Wazazi na ndugu wa mke wangu wananikosesha raha

Wazazi na ndugu wa mke wangu wananikosesha raha

Sina mpango wa kula kulima kwenye maisha yangu ila siku ambayo ndugu wataanza kujazana nyumbani....

Ndio siku ambayo nitaanza kununua mashamba...

Watalima wakiona wamechoka waamshe kwao.
 
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119] kweli bongo nyoso... Kwamba mzee ulikua unabeep kwa mama mkwe ukakuta imejipiga jumlajumla..
 
Wakuu mimi ni mkazi na mzaliwa wa Dar es Salaam maeneo ya Tegeta, tatizo langu kuu mpaka nimekuja kuomba ushauri ni mke wangu kawakusanya ndugu zake na wazazi wake toka kijijini huko Mpwapwa. Yani imekua kero mi mwenyewe ndio natafuta maisha lakini nyumbani tupo jumla watu tisa pamoja na wazazi wake, nyumba yenyewe nimepanga nyumba viwili na sebule.

Sina raha hata kujiachia na mke wangu siwezi, mwezi wa nne huu hata mzigo sijala maana asubuhi nimeenda kazini, nikirudi jioni watu wamejaa na usiku wanalala sebuleni wengine chumbani.

Nimevurugwa kijana mwenzenu pesa yote ninayopata ambayo tungenunua hata kiwanja inaishia kwenye chakula na wanakula mno. Mke wangu nimejaribu kumwambia awambie ndugu zake na wazazi warudi kijijini lakini hataki eti anatamani awe nao karibu ili akibahatika kupata mtoto wamsaidie kulea.

Ndugu zangu naomba ushauri nifanye nini, nikimbie nyumba au niwafukuze mimi mwenyewe.

Rafiki yangu mmoja alinishauri labda nimtongoze mama mkwe lengo achukie aondoke na mmewe lakini cha ajabu amekubali 😥😥😥😥

MNISHAURI SANA🙏🙏🙏🙏NASOMA COMMENTS ZOTE.
Fanya yafuatayo au mojawapo..

1. Shirikisha ndugu wengine WA MKE kwa kuwaeleza namna unavyoshindwa kukamilisha majukumu yako kwa sababu ya uwepo wao na uwaombe wao wakusaidie kuwaondoa.

2. Shirikisha wahudumu wa unakosali kutegemeana na imani yako.. Kama ni mkristo shirikisha mapadre, wachungaji etc au kama ni muislamu shirikisha mashehe na uwaombe wao wawaite na kuomngea nao ili wasepe.

3. Tafuta mzee mmoja au zaidi wanaomuheshimu toka kijijini kwao, nao washirikishe jambo hili huku ukiwaeleza ukweli halisi. Na kwamba kwa sasa unajenga uwezo.. Wakuache ili ujenge uwezo, hivyo waondoke.

4. Katika kuyatekeleza hayo niliyoyasema hapo juu, Anza kwanza kuwaona watu hao ukiwa wewe na mkeo. Unajuwa, tatizo hapo ni kwamba WEWE NA MKEO HAMPO PAMOJA KWENYE JAMBO ZIMA. WEWE UNATAKA WASEPE YEYE ANATAKA WAWEPO. Mwambie mkeo pindi akipata mtoto, anayemuhitaji kuja kumsadia kulea basi aje wakati huo ukifika.

YAKISHINDIKANA HAYO YOTE HAPO JUU

MWAMBIE MKEO UNASEPA MBALI UTARUDI PALE NDUGU ZAKE WATAKAPOKUWA WAMEONDOKA.. Kama ni mfanyakazi sehemu, we danganya unakwenda mbali ambako utaweza kwenda kazini kama kawaida. Ukiwa huko mafichoni usihudumie chochote, na hela unayoipata anza mambo ya ujenzi..

BY THE WAY, KWA LOLOTE UTALOAMUA KULIFANYA HAPO JUU, JIANDAE KISAIKOLOJIA KUTEMANA NA MKEO
 
Kwan hamkushauriana kabla hajawaleta? Je haelewi kua kipato chenu hakitakidhi mahitajo ya hapo nyumbani kama mkiwa wengi? Je hawazi future yenu miaka 5 au 10 ijayo? Suala la akipata mtoto kua atasaidiwa na nani si asubiri mpaka ajifungue? Kaka hapo una majukumu makubwa kubadili akili ya mkeo na mawazo yake juu ya malengo yenu ya hapo baadae
 
Nimecheka kwa sauti kubwa kuona lakini cha ajabu amekubali 😥😥

Fanya juu chini ukiwa kama Mwaume uweze kutatua hiyo changamoto, kila lakheri.
 
Baba mkwe kilaza,mama mkwe kilaza,mke kilaza na inawezekana hiyo familia ya mkeo wengi ni vilaza hawawezi kufikiria wala kujiongeza alaf hawana aibu kabisa.
 
Ukiwa na akili hiyo huwezi toboa maisha walah, yaani changamoto ndogo namna hiyo unakuja kulia lia jf? Wangekuwa ni wazazi wako ungelalamika kiivo? Yaani umenichefua sana. Be a real man
Rubbish unaisi wazazi wake wangekaa apo kwenye mazingira kama hayoo mzazi haumwii wanakuja kukaa chumba kimoja unaakili kweli ingekuwa Mimi wangeona ingekuwaje huu ujinga ukiulea ndyo wanakupanda kichwani
 
Ukiwa na akili hiyo huwezi toboa maisha walah, yaani changamoto ndogo namna hiyo unakuja kulia lia jf? Wangekuwa ni wazazi wako ungelalamika kiivo? Yaani umenichefua sana. Be a real man
 
Atakuwa mrangi...wale watu kama wadudu vile

Hata akihamia mmoja mtaani, basi watakuja na wengine na wengine na wengine tena...hadi jina la mtaa watabadilisha litaitwa mtaa wa warangi!
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ukiwa na akili hiyo huwezi toboa maisha walah, yaani changamoto ndogo namna hiyo unakuja kulia lia jf? Wangekuwa ni wazazi wako ungelalamika kiivo? Yaani umenichefua sana. Be a real man
Comment hii inaonekana imetolewa na jinsia ya kike.
 
Back
Top Bottom