wakirudi likizo wanapika wenyewe mchana au mama yao kabla ya kwenda job akiamka mapema awapikie ubwabwa full suti, binafsi kama nakuwa home vyakula vyangu ni michemsho tu wala havina mambo mengi ni nyama au samaki viazi ndizi na viungo unachanganya pamoja unakadiria maji, unaweka chumvi unatia na mafuta machache unawasha gesi ngoma inajipika yenyewe, hivi hapo shida iko wapi? Ukiona mimi nanunuwa chips ujuwe ni dharura tena ni usiku inanibidu tu.
Hayo yote ulifundishwa utotoni bro?
 
Mimi nadhani imefika mda watoto wa kiume waanze kufundishwa na tactics za uchakataji,,,sio unakuta toto la kiume ziiiito kwenye mademu mwishowe yanakuwa mapunga
 
Kwetu tarime mtoto wa kiuume haruhusiwa kupita karibu na jiko lilipo
siku moja babu mzaa mama almanusura awchomee moto watoto wake wa kiume alipowakuta jikoni wako na mama yao
alifunga kamlango akawasha moto, bahati yao kamlango kalikuwa weak
Unaongelea sehemu ambazo ni uncivilized siwezi kulishangaa hilo.

Ukienda kule ziwani upande wa Rolya mpaka leo jamii kubwa haijuwi umuhimu wa vyoo wanakwenda kunya ziwani tena wakiwemo na wasichana wazuri kabisa.

Kuna jamii kwanza huwezi kuamini kama hawa ni Watanzania yani kijiji kizima hakuna mwenye choo sasa hao watu si wanahitaji elimu kubwa zaidi ya hii?

Halafu kichekesho kuna msomi mkubwa sana yupo wall street John Mashaka anatokea huko.😄😄
 
Watu wanakupinga sana, lakin huo ndo ukweli waswahili huo hatupend ukweli unafiki umetutawala hii ndio sababu ya maendeleo duni. Unamfundisha mtoto wa kiume kupika ili iweje, agundue nn, atajua akikua. Tukiacha unafiki tutaendelea
 
Umenikumbusha Mbali kipindi kile mama ananiforce nipike halafu Mimi peke yang ndio Nilikuwa mtoto WA kiume kwenye family lakini bado walikuwa wanataka eti na mimi nioshe vyombo na kupika isitoshe wenyewe walikuwa zaidi ya wanne ila baada ya father kugundua akapiga marufuku na tangia kipindi hicho kazi zilikuwa kazi nzito kama kuchimba mashimo ya taka,kubeba vitu vizito, kujenga mabanda na cha zaidi kizuri zaidi ninachacho mshukuru father nikaanza na kupiga tizi na kuanza kucheza mpira maana kabla ya hapo Nilikuwa mtu wa kupika na kufanya vikazi vidogodogo baada hapo naenda kukaa kwenye mkeka na mama au kuangalia tamthiliya kiukweli mpaka nafika umri miaka 16 nilikuwa sijui ata kuendesha baiskeli wala kucheza mpira😂😂😂 Nilikuwa aina ya wanaume nyororo

Ila baada ya father kutia mguu nilibadilika sana japo mara kwanza niliona kama ananitesa maana alikuwa na tabia ya kuniamsha saa kumi na kunishwesha maji lita moja na baada hapo mchakamchaka unaanza 😂😂basi mwenyewe Nilikuwa naona kama mateso ila sasa nimekuwa nimeanza kuelewa

Na sasa na mimi nafata legacy alionichia baba yangu yani mfumo dume 😁😁yani Mimi nikiwa kwenye mahusiano demu kazi yangu nikutoa hela nasihitaji kusaidiwa kwenye kutoa matumizi yani kwenye financial Cases nahusika kwa asilimia 100 maana najua kwenye hivyo vikazi vyao sitahusika kwa asilimia 100
 
Safi sana. Kuna watu hawapa wanaona kujifunza kupika ni kama itawaondolea uanaume wao kitu ambacho naona si kweli. Nawaza kijana wa kiume leo hii akianza kujitegemea na hajui kupika ina mana atakua anakula migahawan siku zote? Anyways tunaambiwa kila mtu na chaguo lake.
Njaa ikimshika atajua kupika hapohapo automatically.
Na sio kupoteza muda wa utoto wake kumfundisha jinsi ya kushika mwiko.
 
Swali ni kama kupika sio kitu cha kushangaza kwa mwanaume.
Then ni kwanini wapishi wa utotoni mnahangaika kujitetea kwa nguvu?

Mna mashaka na maamuzi ya wazazi wenu na mko insecure?
Bila shaka ni hivyo hivyo.
 
Njaa ikimshika atajua kupika hapohapo automatically.
Na sio kupoteza muda wa utoto wake kumfundisha jinsi ya kushika mwiko.
Mie mwanangu nitamfundisha, tuna malezi tofauti kila mtu afanye analoona ni sahihi kwake.
 
Mimi nadhani imefika mda watoto wa kiume waanze kufundishwa na tactics za uchakataji,,,sio unakuta toto la kiume ziiiito kwenye mademu mwishowe yanakuwa mapunga
[emoji23][emoji23]
 
Soma vizuri andiko!
Hoja si kwamba mwanamume hahitaji kujua kupika,
Nimeandika kupika Ni kazi ndogo kwa mwanamume anayeamua kupika, na haihitaji tuition ya utotoni
Wanaume wako simpo katika suala la kupika
Akitaka kupika chochote anaweza hata kupiga simu akapewa maelezo mafupi na akapika akala maisha yakaendelea!
Ni ungese kuwa strict kwa mtoto wa kiume kumfundisha kupika, wakati yapo mengi anahitaji afundishwe utotoni
Naunga mkono hoja,mi binafsi siku kupika sana utotoni zaidi ya chai na uji,lkn nilipojitegemea angali bachela nilijifunza kupika,hivyo sio inshu Sana mzazi kitumia nguvu kimfundisha me kupika
 
Ni kwa nini hamna hiyo ruhusa? Mna amini nini mwanaume akiingia jikoni???
Yani mvulana/mwanaume anapoteza muda kwa kuchambua mchele na vitunguu saumu?Mwanaume akisikia njaa anachemsha maji anakunywa.Kupika atawakuta wamepika mbele mbele yao.
 
Yani mvulana/mwanaume anapoteza muda kwa kuchambua mchele na vitunguu saumu?Mwanaume akisikia njaa anachemsha maji anakunywa.Kupika atawakuta wamepika mbele mbele yao.
Mie kwetu wanaume wanapika. Kila mtu na malezi yake.
 
Back
Top Bottom