Wazazi wa mtoto huyu watakesha wanabubujikwa machozi ya furaha na kumuombea maisha marefu Rais Samia

Wazazi wa mtoto huyu watakesha wanabubujikwa machozi ya furaha na kumuombea maisha marefu Rais Samia

Viongozi wa nchi hii wanadhulumu Watanzania kwa ufisadi wa hali ya juu na kushindwa kutoa huduma za msingi halafu wanamega vihela kidogo kumhudumia mtu mmoja au wawili kisha wanajifanya wana utu na wanataka watu wawaabudu na kuwaimba kwamba ni watu wema kumbe kiuhalisia ni chui waliojivika ngozi ya kondoo! Watu wabaya sana.
 
Na wewe toa pesa yako usaidie hata mmoja.
 
Na wazazi wa watoto Nchi nzima waliofutiwa bima ya AFYA na Samia huyo huyo wao watakuwa wanalaani Kweli Kweli.
 
Sasa amepewa ujumbe murua kabisa na watanzania kuwa wao siyo wajinga na hawatapeliki kijinga. Kama anataka gari la kifahari na anasa aende akanunue kwa pesa zake Mwenyewe.
Una roho ya kishetani sana wewe jamaa, ila ujue hujafa hujaumbika.
 
Na wazazi wa watoto Nchi nzima waliofutiwa bima ya AFYA na Samia huyo huyo wao watakuwa wanalaani Kweli Kweli.
Nenda kakate bima kwa ajili ya familia yako na watoto wako kwa gharama nafuu kabisa iliyowekwa na serikali yetu Sikivu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kila nikikaa nikawaza na kufikiria makubwa na mazito anayoyafanya Rais Samia katika Taifa letu kugusa maisha ya watanzania.Nabakia kusema Mama yetu Mpendwa na Rais wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Alizaliwa katika ardhi ya Tanzania kuja kuwafuta watu machozi na kuwarejeshea tabasamu katika mioyo yao.

Mama yetu Daktari Samia ni Mama Mwenye huruma isiyoelezeka wala kupimika katika mzani.Ni mama mwenye moyo wa upendo wa hali ya juu sana,ni Mama mwenye utu na kuguswa na matatizo ya watu.ni Mtumishi wa kweli wa watu ,ni Mama ambaye moyo wake na Maisha yake amejitolea kwa ajili ya kuwatumikia watanzania kwa moyo wake wote.

Embu fikiria ndugu yangu mtanzania, Unafikiri wazazi wa Mtoto huyu ambaye Mama yetu na Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia ameahidi kumhudumia na kumsaidia kupata mguu wa bandia . unafikiri wazazi wa Mtoto huyu wana furaha kiasi gani mioyoni Mwao? Unafikiri ni vipi wanaweza sahau upendo na huruma ya Rais Samia kwa mtoto wao? Ni vipi watalala na wakapata usingizi bila kumuombea maisha marefu Rais Samia?

Unafikiri Mtoto huyu na Mwanafunzi huyu aliyegusa hisia za watu atamsahau vipi Rais Samia? Unafikiri ni furaha kiasi gani atakayokuwa nayo mtoto huyu pindi atakapopatiwa Mguu wa Bandia? Unafikiri anaweza vipi kulisahau jina la Rais Samia moyoni Mwake katika uhai wake wote hapa Duniani ? Unafikiri atawasimulia nini watoto wenzake mpaka wajukuu zake panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu?

Ndugu zangu Watanzania unaweza kuwa na chuki binafsi na Rais Samia .lakini ukweli ni Kuwa Rais Samia ni mtu na nusu,ni kiongozi ambaye tunapaswa kumuombea Maisha marefu na kumuunga mkono kuendelea kutuongoza Watanzania. Ni kiongozi ambaye wapo watu watakuja waje wamkumbuke sana na kumlilia sana kwa mazuri aliyo watetendea atakapomaliza muda wake wa Urais hapo 2030 panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

View attachment 3045822

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Bila kumsahau yule mama.

Pili Rais ametoa wito Kwa jamii kuwa na bima ya Afya vinginevyo majanga kama hayo yakiwakuta wasije laumu Rais.

View: https://www.instagram.com/p/C9kPcA-qCbS/?igsh=MWQ1OHV6c3FmeW51dA==
 
Katika vitu/mazingira ambayo kiongozi wa nchi hapaswi kufanya au anapaswa kufanya zaidi hasa akiwa kwenye ziara rasmi ni KUONESHA UPENDELEO WA WAZI!

Ingekuwa ni ishu binafsi ningepongeza. Lakini kwenye hili Rais SSH alipaswa afanye kisera zaidi!

Hapo kasaidia tu mtoto mmoja... Je wapo wangapi kama huyo mtoto?
Je, nao watoke kokote walipo waende kwenye mikutano ya SSH kusuburia?
bahati zao?
Kwani anashindwa nini kutoa maelekezo ya kisera huyo akasaidiwa na wengine kote nchini nao wakatafutwa na kusaidiwa?

Urais siyo NGO ya kufurahisha wachache!
 
Nenda kakate bima kwa ajili ya familia yako na watoto wako kwa gharama nafuu kabisa iliyowekwa na serikali yetu Sikivu.
Kabla ya Samia kuingia, watoto chini ya umri wa miaka 5, walipata bima Bure.

Samia amefuta,

Halafu wewe chawa unakuja kutapika hapa!!
 
Kabla ya Samia kuingia, watoto chini ya umri wa miaka 5, walipata bima Bure.

Samia amefuta,

Halafu wewe chawa unakuja kutapika hapa!!
Alafu anakuja kufanya showoff kwa kusaidia mtoto mmoja mwenye mahitaji maalumu wakati wapo wengi wenye mahitaji hayo hayo hawajui hatma yao!
Shame!
 
Katika vitu ambavyo kiongozi wa nchi hapaswi kufanya hasa akiwa kwenye ziara rasmi ni KUONESHA UPENDELEO WA WAZI!
Ingekuwa ni ishu binafsi ningepongeza. Lakini kwenye hili Rais SSH alipaswa afanye kisera zaidi!
Hapo kasaidia tu mtoto mmoja... Je wapo wangapi kama huyo mtoto?
Je, nao watoke kokote walipo waende kwenye mikutano ya SSH kusuburia bahati zao?
Kwani anashindwa nini kutoa maelekezo ya kisera huyo akasaidiwa na wengine kote nchini nao wakatafutwa na kusaidiwa?
Unaelewa maana ya upendeleo? Wewe umefanya nini kuwasaidia hao unao waona huko kwako? Acheni wivu na roho mbaya.kwa hiyo ulitaka asumsaidie mtoto huyo? Vipi angekuwa mtoto wako ndio kasaidiwa? Ungekuja kuzubgumza maneno hayo uliyoyazungumza hapa?
 
Bila kumsahay yule mama.

Pili Rais ametoa wito Kwa jamii kuwa na bima ya Afya vinginevyo majanga kama hayo yakiwakuta wasije lauku Rais.
Ni kweli kabisa alipokuwa Mlowo napo amegusa hisia za watu wengi sana .kwa yule mama mwenye mtoto pamoja na yule aliyepata majereha mabaya kwa ajali. Kiufupi ni kuwa Rais Samia anaendelea kumfikia kila mwenye kuhitaji msaada
 
Unaelewa maana ya upendeleo? Wewe umefanya nini kuwasaidia hao unao waona huko kwako? Acheni wivu na roho mbaya.kwa hiyo ulitaka asumsaidie mtoto huyo? Vipi angekuwa mtoto wako ndio kasaidiwa? Ungekuja kuzubgumza maneno hayo uliyoyazungumza hapa?
Hii ni zaidi ya wivu... Ni UPENDELEO wa wazi!
Anyways, unaweza kuweka bayana vigezo vilivyotumika kumpa huyo mtoto hiyo nafasi huku wengine nchi nzima hawajui hatma yao?

Use your brain wisely if at all you have it!
 
Back
Top Bottom