Wakuu mimi ni mkazi na mzaliwa wa Dar es Salaam maeneo ya Tegeta, tatizo langu kuu mpaka nimekuja kuomba ushauri ni mke wangu kawakusanya ndugu zake na wazazi wake toka kijijini huko Mpwapwa. Yani imekua kero mi mwenyewe ndio natafuta maisha lakini nyumbani tupo jumla watu tisa pamoja na wazazi wake, nyumba yenyewe nimepanga nyumba viwili na sebule.
Sina raha hata kujiachia na mke wangu siwezi, mwezi wa nne huu hata mzigo sijala maana asubuhi nimeenda kazini, nikirudi jioni watu wamejaa na usiku wanalala sebuleni wengine chumbani.
Nimevurugwa kijana mwenzenu pesa yote ninayopata ambayo tungenunua hata kiwanja inaishia kwenye chakula na wanakula mno. Mke wangu nimejaribu kumwambia awambie ndugu zake na wazazi warudi kijijini lakini hataki eti anatamani awe nao karibu ili akibahatika kupata mtoto wamsaidie kulea.
Ndugu zangu naomba ushauri nifanye nini, nikimbie nyumba au niwafukuze mimi mwenyewe.
Rafiki yangu mmoja alinishauri labda nimtongoze mama mkwe lengo achukie aondoke na mmewe lakini cha ajabu amekubali π₯π₯π₯π₯
MNISHAURI SANAππππNASOMA COMMENTS ZOTE.
Fanya yafuatayo au mojawapo..
1. Shirikisha ndugu wengine WA MKE kwa kuwaeleza namna unavyoshindwa kukamilisha majukumu yako kwa sababu ya uwepo wao na uwaombe wao wakusaidie kuwaondoa.
2. Shirikisha wahudumu wa unakosali kutegemeana na imani yako.. Kama ni mkristo shirikisha mapadre, wachungaji etc au kama ni muislamu shirikisha mashehe na uwaombe wao wawaite na kuomngea nao ili wasepe.
3. Tafuta mzee mmoja au zaidi wanaomuheshimu toka kijijini kwao, nao washirikishe jambo hili huku ukiwaeleza ukweli halisi. Na kwamba kwa sasa unajenga uwezo.. Wakuache ili ujenge uwezo, hivyo waondoke.
4. Katika kuyatekeleza hayo niliyoyasema hapo juu, Anza kwanza kuwaona watu hao ukiwa wewe na mkeo. Unajuwa, tatizo hapo ni kwamba
WEWE NA MKEO HAMPO PAMOJA KWENYE JAMBO ZIMA. WEWE UNATAKA WASEPE YEYE ANATAKA WAWEPO. Mwambie mkeo pindi akipata mtoto, anayemuhitaji kuja kumsadia kulea basi aje wakati huo ukifika.
YAKISHINDIKANA HAYO YOTE HAPO JUU
MWAMBIE MKEO UNASEPA MBALI UTARUDI PALE NDUGU ZAKE WATAKAPOKUWA WAMEONDOKA.. Kama ni mfanyakazi sehemu, we danganya unakwenda mbali ambako utaweza kwenda kazini kama kawaida. Ukiwa huko mafichoni usihudumie chochote, na hela unayoipata anza mambo ya ujenzi..
BY THE WAY, KWA LOLOTE UTALOAMUA KULIFANYA HAPO JUU, JIANDAE KISAIKOLOJIA KUTEMANA NA MKEO